Wafanyabiashara Halali wa Mbagala wanawezaje kulipa kodi ikiwa Wamezibwa 100% na Wamachinga?

kuna Cartel kubwa sana hapo: Kuna wa fanya biashara wakubwa wanawapa mzigo wamachinga wauze ili kukwepa kodi maana wamachinga hawatoi risiti. Hao madiwani na viongozi wa mitaa washawekwa mifukoni mwa hao wafanyabiashara hivyo hutaona cha mgambo wala askari.
 
Bongo tunaishi kama mashetani. Maendeleo huwa yanakuja na vilio ni vyema Serikali ikapangilia miundombinu wakati huu kuliko kusubiri ongezeko liwe kubwa zaidi.

Kuna raha yake jiji likipangiliwa vizuri.
 
Kuna kariakoo pia Yani ni kero kabisaaa,Watu na majiko wanapika ugali,Wanakaanga chips,sambusa,mihogo,wanapika Tena chini ya transforma!!!
Bado wauza kahawa,mishikaki wanatembea na majiko yao ndani ndani kwenye maduka ktk maghorofa. Na zaid mavyakula yanauzwa hovyo watu wanaumwa tumbo na kuharisha(Nimeshuhudia na wengi nawajua inawatokea baada ya kula)

Yani kkoo kushakua Sasa ni pahovyo mnoo.
Ajabu mkuu wa mkoa na team yake wanashindwa kuona haya machache!Basi hebu wazibiti matumizi holela ya moto kkoo na hao machinga wawapange basi daah
 
Kkoo mtu chini ya transforma Tena mbele ya duka la mtu kaweka Banda la chipsi,anachoma mihogo,vitumbua.Usalama uko wapi namna hii?
Kweli ghafla moto ukamate,si wenye maduka washapoteza mali zao.
Mamlaka husika watolee macho,Bora wasisitize ujengaji wa migahawa na hotel ambazo wataeza kuzicontrol.
Naunga mkono wamachinga kujitafutia vipato vyao ila wapangwe vizuri na wamachinga wa upishi barabarani hapana kabisa
 
Uzuri wa Mbagala vitu ni bei chee, Kuna nyanya za 200, mboga mboga fungu 300, maisha ya kule ni rahisi mno
 
Chadema baada ya wamachinga kuwapiga chini Sasa mshawageuza maadui
 
Baada ya wewe kuandika haya utawasaidia kwa lipi!
 
Mkuu hebu jaribu siku moja kupita Mbagala, hakuna serikali kabisa!
Mbagala ni kero.
Usisahau na uhalifu upo hadharani, wale wa minada fake njia ya Chamanzi. Wanaonwa hawakamatwi.
Siwezi kulea mtoto wangu au kuishi huko Mbagala.
 
Serikali ime-collapse siku nyingi. Kipande kidogo cha serikali kilichobaki wima ni kile kinachohusika na uuaji, utesaji, ukandamizaji na propanda ili watawala wachache waendelee kufaidi. Iko siku kila mtu ataelewa maana ya maneno haya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…