Wafanyabiashara Stendi ya Magufuli wataka mabasi yote yashushe na kupakia abiria hapo stendi ili wapate wateja

Wafanyabiashara Stendi ya Magufuli wataka mabasi yote yashushe na kupakia abiria hapo stendi ili wapate wateja

Kama ni hivyo Sasa si wangeifanya iwe na mkuu wa mkoa mmoja na mkuu wa wilaya mmoja tu, kulikuwa na sababu gani ya kujaza wakuu wa wilaya watano
Wakuu wa wilaya ni sababu ya kuhudumia idadi ya watu na si geographically. Kijiografia dar ni ndogo sana kuiwekea stend 3 ni matumiz mabaya ya pesa za umma.
 
Basi mpya za mwendokasi zimeshakuja?
Halafu daladala pia zinatakiwa ziwe zinapakiza abiria level seats tu, Abiria waliopo hata hamuwezi kuwahudumia vizuri, hiki kinachofanyika sasa kwenye dalala kupakiza abiria kwa kushindilia kama nyanya kwenye tenga ni wendawazimu halafu na bado mna tamaa ya fisi kuchukua hata wachache wanaobebwa na mabasi.
Daladala zinatakiwa kupakia level seats ndiyo na pia bus inatakiwa isiwe na vituo vingi vya kushusha abiria zinaongeza msongamano mjini. Tumien fursa ya kushindilia kuongeza daladala nyingi na hivyo mtakuwa mmetengeneza ajira zaidi. Bus za mwendokasi Mpya zitakuja very soon.
 
Mbona kuna magari ya kuwachukua abiria wa ndege na kuwapeleka airport, au hilo hujui mzee wangu?
Hahaaa! Kwani nikienda na tax itakatazwa mi kunifikisha karibu na eneo maalumu la kushushia abiria wanaosafiri kwa ndege?
 
Imejengwa kwa mikopo yenye riba nafuu siyo pesa zako. Tunasubiri ushuke pale tupate kodi tukalipe deni. Nafananisha ndege na bus kwa kuwa vyote vina vituo maalumu vya kupakia na kushusha, hata hiace zina vituo maalumu vya kupakia na kushusha. Bus zingekuwa na msaada huo zisingelalamika kuomba kupandisha nauli, mafuta yakishuka mbona hawaombi kushusha nauli?? Ni uhuni tu.
Huo mkopo na hiyo riba analipa nani ?!
 
Tatizo la Dar es salaam kwenye uongozi ni mawili wengi wa viongozi WA Dar kuwepo huwekwa sababu wanapendelewa Wana connection lakini vichwani hamna kitu wenye akili hupelekwa mikoani ndio maana mikoani kunafanya vizuri

Pili viongozi wengine huhamishiwa Dar Kwa sababu za kiafya ili wakae karibu na hospital ya rufaa ya Mloganzila na Muhimbili wanakotakiwa kuwa wanahudhuria matibabu mara Kwa mara Kwa hiyo mkoa unakuta unaongozwa na wagonjwa wazima wako mikoani

Hii combination ya akili finyu na wagonjwa ndio inasababisha hizo chaos tunazoona

Jiji la Dar linahitaji watu wazima na wenye akili hasa
😄😄😄😄😄😄Lakini sababu nyingine pia dar ni mkoa uliojaa watu wa lawama sana kila kitu unachofanya hawakitaki yaani hawana jema.
Akija mkuu wa mkoa mchapakazi hawamtaki wanamuona katili kwa sababu watu wanataka kuishi kimazoea lakini baadae kuishi kwao kimazoea kukisababisha maafa fulani pia wanageuka na kuanza kulaumu serikali ina viongozi wazembe hawafuatilii raia.
Mfano mzuri ni wale raia wanaoishi sehemu za mafuriko kama jangwani na msimbazi serikali huwa inawatahadharisha kuhama maeneo ya mabondeni hawasikii na huwa wanapewa viwanja nje ya mji wakaishi huko wanakataa na kubeza kwamba hawawezi kwenda kuishi kijijini.
Baadae mafuriko yakija wanasombwa na maji wanaanza kulaumu serikali tena kwamba haijali raia wake watu wanasombwa na maji hao wanaangalia tu.
 
Back
Top Bottom