Wafanyabiashara Stendi ya Magufuli wataka mabasi yote yashushe na kupakia abiria hapo stendi ili wapate wateja

Kama ni hivyo Sasa si wangeifanya iwe na mkuu wa mkoa mmoja na mkuu wa wilaya mmoja tu, kulikuwa na sababu gani ya kujaza wakuu wa wilaya watano
Wakuu wa wilaya ni sababu ya kuhudumia idadi ya watu na si geographically. Kijiografia dar ni ndogo sana kuiwekea stend 3 ni matumiz mabaya ya pesa za umma.
 
Daladala zinatakiwa kupakia level seats ndiyo na pia bus inatakiwa isiwe na vituo vingi vya kushusha abiria zinaongeza msongamano mjini. Tumien fursa ya kushindilia kuongeza daladala nyingi na hivyo mtakuwa mmetengeneza ajira zaidi. Bus za mwendokasi Mpya zitakuja very soon.
 
Mbona kuna magari ya kuwachukua abiria wa ndege na kuwapeleka airport, au hilo hujui mzee wangu?
Hahaaa! Kwani nikienda na tax itakatazwa mi kunifikisha karibu na eneo maalumu la kushushia abiria wanaosafiri kwa ndege?
 
Huo mkopo na hiyo riba analipa nani ?!
 
πŸ˜„πŸ˜„πŸ˜„πŸ˜„πŸ˜„πŸ˜„Lakini sababu nyingine pia dar ni mkoa uliojaa watu wa lawama sana kila kitu unachofanya hawakitaki yaani hawana jema.
Akija mkuu wa mkoa mchapakazi hawamtaki wanamuona katili kwa sababu watu wanataka kuishi kimazoea lakini baadae kuishi kwao kimazoea kukisababisha maafa fulani pia wanageuka na kuanza kulaumu serikali ina viongozi wazembe hawafuatilii raia.
Mfano mzuri ni wale raia wanaoishi sehemu za mafuriko kama jangwani na msimbazi serikali huwa inawatahadharisha kuhama maeneo ya mabondeni hawasikii na huwa wanapewa viwanja nje ya mji wakaishi huko wanakataa na kubeza kwamba hawawezi kwenda kuishi kijijini.
Baadae mafuriko yakija wanasombwa na maji wanaanza kulaumu serikali tena kwamba haijali raia wake watu wanasombwa na maji hao wanaangalia tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…