Wafanyabiashara jipangeni malalamiko yenu yaeleweke, na pia mtimize wajibu wenu

Wafanyabiashara jipangeni malalamiko yenu yaeleweke, na pia mtimize wajibu wenu

Madai yasiyo na mashiko ni kama haya;
1. Service levy itolowe- Kwa nini mnataka itolewe
Service levy kwa sisi wafanyabiashara sio issue sana ila usumbufu wake sasa, sijui utoe risiti ucaclulate, then uende mpaka ofisi ya jiji kule ukapange foleni, sometime unapoteza siku nzima, inshort hii kodi wafanyakazi wa jiji hadi wanaosimamia usafi ambao hata haiwahusu wanaitumia kama kichaka cha kuwaomba Rushwa wafanyabiashara, kuna Dai jengine lina sema kodi zijumuishwe, idumbukizwe huko.
2.Kodi ya TV- hii itakuwa imewekwa kwa sababu ya ugumu wa kukusanya kodi ya sanaa nchi hii
3. Faini iwe kama kwenye magari- Hili haliwezekani kwa sababu mapato ya gari yanafahamika kutokana na idadi ya siti lakini mapato ya duka huwa yanabadilika sana
Faini ya sasa ni 1.5M+ sometime 3M+ usipotoa risiti, na kuna tetesi wanataka waiongeze. definition ya kutotoa risiti ni pana sana, anaweza akapita Afisa Tra akawaSha Machine yako ambayo asubuhi ilikua inafanya kazi ila for some reason imegoma mchana, kama jana yake ni jpili ama huku toa Z report anahesabu umekaa na machine mbovu zaidi ya masaa 24 unaandikiwa ulikua unauza bila kutoa risiti,

Mimi binafsi nilipigwa fine ya kutotoa risiti kwa kosa la kuchelewa ku update machine, unakuta makadirio ya mwaka 1m ila fine zaidi ya makadirio ya mwaka haimake sense kabisa.
4.Kodi zote ziwe kapu moja- Hili haliwezekani, duniani kote huwa kuna mamlaka tofauti ya kutoza kodi
Ila zinaweza kulipwa pamoja, mfanya biashara wa Kariakoo ni one man army, aamke saa 11 asubuhi awahi dukani sometime hadi usiku yupo dukani, anapata wapi muda wa kupanga foleni kila ofisi? Nini kinawashinda Serikali kutengeneza Wallet ama njia ya malipo ikaunganishwa na Tin no? Ikajumuisha madeni yako yote ukawa unalipa pamoja? Just imagine kwa siku unaingiza laki na kitu ila sababu ya kikodi kisicho na mbele wala nyuma uache kazi siku hio upange foleni kulipa 20,000.
5.Risiti sio kodi- Hili ni dai la kijinga, risiti lazima zitolewe kwa wateja
Hili suala niliwahi kuliongelea uzi mwengine, mfanyabiashara unakuta hatoi risiti mizigo yote ila still kodi anayo lipa ni hata 40% ya kipato chake, kuna watu wanalia humu kila siku, maoni yangu binafsi watoe kodi kwa wafanyabiashara wa kawaida waweke Tozo, watengeneze database ya bidhaa mfano Tozo ya pochi 1,000 umeuza pochi 10 kwa siku basi kuwe na 10,000 ya serikali ikiwezekana ilipwe siku hio hio kupitia wallet ya serikali.

Hali ya sasa wafanyabiashara wanaumia hasa wenye frame, unapewa mzigo kwa 98,000 unauza 100,000 faida yako ni 2000 ila ukitoa Risiti kule Tra inasoma 100,000 na unatakiwa uilipie kodi ambayo ni zaidi ya serikali inayotakiwa kuchukua sababu kodi halali ilitakiwa ikatwe kwenye 2,000. kutokana na udogo wa biashara na kutokuwa na mahesabu ya VAT plus mapapa wenye mizigo kuwapa maduka mizigo bila risiti hali ya mfanyabiashara wa frame inakua ngumu.
6. Ukomo wa kodi ya makadirio- Hili ni dai la kijinga, makadirio lazima yaendane na ukubwa wa biashara.

Madai mengi mengi ya kamatakamata, hesabu kukataliwa n.k ni masuala ya utendaji zaidi wa TRA, mamlaka nyingine za udhibiti na pia mfumo mzima wa biashara usio na mazingira rafiki ambao unahitaji mabadiliko makubwa ya kimfumo, sera, utendaji na usimamizi kwa kuhusisha wadau wengi.
Kifupi mkuu hapo vimeandikwa tu kwa shortcut kila mtu ana tabu zake, tuache kukopi mifumo ya Ulaya tu innovate kutokana na hali zetu, tupanue wigo wa kodi kwa kuhakiki Sha watu wengi zaidi wanalipa kodi badala kung'ang'ania wachache wanaolipa walipe kingi zaidi.
 
Hii haiapaswi kuwa hoja ya msingi kama unatoa risiti na kutunza rekodi, hoja ya msingi inapaswa kuwa ukubwa wa kodi.

Kingine makusanyo ya Kodi yananunua magari ya Mawaziri hayawasaiidii wafanyabiashara kutafuta masoko wala kukuza mitaji.

Hakuna kiwango maalum cha kodi kwa kila duka inasababisha usumbufu sana
 
Service levy kwa sisi wafanyabiashara sio issue sana ila usumbufu wake sasa, sijui utoe risiti ucaclulate, then uende mpaka ofisi ya jiji kule ukapange foleni, sometime unapoteza siku nzima, inshort hii kodi wafanyakazi wa jiji hadi wanaosimamia usafi ambao hata haiwahusu wanaitumia kama kichaka cha kuwaomba Rushwa wafanyabiashara, kuna Dai jengine lina sema kodi zijumuishwe, idumbukizwe huko.
Hapa mngesema service levy ilipwe Halmashauri kwa njia ya mtandao, nakubaliana na wewe kwamba mambo ya kwenda kupanga foleni kwenye ofisi za mtaa au kijiji kufanya malipo yamepitwa na wakati.
 
Duniani kote reconciliation ni kazi ya mfanyabiashara mwenyewe. Kama huwezi ajiri mtu anayejua kodi vizuri.
Si kweli, sisi ndo tumeamka sasa hivi VAT reconciliation hafanyi mfanyabiashara, mfumo unafanya. Huitaji mhasibu kuchukua risiti za mauzo na manunuzi tena, ukinunua kwa risiti ukauza kwa risiti system yenyewe inajireconcile unapewa assesment. Wenzetu wapo mbali zaidi. Mifumo inasomana, si rahisi kukwepa kodi na ukiikwepa ni rahisi kutambulika sababu kazi za reconciliation si za mfanyabiashara. Kazi yake ni kuhakiki iwapo notice ipo sawa.

Mtu ana mzunguko wa M200 haitaji mhasibu, anahitaji karani tu. Mifumo ikiwa sawa ikasomana karani anafanya yote hayo na serikali itapokea kodi bila shida. Kwanza below 500M hata mahesabu hatakiwi kulazimisha kutengeneza.
Kama mfanyabiashara anazo rekodi za risiti na nyaraka nyingine muhimu za kibiashara reconciliation, ulipaji na uwasilishaji wa kodi tena kwa muda sahihi kwa TRA haiwezi kuwa tatitizo hata kidogo.
Mifumo ikisomana ndo hakuna tatizo, nimekupa mfano, Huitaji mhasibu kufanya VAT reconciliation, ukinunua kwa risiti ukauza kwa risiti system yenyewe inajireconcile unapewa assesment.
Tatitizo ni kwamba wafanyabiashara wengi hawataki kufanya biashara kwa kuwa mfumo wa risiti na kutunza rekodi ili wakwepe kodi.
Mifumo tu. Ukishakuwa na mfumo unaotoa kodi halali watu watalipa. Sio mifumo wa kuangalia mzunguko bank ulazimishie kodi hapo wakati kuna watu wanaazima hadi pesa waweke bank wakopesheke.
 
Faini ya sasa ni 1.5M+ sometime 3M+ usipotoa risiti, na kuna tetesi wanataka waiongeze. definition ya kutotoa risiti ni pana sana, anaweza akapita Afisa Tra akawaSha Machine yako ambayo asubuhi ilikua inafanya kazi ila for some reason imegoma mchana, kama jana yake ni jpili ama huku toa Z report anahesabu umekaa na machine mbovu zaidi ya masaa 24 unaandikiwa ulikua unauza bila kutoa risiti,

Mimi binafsi nilipigwa fine ya kutotoa risiti kwa kosa la kuchelewa ku update machine, unakuta makadirio ya mwaka 1m ila fine zaidi ya makadirio ya mwaka haimake sense kabisa.
Mkuu sasa hapa mlitakiwa kuishauri serikali ni kwa namna gani hasa itadhibiti ukwepaji kodi kwa kutotoa risiti kunakofanywa na wafanyabiashara kwa sababu ukweli ni kwamba wafanyabiashara wengi hasa kariakkoo hawatoi risiti stahiki, mashine za risiti wanakaa nazo kama mapambo tu na kuzugia.
 
Kama mfanyabiashara anazo rekodi za risiti na nyaraka nyingine muhimu za kibiashara ulipaji na uwasilishaji wa kodi tena kwa muda sahihi kwa TRA haiwezi kuwa tatitizo hata kidogo. Tatitizo ni kwamba wafanyabiashara wengi hawataki kufanya biashara kwa kuwa mfumo wa risiti na kutunza rekodi ili wakwepe kodi.
Mimi nafikiri pia kuna changamoto ya elimu ya kikodi, kibiashra na pia changamoto ya kupata wataalamu wazuri wa masuala ya biashara na kodi.

Japo kuna issue ya mazoea ya muda uliopita ukiongezea na ukuaji wa teknolojia kurahisisha TRA kufuatilia kwa karibu.
 
Mimi nafikiri pia kuna changamoto ya elimu ya kikodi, kibiashra na pia changamoto ya kupata wataalamu wazuri wa masuala ya biashara na kodi.
Hakuna tatizo la elimu ya kodi Tanzania hasa kwa wafanyabiasha wa kati na wakubwa, ukweli ni kwamba hao wafanyabiashara wanajua vizuri kodi inavyopaswa kulipwa. Tatizo ni ukubwa wa kodi, mfumo mbovu wa kulipa baadhi ya kodi ukwepaji makusudi wa kodi, matumizi mabaya ya kodi na upangiliaji mbovu wa biashara wa kuwaweka wamachinga na wenye maduka/fremu pamoja ndio vinaleta shida zote hizi.
 
Duniani kote reconciliation ni kazi ya mfanyabiashara mwenyewe. Kama huwezi ajiri mtu anayejua kodi vizuri.
Kama mfanyabiashara anazo rekodi za risiti na nyaraka nyingine muhimu za kibiashara reconciliation, ulipaji na uwasilishaji wa kodi tena kwa muda sahihi kwa TRA haiwezi kuwa tatitizo hata kidogo. Tatitizo ni kwamba wafanyabiashara wengi hawataki kufanya biashara kwa kuwa mfumo wa risiti na kutunza rekodi ili wakwepe kodi.
Tatizo linaakuja kwenye mfumo mzima wakodi .jinsi unavyoondelea kutoa risit unavyokabwa na kodi
 
Nimeyasoma madai ya wafanyabiashara yanayouzunguka mtandaoni(ambayo yaka kama 14) na nimeona mengi hayana mashiko, hayaeleweki au ni vigumu kutekelezeka. Halafu madai ni mengi mno kiasi kwamba inakuwa vigumu kofocus kwenye mambo yapi ni muhimu. Pia kuna mambo yanawahusu wafanyabiashara wenyewe kutimiza wajibu ambayo nayo lazima yazingatiwe na wafanyabiashara

Ili kujikita katika mambo muhimu iltakiwa haya yadaiwe, yafanyike au yatekelezwe;

1. VAT upande Tanzania bara ipunguzwe kuwa 15% kama ilivyo Zanzibar

2. Winga na wamachinga wanouza barabarani mbele ya maduka/fremu hasa Kariakoo waondolewe.

3. Wafanyabiashara WOTE mtoe risiti halali kwa wateja

Madai yasiyo na mashiko ni kama haya;
1. Service levy itolowe- Kwa nini mnataka itolewe
2. Kodi ya TV- hii itakuwa imewekwa kwa sababu ya ugumu wa kukusanya kodi ya sanaa nchi hii
3. Faini iwe kama kwenye magari- Hili haliwezekani kwa sababu mapato ya gari yanafahamika kutokana na idadi ya siti lakini mapato ya duka huwa yanabadilika sana
4. Kodi zote ziwe kapu moja- Hili haliwezekani, duniani kote huwa kuna mamlaka tofauti ya kutoza kodi
5. Risiti sio kodi- Hili ni dai la kijinga, risiti lazima zitolewe kwa wateja
6. Ukomo wa kodi ya makadirio- Hili ni dai la kijinga, makadirio lazima yaendane na ukubwa wa biashara.

Madai mengi mengi ya kamatakamata, hesabu kukataliwa n.k ni masuala ya utendaji zaidi wa TRA, mamlaka nyingine za udhibiti na pia mfumo mzima wa biashara usio na mazingira rafiki ambao unahitaji mabadiliko makubwa ya kimfumo, sera, utendaji na usimamizi kwa kuhusisha wadau wengi.
Serikali yoteyote corrupt ina sumbua kwenye kodi! Inambana mwananchi!
Hapo bado tozo
 
Kodi inanihusu, kuna wafanyabiashara matapeli wengi sana hawatoi risiti kabisa au wanatoa risiti za kijanja.
Kwenye huu mgomo kama tatizo lako ni risiti tu. Bila shaka unafanya hoja yangu iwe na nguvu zaidi mchango wako utakuwa mdogo sana kwenye tatizo zima na ni bora usikilize, ujifunze halafu unaweza kurudi kuchangia ukiwa na madini lakini kwa hoja zako za mwanzoni unaoneka hujui chochote kuhusu biashara za mitaji mikubwa na mahusiano yao (wafanyabiashara) na TRA, Halmashauri, hizo taasisi nyingine kama WCF, OSHA, Zimazoto na kadhalika.
 
Sema tu labda hawajajiandaa kuelezea ila kkoo km una frem unaweza kuikimbia maana kuna kipindi wakusnya hela ni wengi akitoka huyu anaingia huyu mpaka unajiuliza kwani hawa si wanakusanya hela yote ni ya serikali kwa nn wasiunganishe ulioe hata sehem tatu ama mbili basi.
 
Back
Top Bottom