Wafanyabiashara ni wengi kuliko waajiriwa lakini watanzania wanaoishi angalau maisha standard waajiriwa ni wengi, Tuendelee kuponda ajira?

Gari sio liability ni basic need kwa mtu anaeweza kuligharamia bila kutikisika kiuchumi, gari litamsaidia kufika anakotaka kwa urahisi, kuokoa muda, kukaa comfortably, n.k.

Kwa akili yako wewe hata kujenga choo ni liability utakuwa unashusha kimba porini maana choo cha nyumbani hakikuingizii pesa
 
Ni kama umeandika point ila kuna kitu umesahau. Sio kila aliyejiajiri ni mfanyabiashara. Tofauti ya aliyejiajiri na aliyeajiriwa ni moja tu. Ni kwamba mmoja anajipangia mambo yake na mwingine anapangiwa na mwajiri wake. Ila wote kwa pamoja wanakula msoto. Tena yule aliyejiajiri kuna wakati anakula msoto mkali zaidi kwasababu asipoenda ofisini ndo kakosa riziki. Hakuna cha mshahara mwisho wa mwezi. Hili kundi la waliojiajiri ni kubwa mno nchini kuliko walioajiriwa.

Mfanyabiashara yeye anakuwa kashavuka hiyo hatua ya kujiajiri. Huyu anakuwa kafika stage ya kuajiri watu wengine kumfanyia kazi zake. Hata asipoenda ofisini kazi zinaendelea. Yaani kajiajiri na kuajiri. Kuna baadhi ya wafanyabiashara ili kutoingilia sana hesabu za kampuni huwa wanajipangia kabisa mshahara na kulipwa kama wafanyakazi wake. Hili kundi nalo lina wafanyabiashara wadogo hadi wakubwa. Na ni waajiriwa wachache sana wa vipato vya juu wanawazidi hili kundi kwa pesa.
 
Nilichomuelewa mtoa mada yeye kawachukua watu wote ambao hawajaajiliwa kawaweka kundi la wafanyabiashara [emoji1787][emoji1787][emoji1787],mwambieni arudi mtaani akafanye utafiti wa wajasiriamali,wafanyabiashara,wakulima,mawinga,madalali na machinga
 
Huna akili af huna heshima

Umeprove huwezi kujenga hoja, siwezi endelea argue na wewe.

Ignore list + 1
 
Mfanya biashara kama hatapata janga, yupo juu zaidi ya mwajiriwa. Fanya uchunguzi utagundua mfanya biashara anaishi maisha mazuri kuliko mwajiriwa. Mfanya kazi ukinywa beer 2 tu kila siku mshahara unaisha ila mfanya biashara anapeta.
Hilo halipingiki lakini idadi ya hao ni wachache, tena ni mabilionea
 
Huna akili af huna heshima

Umeprove huwezi kujenga hoja, siwezi endelea argue na wewe.

Ignore list + 1
Wewe ni mweupe umedhani ukitaja liability wengine hatujui, nikujulishe ya kwamba hayo mambo mimi nimeyasomea darasani kwa miaka, wewe umegoogle kwa juu juu tu ukahisi unajua kila kitu kuhusu liability na asset, its more than that !! hata hio id unayojiita kali linux nina uhakika wewe ni mweupe kwenye hacking
 
Mfanya biashara kama hatapata janga, yupo juu zaidi ya mwajiriwa. Fanya uchunguzi utagundua mfanya biashara anaishi maisha mazuri kuliko mwajiriwa. Mfanya kazi ukinywa beer 2 tu kila siku mshahara unaisha ila mfanya biashara anapeta.
Siku moja mwaka 2006 niko na rafiki yangu bar moja inaitwa Jogoo House Arusha mida ya jioni kama saa 11 hivi. Kukawa na watu wengi sana hiyo siku. Kwenye meza tulikaa na mama mmoja hivi. Yule mama akavunja ukimya kwa kusema "leo bar imejaa kwa sababu ya hawa waalimu na vijimishara yao ambayo inakaa tu kwenye mfuko wa shati"... akaendelea kusema yaani hapa wamepita bar baada ya kutoka soko kuu kununua mazagazaga ya nyumbani. Na kweli chini ya meza tuliona mifuko ya plastic imejaa vitu.
 
Wafanya kazi wengi wanaishi maisha magum ukitaka kuona ilo magufuli alivowanyima kutopandisha daraja kipindi chake walikuwa wanaishi maisha magum sn hata ss ivi wengi wanaishi maisha magum wachache wanaofanya kazi mashirika ya umma ndo wapo poa ila sio wale wa tamisemi mtu anakopa mpk take home inakuwa laki 2 ss uyo si bora boda boda anakuwa ana maisha mazuri
 
Msome jamaa vizuri halafu weka hoja zako. Bro unaamini kabisa mtu anunue gari hata kama la mkopo halafu ashindwe kununua mafuta?? Sio kweli,
Mkuu,
Unaishi mkoa gani? Huku dasalama tuna magar Ila sometimes hatunaga pesa ya MAFUTA
 
Wana maisha magumu kuzidi wafanyabiashara machinga, wauza karanga, figili, n.k. ?????
 
Huyu anashindwa kutofautisha kati ya Mfanyabiashara, Machinga, Dalali na Winga. Anawaweka kundi moja ndo maana wanakuwa wengi machoni pake.

Sio kila mjasiriamali ni mfanyabiashara.
Hao wote ni kundi moja tafauti ni bidhaa na huduma tu
 
Mfanya biashara kama hatapata janga, yupo juu zaidi ya mwajiriwa. Fanya uchunguzi utagundua mfanya biashara anaishi maisha mazuri kuliko mwajiriwa. Mfanya kazi ukinywa beer 2 tu kila siku mshahara unaisha ila mfanya biashara anapeta.
Mbona mimi nakunywa kreti na nahonga na hela haiishi?
 
NIAMBIE MZEE WA VIWANGO

Je siye boda boda na hao watumishi wa umma nani anaishi standard life?
 
Hivi mfanyakazi yupi huyo anayeishi maisha magumu mbona mimi alhamdulillah mtelezo tu
 
Makundi yapo mengi

Waajiriwa
Waliojiajiri
Wafanyabiashara
Waliowekeza

Hawa wote wanautofauti wake!!
 
Hila hii agenda ya wafanyabiashara na wachuuzi iwekwe wazi!
(wajasiriamali,wafanyabiashara,wakulima,mawinga,madalali na machinga)
Ukifikia level ya kuitwa mfanyabiashara unatakiwa huwe umeajiri! Mfanyabiashara kazi yake kuongoza na kusimamia mwenendo wa biashara! Sio mtu wa 💯 kuwa sehemu ya biashara!
 

Attachments

  • 1712677793297.gif
    42 bytes · Views: 9
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…