JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
Naibu Katibu Mkuu Jumuiya ya Wafanyabiashara wa Mkoa wa Dar es Salaam, Muliro amesema: “Changamoto ya Kariakoo chanzo ni Bandarini kwenye kitengo cha Forodha, pale mifumo ya kodi si rafiki, ukitaja thamani ya kodi halisi hauwezi kutoa mzigo.
Kinachofuata unashirikiana na makamishna wa Forodha mnadanganya kwa pamoja, mfano mzigo wa Tsh. Milioni 300 mnasema una thamani ya Tsh. Milioni 80, hivyo ukishadanganya Bandarini ukija kwenye soko unashindwa kuandika uhalisia kwenye Mashine ya EFD, matokeo yake inatokea kamatakamata.
Tumeshafikisha malalamiko kwa Waziri wa Fedha na Waziri wa Viwanda lakini ni kama wanamtesa Rais kwa kuwa hawamsaidii ipasavyo.
Serikali irudi Bandarini ikaboreshe, sasa hivi Afisa wa Kodi anaweza kuamka akasema hana hela, akiingia mtaani kwenye kamatakamata hawezi kukosi si chini ya Tsh. Milioni 5