Wafanyabiashara jipangeni malalamiko yenu yaeleweke, na pia mtimize wajibu wenu

Yoda

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2018
Posts
48,475
Reaction score
70,102
Nimeyasoma madai ya wafanyabiashara yanayouzunguka mtandaoni(ambayo yaka kama 14) na nimeona mengi hayana mashiko, hayaeleweki au ni vigumu kutekelezeka. Halafu madai ni mengi mno kiasi kwamba inakuwa vigumu kofocus kwenye mambo yapi ni muhimu. Pia kuna mambo yanawahusu wafanyabiashara wenyewe kutimiza wajibu ambayo nayo lazima yazingatiwe na wafanyabiashara

Ili kujikita katika mambo muhimu iltakiwa haya yadaiwe, yafanyike au yatekelezwe;

1. VAT upande Tanzania bara ipunguzwe kuwa 15% kama ilivyo Zanzibar

2. Winga na wamachinga wanouza barabarani mbele ya maduka/fremu hasa Kariakoo waondolewe.

3. Wafanyabiashara WOTE mtoe risiti halali kwa wateja

Madai yasiyo na mashiko ni kama haya;
1. Service levy itolowe- Kwa nini mnataka itolewe
2. Kodi ya TV- hii itakuwa imewekwa kwa sababu ya ugumu wa kukusanya kodi ya sanaa nchi hii
3. Faini iwe kama kwenye magari- Hili haliwezekani kwa sababu mapato ya gari yanafahamika kutokana na idadi ya siti lakini mapato ya duka huwa yanabadilika sana
4. Kodi zote ziwe kapu moja- Hili haliwezekani, duniani kote huwa kuna mamlaka tofauti ya kutoza kodi
5. Risiti sio kodi- Hili ni dai la kijinga, risiti lazima zitolewe kwa wateja
6. Ukomo wa kodi ya makadirio- Hili ni dai la kijinga, makadirio lazima yaendane na ukubwa wa biashara.

Madai mengi mengi ya kamatakamata, hesabu kukataliwa n.k ni masuala ya utendaji zaidi wa TRA, mamlaka nyingine za udhibiti na pia mfumo mzima wa biashara usio na mazingira rafiki ambao unahitaji mabadiliko makubwa ya kimfumo, sera, utendaji na usimamizi kwa kuhusisha wadau wengi.
 
Uko sahihi, binafsi nimeyaona lakini inaonekana pamoja na madai yao yamsingi hawakujipanga na hakuna watu smart kati yao wanaoweza kuwashauri yapi yamsingi wayawekembele.

Shida ya Watanzania wengi wetu tunapenda Sana oyaoya, kufuata mkumbo na ushabiki bila kutafakari mambo Kwa akili yako iliyohuru matokeo yake wengi tunakuwa oyaoya - HAPA NDIPO WANASIASA WANATUWAHI NA KUKAA MBELE KWENYE KILA JAMBO LETU.
 
Nimeyasoma madai ya wafanyabiashara yanayouzunguka mtandaoni(ambayo yaka kama 14) na nimeona mengi hayana mashiko, hayaeleweki au ni vigumu kutekelelezeka. Halafu madai ni mengi mno kiasi kwamba inakuwa vigumu kofocus kwenye mambo yapi ni muhimu. Pia kuna mambo yanawahusu wafanyabiashara wenyewe kutimiza wajibu ambayo nayo lazima yazingatiwe na wafanyabiashara

Ili kujikita katika mambo muhimu iltakiwa haya yadaiwe, yafanyike au yatekelezwe;

1. VAT upande Tanzania bara ipunguzwe kuwa 15% kama ilivyo Zanzibar

2. Winga na wamachinga wanouza barabarani mbele ya maduka/fremu hasa Kariakoo waondolewe.

3. Wafanyabiashara WOTE mtoe risiti halali kwa wateja
Upo sawa boss.
Madai yasiyo na mashiko ni kama haya;
1. Service levy itolowe- Kwa nini mnataka itolewe
Iunganishwe kwenye kodi za leseni. Mamlaka ni nyingi mno boss. Umetoka kufanya kikao na wcf, Levy hawa hapa umemaliza halmashauri hawa hapa.
2.Kodi ya TV- hii itakuwa imewekwa kwa sababu ya ugumu wa kukusanya kodi ya sanaa nchi hii
Upo sawa.
3. Faini iwe kama kwenye magari- Hili haliwezekani kwa sababu mapato ya gari yanafahamika kutokana na idadi ya siti lakini mapato ya duka huwa yanabadilika sana
Upo sawa
4.Kodi zote ziwe kapu moja- Hili haliwezekani, duniani kote huwa kuna mamlaka tofauti ya kutoza kodi
Si lazima ziwe kapu moja ila mifumo isomane kodi ilipwe sehemu chache wareconcile huko ndani kwa ndani, serikali si ni moja?.

Mkuu, kuna Witholding Tax, VAT, PAYE na SDL, WCF zote zinahitaji compliance n compliance ni gharama. Nakukusanyia VAT nikichelewa kuleta unanipiga fine, mimi napata nini kuwa wakala wako?

Mtu ana mtaji wa M400 wa mkopo unaohitaji umakini wa makusanyo bado tena unampa kazi ya kutafuta mwasibu mara ashirikiane na TRA wasio waaminifu tunaumizana huo ndo uhalisia.
5.Risiti sio kodi- Hili ni dai la kijinga, risiti lazima zitolewe kwa wateja
Naunga mkono hoja.
6. Ukomo wa kodi ya makadirio- Hili ni dai la kijinga, makadirio lazima yaendane na ukubwa wa biashara.
Naunga mkono hoja
 
90% ya wafanyabiashara wa Kariakoo ni Wakinga na wengi wao ni la 7 ila Wana mitaji mikubwa

Unaweza kukuta hayo malalamiko wameandikiwa na Mfalme wao Jah people 😂😂
 
Upo sawa boss.

Iunganishwe kwenye kodi za leseni. Mamlaka ni nyingi mno boss. Umetoka kufanya kikao na wcf, Levy hawa hapa umemaliza halmashauri hawa hapa.

Si lazima ziwe kapu moja ila mifumo isomane kodi ilipwe sehemu chache wareconcile huko ndani kwa ndani, serikali si ni moja?.

Mkuu, kuna Witholding Tax, VAT, PAYE na SDL, WCF zote zinahitaji compliance n compliance ni gharama. Nakukusanyia VAT nikichelewa kuleta unanipiga fine, mimi napata nini kuwa wakala wako?

Mtu ana mtaji wa M400 wa mkopo unaohitaji umakini wa makusanyo bado tena unampa kazi ya kutafuta mwasibu mara ashirikiane na TRA wasio waaminifu tunaumizana huo ndo uhalisia.
Ingeeleweka kama wangelalamikia viwango vya kodi, malalamiko ya kwamba vyombo vya ukusanyaji ni vingi hayana mashiko sana.

Service levy, Withholding Tax, VAT na PAYE huwezi kuzichanganya pamoja
SDL, WCF na vibali vya OSHA zinaweza kuchangwa pamoja
Leseni ya biashara kote duniani lazima ulipie, hii labda ndio inaweza kuchanganywa na ada ya zimamoto. Ukilipia leseni ya biashara ijumuishe zimamoto.
 
Ndo nachosema boss, ziwe grouped kurahisisha, si rahisi kudeal na haya mambo, assume mshahara wako ungekuwa unapewa wote halafu wewe ndo ulipe Paye na NSSF na kutuma report kwa TRA ukichelewa Fine.

Hayo unayosema huwezi yaweka pamoja yote yanahitaji compliance kwa tarehe tofauti na zikichelewa one minute penati inaingia. Anayefanya hivyo na yeye analipa kodi yake kama wengine waliopo kwenye ajira na siasa. Kwanini anayeifanya hiyo kazi bure kwa gharama zake asitengenezewe mazingira rafiki?

Agency ziwe chache, Almashauri na TRA, watoto wao wote waingie humo wafanye reconcilliation zao.
 
Nimeyasoma madai ya wafanyabiashara yanayouzunguka mtandaoni(ambayo yaka kama 14) na nimeona mengi hayana mashiko, hayaeleweki au ni vigumu kutekelezeka. Halafu madai ni mengi mno kiasi kwamba inakuwa vigumu kofocus kwenye mambo yapi ni muhimu. Pia kuna mambo yanawahusu wafanyabiashara wenyewe kutimiza wajibu ambayo nayo lazima yazingatiwe na wafanyabiashara

Ili kujikita katika mambo muhimu iltakiwa haya yadaiwe, yafanyike au yatekelezwe;

1. VAT upande Tanzania bara ipunguzwe kuwa 15% kama ilivyo Zanzibar

2. Winga na wamachinga wanouza barabarani mbele ya maduka/fremu hasa Kariakoo waondolewe.

3. Wafanyabiashara WOTE mtoe risiti halali kwa wateja

Madai yasiyo na mashiko ni kama haya;
1. Service levy itolowe- Kwa nini mnataka itolewe
2.Kodi ya TV- hii itakuwa imewekwa kwa sababu ya ugumu wa kukusanya kodi ya sanaa nchi hii
3. Faini iwe kama kwenye magari- Hili haliwezekani kwa sababu mapato ya gari yanafahamika kutokana na idadi ya siti lakini mapato ya duka huwa yanabadilika sana
4.Kodi zote ziwe kapu moja- Hili haliwezekani, duniani kote huwa kuna mamlaka tofauti ya kutoza kodi
5.Risiti sio kodi- Hili ni dai la kijinga, risiti lazima zitolewe kwa wateja
6. Ukomo wa kodi ya makadirio- Hili ni dai la kijinga, makadirio lazima yaendane na ukubwa wa biashara.

Madai mengi mengi ya kamatakamata, hesabu kukataliwa n.k ni masuala ya utendaji zaidi wa TRA, mamlaka nyingine za udhibiti na pia mfumo mzima wa biashara usio na mazingira rafiki ambao unahitaji mabadiliko makubwa ya kimfumo, sera, utendaji na usimamizi kwa kuhusisha wadau wengi.
Una bilioni ngapi kwenye account yako? Tuache ujuaji tuwasikilize wafanyabiashara
 
Utitiri wa kodi,
 
Kama huna biashara ya mtaji mkubwa ni bora ukae kimya. Huwezi kuja kuongelea mambo yasiyokuhusu.
 
Ndo nachosema boss, ziwe grouped kurahisisha, si rahisi kudeal na haya mambo, assume mshahara wako ungekuwa unapewa wote halafu wewe ndo ulipe Paye na NSSF na kutuma report kwa TRA ukichelewa Fine.

Hayo unayosema huwezi yaweka pamoja yote yanahitaji compliance kwa tarehe tofauti na zikichelewa one minute penati inaingia. Anayefanya hivyo na yeye analipa kodi yake kama wengine waliopo kwenye ajira na siasa. Kwanini anayeifanya hiyo kazi bure kwa gharama zake asitengenezewe mazingira rafiki?

Agency ziwe chache, Almashauri na TRA, watoto wao wote waingie humo wafanye reconcilliation zao.
Duniani kote reconciliation ni kazi ya mfanyabiashara mwenyewe. Kama huwezi ajiri mtu anayejua kodi vizuri.
Kama mfanyabiashara anazo rekodi za risiti na nyaraka nyingine muhimu za kibiashara reconciliation, ulipaji na uwasilishaji wa kodi tena kwa muda sahihi kwa TRA haiwezi kuwa tatitizo hata kidogo. Tatitizo ni kwamba wafanyabiashara wengi hawataki kufanya biashara kwa kuwa mfumo wa risiti na kutunza rekodi ili wakwepe kodi.
 
Una bilioni ngapi kwenye account yako? Tuache ujuaji tuwasikilize wafanyabiashara
Kama mfanyabiashara anazo rekodi za risiti na nyaraka nyingine muhimu za kibiashara ulipaji na uwasilishaji wa kodi tena kwa muda sahihi kwa TRA haiwezi kuwa tatitizo hata kidogo. Tatitizo ni kwamba wafanyabiashara wengi hawataki kufanya biashara kwa kuwa mfumo wa risiti na kutunza rekodi ili wakwepe kodi.
 
Kama huna biashara ya mtaji mkubwa ni bora ukae kimya. Huwezi kuja kuongelea mambo yasiyokuhusu.
Kodi inanihusu, kuna wafanyabiashara matapeli wengi sana hawatoi risiti kabisa au wanatoa risiti za kijanja.
 
Back
Top Bottom