DOKEZO Wafanyabiashara Kibaha tunaishi kama digidigi, tunawakimbia Halmashauri ambao wanafunga maduka yetu

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Kufunga Biashara sio Solution.
kwa kawaida leseni ni funguo ya kuanza kufanya biashara, kama hauna solution ya kwanza ni kupatiwa elimu na kusajiliwa mara moja ila kama hautoi ushirikiano kinachofuata ni kufungiwa hiyo biashara yako lengo la elimu ni kukupa muongozo wa utendaji wa hiyo biashara na hata ukipata hiyo leseni ukikiuka masharti afisa anahaki ya kukunyang'anya hiyo leseni
 
Ukifungia Biashara hata hicho kidogo hupati hebu fikiria vizuri.
 
Ni uelewa mdogo
 
Leseni ni fees sio kodi mnaweza hata kufanya shilingi 5000.
hata hiyo elfu tano unayosema watu hawatoacha kulalamika, kwa kawaida halmashauri nyingi zinatoza ushuru wa sokoni(vizimba) au ktk stendi za daladala 500/= lakini tazama wafanya biashara na hao makondakta wanavyolalamika
 
hata hiyo elfu tano unayosema watu hawatoacha kulalamika,
Watu wanacholalamika ni fedha wanazotoa kuibiwa kwenye Manispaa na Halmashauri.

Fees lazima ziwe Affordable ili kuwashawishi Watu wengi kufungua Biashara ili wakue wawe walipakodi wakubwa lakini kuwapiga mikwara na kuwafungia ni ninyi mnakosa na wao wanakosa huo sio ujinga kweli?!🤔
 
ubadhirifu wa fedha upo kigezo kikubwa tunaona hati chafu zinazotolewa na mkaguzi mkuu, lakini sio kigezo cha kutolipa kodi cha msingi ni kuwachagua viongozi imara watakao simamia vyema rasilimali zetu zikiwemo hizo kodi zetu zinazokatwa na hawa mabwana wa halmashauri na manispaa/majiji
 
Na huku mbeya mkuu na mbuga zetu, fukwe, visiwa vinauzwa na maduka wanafunga wanakusanya hela tu. Wakinyimana wanatumbuana
 
Vi
Hakuna kiongozi imara atatoka nje ya CCM mkuu viongozi imara watatoka ndani ya chama humo humo. Na hivyo hatuitaji kiongozi imara zaid ni taasis imara zitakazo simamia rasilimali zote za nchi. Na kiongozi mmoja
 
Lipa kodi tu , unataka sewage system nzuri , usafi , taka zizolewe n.k na laki tu ya kodi unazua. Tulipe kodi tujitegemee
 
Hii nchi ina Marais wangapi? Mama Samia si alipiga marufuku huu tabia ya kufunga biashara za watu?

Sasa unafunga biashara ya mtu hizo pesa za kuwalipa akazitowe wapi?

Kwanini wasitowe demand note ya mwezi mmoja?
Raisi hafiki kila kata ili tatizo la wateule kuanzia Rc,Dc na wakurugenzi
 
Leseni inatakiwa iwe bure ili kuondoa mzigo kwa wafanyabiashara.
Huyu ni mwanaCCM . Ni kipofu haoni ubaya wa CCM wala uzuri wa nchi.


Ukimuuliza makodi yote ya pango la nyumba nchi nzima na Zile za NHC miji yote Tanzania zinatumikaje hawezi akakupa jibu zaidi ya mama anaupiga mwingi bila kujua kuwa kuna pesa nyingi zinaliwa wa urefu wa kamba ya kila idara na wizara badala ya pesa zote kuingia hazina na kuondosha mianya ya upigaji kwa kufuta taratibu za kila idara kukusanya mapato na tozo halafu wafanye marumizi yao na zinazobaki ndio ziende hazina.
 
Nchi haina utaratibu wa kulea na kustawisha wafanyabiashara wa ndani.
Ilitakiwa mtu asajili biashara bure, tin bure na leseni bure.
Afanye biashara baada ya mwaka ndio apangiwe kulipia kodi, na leseni.
Kwa mazingira ya sasa ni ngumu kwa mfanyabiashara kustawi kwa kutumia mtaji wake,
ni awe na kona kona nyingi ili aweze kuishi.

Na ndio maana biashara ya kuuza nje hakuna, fedha za kigeni hakuna.
Hii ya kukusanya nyingi, na kutumia kwa wingi.
haitakaa uchumi wa nchi ukawa sawa, labda ccm itoke
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…