Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 128,308
- 245,426
Nimepita Mbagala wiki hii nikielekea kwenye Shamba langu Mkuranga, Hakika Mbagala ni Nchi nyingine kabisa, Utaratibu wao wa kuishi ni tofauti kabisa na Utaratibu wa Tanzania.
Wamachinga wamepanga bidhaa kuanzia kwenye milango ya maduka ya watu hadi katikati ya Barabara bila wasiwasi wowote, Wala hawaogopi hata milango ya Benki! yaani ni kama Mbagala haina serikali yoyote ile na ni kama hakuna mgambo wala polisi, Kumbukeni hawa Wamachinga hawalipi kodi yoyote ile, Ugali wa Mama Lishe unasongewa barabarani na magari yanasubiri msongaji amalize ndio yapite, Hili kwangu ni jambo la Ajabu mno!
Marafiki zangu wa kihindi wanaofanya biashara eneo hilo nilipowahoji kuhusu hali hiyo wamenieleza kwamba wanatishwa kulogwa ikiwa watafanya kampeni yoyote ya kuwazuia walioziba Milango yao!
Taarifa za chini chini zinaeleza kwamba Meya wa Eneo hilo, ambaye anatajwa kutisha kwa Ushirikina ndiye mlinzi wa Kwanza wa mambo hayo, anaunga mkono kila uchafu wa Wamachinga bla kujali athari zake, Kimsingi Wafanyabiashara wa Mbagala wanachosubiri ni kudura za Mungu, Hali yao ni mbaya kuliko nilichoandika.