Wafanyabiashara Stendi ya Magufuli wataka mabasi yote yashushe na kupakia abiria hapo stendi ili wapate wateja

Wafanyabiashara Stendi ya Magufuli wataka mabasi yote yashushe na kupakia abiria hapo stendi ili wapate wateja

Watu hamtaki utaratibu, Tukitaka tuendelee tufuate utaratibu. Kama kuna haja ya kuwa na Bus terminal /stand kila wilaya basi lifanyike, lakini vituo vilivyopo viheshimike.

Lakini hao wachache wanaotaka kupandisha na kushusha abiria nje ya vituo halali sio sawa.
Mkuu umetoka jela nini? Naona unazingatia sana neno utaratibu
 
Sasa wenye Mabasi hawatakiwi waachwe huru kiasi hiko....
Lazima wafuate utaratibu,,,
Mana sasa hayo Mabasi hadi Chanika na Vijibweni nisha yaona.....

Hatakama tupo Soko huru lakini lazima vitu vifanyke kwa utaratibu...
Ukiona yapo huko jua wameona fursa ikiwamo wingi wa abiria kwann wasiende maeneo mengine kama makumbusho labda au masaki kule wanajua kule hawana abiria so

Fursa

Hata hizi kuku zinazo jiita wafanyabiashara stand zinapswakujiongeza wafate mabus yanapolala
 
Siku zote biashara haitakiwi kutegemea Stendi, bali stendi ndio inapaswa kutegemea biashara yako, shida ni hawa wafanyabiashara walidanganywa na ccm

Nimepita hapo stendi zaidi ya mara 50 lakini sikuwahi kununua chochote, hii ni kwa sababu si lazima abiria kununua kitu hapo stendi, sasa wanacholilia ni nini?
Wanashangaza sana.
 
Mbona Treni ipo katikati ya mji?. Na hata uwanja wa ndege upo katikati ya mji ila stendi ya mabasi wamepeleka mafichoni.
Aliyekwambia mbezi nje ya mji nani? Nje ukianzia wapi
Nanujue hata tren pia ipo mbali na maeneo mengi mfano mi nakaa kiluvya mbezi ni jirani kuliko kuifata tren huko posta au pugu

Acha kuwaza undezi
Sio lazma biashara yako iwe stand wa umekuwa mpiga debe
 
Viwanja vya ndege vyote hapa nchini na nje ya nchi huwa vinatakiwa kujengwa nje ya mji....
Sema kwa Mkoa wetu huu,Mipango miji huwa wanaruhusu ujenzi holela na watu kufanya ujenzi kwenye maeneo yaliyotengwa kwa maviwanda makubwa na miundombinu kama hiyo..mm
Aorport yetu iko nje ya mji ila mtoa mada kwa akuwa anakaa nako basi haowezi kuona hilo
Kulr ni nje kabisa mashambani ni vile kwa sasa dar imejaa kila kona hakuna nje ya mji tena
 
Selikali haipotezi mapato manake pale stand hakuna basi ambalo haliingii kuacha hela hata mara moja
Na ndio mana husikii kelele za selikali shida ni hawa wanaojiita wafanya biasharabwaliokosa ubunifu na kulazimisha watu wanunue bidhaa zao kinguvu kenge kabisa hawa
 
Mimi mfano nakaa mbezi ila nikifika kituoni nataka kwenda Moro naambiwa usafiri wa mabasi ya Abood haupatikani hapo ...Yapo Urafiki. Basi linajazia urafiki then linapita juu kwa juu Mbezi bila ya kuingia ndani stendi!

Zaidi ya asilimia 75-80 ya basi zinazoondoka alfajiri haziingii ndani ya stendi ya Magufuli badala yake zinapita juu kwa juu.

Wamiliki wa mabasi wanaihijumu serikali , wanaikosesha serikali mapato yake ya getini. Pia wanawahujumu watanzania kwa kuwakosesha ajira
Kumbe stand wanaingia
Negundua wewe una roho ya kichawi anapojaza abiria we hutaki sasa unataka nini?
 
Kwa wageni wa mji watapiga kelele tu bila sababu. Zamani hayo mabasi haya kuwa na ofisi binafsi. Tiketi ziliuzwa kiholela tu na masarange walifaidika na kupiga watu sana kwa utapeli wao.

Sasa hivi karibu mabasi Yote yana ofisi zao binafsi. Abiria wanakata tiketi kwa utulivu na bila ulanguzi. Ofisi hizi za mabasi pia ndio sehemu ya kupakia mizigo na baadhi ya wafanyakazi wa mabasi huanzia hapo.
Abiria anapokata tiketi anaambiwa muda wa ku ripoti na muda safari ina anza. Sasa abiria anachagua sehemu ya kupandia basi wakati wa kukata tiketi. Kama ameweza kufika ofisi ya basi kwa urahisi atapandia hapo... Kama kafika ofisi ya Magufuli kwa urahisi pia ndio atakapo pandia basi.

Kama basi halijapata abiria hapo Magufuli kuna haja gani ya kuingia kituoni? Sana sana watatoa ushuru tu wa kituo. Kwanini ulazimishe basi lipite hapo kama hakuna abiria wa kupakia? Au kwanini basi lipite hapo kama hakuna abiria anaeshuka hapo!?

Na mabasi mengi sasa hivi wanagawa ndani bites na vinywaji mbali mbali baridi.. Watanunua nini hapo stendi?
 
Watu hamtaki utaratibu, Tukitaka tuendelee tufuate utaratibu. Kama kuna haja ya kuwa na Bus terminal /stand kila wilaya basi lifanyike, lakini vituo vilivyopo viheshimike.

Lakini hao wachache wanaotaka kupandisha na kushusha abiria nje ya vituo halali sio sawa.

Kwa sasa hivyo vituo hakuna ndio maana utaratibu úliopo ndio huo unaouona.
 
Sgr nayo iwe inafuata abiria. Mkuu utaratibu lazima uwepo na upo kila nchi. Hiyo ya mabus kufata abiria sio sahihi ni kulazimisha tu
biashara ni ushindani kinachofanyika now ni ujanja wako na uwezo wako ndivyo vitakupa wateja mtu akisema afuate bus toka kigamboni mpka magu stand anaingia gharama na kupoteza muda kusiko na sababu wakati angeweza panda kilimanjaro yake pale ferry akasepa kwa uhakika..... usafiri wenyewe wa tabu bado muone shida watu wakiwekewa huduma karibu.

mlidanganywa sana na yule mzee Na bado mnadanganywa na huyu bibie
 
Abood Bus service

BM

Ally's star

Katarama

Happynation

Kilimanjaro

Tilisho

Kimbinyiko

Shabiby

Newforce

N.k

Ni miongoni mwa kampuni nyingi ambazo hazitaki kuingia Magufuli Bus terminal....usafiri wa asubuhi ni kazi sana , wanapita juu kwa juu
Nauli ya kutoka mbeya to Dar ni shingapi sahii
 
Back
Top Bottom