Wafanyabiashara Kariakoo wanapata hasara kwa kutokujua kiwango cha kubadilishia pesa cha dola kwenda Yuan au shilingi kwenda Yuan

Wafanyabiashara Kariakoo wanapata hasara kwa kutokujua kiwango cha kubadilishia pesa cha dola kwenda Yuan au shilingi kwenda Yuan

Mwande na Mndewa

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2021
Posts
1,117
Reaction score
3,153
Mfanyabiashara unaweza kupata taarifa ya viwango vya kubadili fedha kupitia simu yako, una-google, kutembelea mabenki n.k lakini cha muhimu zingatia utofauti wa kiwango cha kubadilishia fedha hiyo, Wafanyabiashara wengi mwanzo wa mwaka hadi mwisho wa mwaka anakuwa haelewi kwa sababu hajui viwango vya kubadili shilingi kwenda Yuan, mfano ukimpigia simu mchina kule China kwa whats up call unaulizia bei ya 3pcs ya Pazia atakwambia ni Yuan 100 kwa haraka haraka unachukua Yuan 100 unazidisha kwa rate ya leo ya Yuan kwenda shilingi ambayo ni 356 mahesabu yatakuwa hivi (100 × 356) sawa na shilingi 35,600 kwa hapa Tanzania basi utaongeza ongeza kodi na gharama zako za usafiri utauza 70,000 huku Tanzania, huu ni mfano tu.

Pesa ya China Yuan au kwa jina lingine RMB AU CNY kwa sasa inaanza kutumiwa sana na Wafanyabiashara kwa sasa kutokana na upungufu wa dola uliopo, rate ya leo ya dola ni 2386 ili kupata rate ya Yuan unagawanya kwa 6.7 ( rate ya mtaani) au 6.9 (rate ya mtandaoni) ambayo ni rate kubadili Yuani kwenda dola ukiwa China, 2386 ÷ 6.7 = 357 au 2386 ÷ 6.9 = 346 haya ni mahesabu ya kupata rate ya shilingi kwenda Yuan (RMB,CNY) ukiwa na shilingi 238,600,000 unagawanya na 357 kupata hela ya China Yuan, mahesabu yatakuwa hivi 238,600,000 ÷ 357 = 668,348 Yuan. Nimetoa mfano wa 238,600,000 kwa sababu ni sawa na dola 100,000 ambayo ukiwa China kupata Yuan itabidi utumie rate ya China kutoka dola kwenda Yuan, mahesabu yatakuwa hivi 100,000 × 6.87 = 687,000 Yuan,utofauti na hasara huwa zinaanzia hapa,ukichukua Yuan 687,000 - 668,348 = 18,652 Yuan ,utofauti wa shilingi 18,652 kuibadili iwe shilingi mahesabu yanakuwa hivi Yuan 18,652 × 357(rate) = 6,658,764 hii ndio hasara unayokula kwenye rate tu unapobadili hela kabla ya kununua mzigo, Rejea mifano ifuatayo;-

2390 ÷ 6.9 = 347
2386 ÷ 6.9 = 346
2380 ÷ 6.9 = 345
Hasara 2386 × 6.7 = 357

USD 100,000 × 6.87 = 687,000
TZS 238,600,000 ÷ 357 = 668,348 ( kumbuka 2386 ÷ 6.7 = 357 so rate ya 357 ni sawa na 6.7)
Yuan 687,000 - 668,348 Yuan = 18,652 Yuan
Yuan 18,652 × 357 = 6,658,764 Shilingi (Hasara)
Dola kwenda Yuan,
2386 ÷ 345 = 6.89
2386 ÷ 357 = 6.7
Sasa Dola 100,000 × 6.89 = 689,000
Dola 100,000 × 6.7 = 670,000
Tofauti ni = 19,000 Yuan ( 19,000 × 357 = 6,783,000 Shilingi (hasara)
Nimalizie kwa kusema kwamba kiwango kizuri cha faida cha kubadili shilingi kuwa Yuan ni 345 au 346 ambacho ni sawa na 6.9 kwa China hela ya China Yuan inaongezeka,na kiwango cha 356 au 357 ambacho ni sawa na 6.7 kwa China ni hasara kwa mfanyabiashara,hela ya China Yuan inapungua.

Nikiishia hapa, Mimi ni
Msemakweli Chakubanga,
Dar es Salaam.
0755078854

-Bachelor of Business Administration in International Business.

-Master of Leadership and Management.

Recent Publications;-
-Assessment on the effect of Micro-Financing on Poverty Reduction.
 
Naona dola ya mmarekani mambo yashakuwa mengi..
 
Back
Top Bottom