Wafanyabiashara Tanzania tupunguze kudhulumiana na tuwe waaminifu

Wafanyabiashara Tanzania tupunguze kudhulumiana na tuwe waaminifu

MamaSamia2025

JF-Expert Member
Joined
Mar 29, 2012
Posts
21,387
Reaction score
44,030
Wakuu naandika kwa masikitiko makubwa sana kwa kinachoendelea kwenye biashara nchini Tanzania. Huu uzi ni maalum wa kujisema na kujitaka kujisahihisha. Wengi wa wafanyabiashara kuanzia wadogo, wa kati na wakubwa wana uhaba mkubwa wa uaminifu na kuishia kuwa watu wa dhuluma. Hii ni tabia ya hovyo mno.

Kwanza wafanyabiashara kudhulumiana wenyewe kwa wenyewe ni jambo ambalo linazidi kuota mizizi. Utakuta mfanyabiashara mdogo kapewa mzigo wa mali kauli ila kulipa ni mzozo. Mfanyabiashara mkubwa naye katumiwa pesa lakini kutuma mzigo kama makubaliano yanavyotaka inakuwa changamoto. Ni wachache mno walionyooka. Wale wanaoagizia watu mizigo China, Dubai na Uturuki ndo hawafai kabisa. Pia kuna hizi kampuni za usafirishaji nazo ni kero kubwa.

Kimsingi hata hawa TRA na mabenki bila kukaza msuli hawawezi ambulia chochote toka kwa wafanyabiashara walio wengi. Yaani imefikia sehemu ukijitambulisha kama mjasiriamali unaonekana tapeli. TUJISAHIHISHE.
 
Ndio Taifa tulioamua kujenga. Kuanzia ngazi ya familia mpaka taifa. Wanasiasa, wafanya biashara, wamama, wababa, wanafunzi wote ni matapeli.
Tunda halianguki mbali na mti
 
Ni kama utamaduni wa nchi nzima, kuanzia kwa watawala wa juu mpaka wamachinga, wapika mihogo na wafagiaji wa barabara.
 
Ndio Taifa tulioamua kujenga. Kuanzia ngazi ya familia mpaka taifa. Wanasiasa, wafanya biashara, wamama, wababa, wanafunzi wote ni matapeli.
Tunda halianguki mbali na mti
Uko sahihi mkuu. Familia ndo msingi wa yote haya. Hata mafisadi wengi waliandaliwa wakiwa wadogo. Kumwambia mtoto asome kwa bidii ili aje afanye kazi serikalini kwenye marupurupu mengi ni sawa na kumwandaa fisadi kwa sababu marupurupu mengi huwa ni madili ya kifisadi serikalini. Ni muda sasa wa kujirekebisha.
 
Ndio maana watu wanataka reform
 
Ni collective mindset hii, sehemu kubwa ya Watz si waaminifu wanapenda pesa za chap chap...Vijana wanaona Hali ya mambo ilivyo huko juu hivyo tunaambukizana Kwa namna hii, watu hawajui Tu kwenye biashara kitu cha Kwanza ni uaminifu.
 
Mkuu reform ianzie ngazi ya familia.. kila mtu ajirekebishe
Kwa sasa kutoka chini kwenda juu ni ngumu sana. It will take 100 years to shape hii jamii. Kutoka juu kwenda chini ni rahisi sana na very effective. Case study Magufuli administration.
 
Mkuu reform ianzie ngazi ya familia.. kila mtu ajirekebishe
Kumbe unajua kuhusu masuala ya reform? Na huku umekaza mshipa wa matako na sura imekukakamaa watu wanapogusia kuhusu reform? mazafaka
 
Back
Top Bottom