Nyakijooga
JF-Expert Member
- Dec 9, 2018
- 276
- 473
Halmashauri ya Kibaha Mjini imeanzisha oparesheni kamata kamata na kufunga biashara tangu wiki iliyopita.
Wanafika kwenye sehemu za biashara wakikuta unadaiwa kiasi chochote kile wanakutoa kwenye biashara yako, wanafunga na makufuli makubwa na kukutka kwenda kuchukua Control Number ili ulipie, kiwango kikianzia Tsh. 70,000
Oparesheni hiyo inafanyika kwenye maduka kuanzia maeneo ya Kibaha Mili Moja kupanda hadi Shule ya Maili Moja Msingi, Kwa Mang'umbi, Tankini hadi Mitaa ya Muheza.
Kinachoniuma ni kuona wanafungia hadi biashara ndogondogo, mtu ana kifremu chake anatakiwa kwenda kulipia, hawataki kusikia maelezo ya aina yoyote ile.
Kinachoendelea sasa ni Watu kufunga biashara zao, wakiwakwepa maafisa wa Halmashauri, hivi Rais Samia si alipiga marufuku hii staili ya kufunga biashara kisa tu mtu au watu wanadaiw kodi fulani ya Serikali au watasema yale ni maneno ya Kisiasa?
Hivi kwani si Rais Samia alisema hakuna kufunga biashara kwa sababu za mambo kama hayo, kwa nini hawawapi nafasi Wafanyabiashara wakajieleza na kama ni kulipa walipe kwa ustaarabu.
Mtu ana kifrem chake kidogo kaweka cherehani, jamaa wanapiga kufuri na kumtaka alipe Shilingi 70,000 wakati yeye mwenyewe ukute hiyo hela anaipata baada ya mwezi kwa tenda zake za kushona kwa bukubuku au 500.
Majibu ya Halmashauri ~ Malalamiko ya Kufunga Maduka, Halmashauri ya Kibaya yasema “Wanafunga wenyewe, hatujafunga sisi"