Dr Msaka Habari
Member
- Apr 9, 2022
- 66
- 32
Na. Jonathan Kalunga
Wafanyabiashara wa ferri watakiwa kuepuka kufanya biashara pembezoni mwa barabara, mpaka pale watakapo tafutiwa maeneo mazuri kwa ajili ya shughuli zao.
Katazo hilo limetolewa na Diwani wa Kata ya Kigamboni Dotto Msawa, alipowahutubia wafanyabiashara hao Mara baada ya kumalizika kwa zoezi la usafi, ambalo ufanyika kila jumamosi ya mwisho wa mwezi.
Katika zoezi hilo Diwani aliongozana na Viongozi mbalimbali wakiwemo wenyeviti na wajumbe wa Serikali za Mitaa maafisa Mazingira pamoja na Viongozi wa Chama cha Mapinduzi.
Akizungumza na Wafanyabiashara hao pamoja na Wakazi wa Kigamboni Dotto Msawa alisema kuwa Halmashauri ya Manspaa ya Kigamboni inawaandalia maeneo mazuri na salama watakayo yatumia kufanya biashara pasipo kuwepo usumbufu na tatizo lolote.
"Nitoe rai kwenu ndugu zangu tusifanye biashara katika maeneo yasiyo rasmi, hasa pembezoni mwa barabara kwa ni hatari kwa maisha yenu, tufanye katika maeneo husika" alisema Dotto.
Pia amewaondolea wasiwasi wafanyabiashara hao, kwamba Halmashauri ya Wilaya ya Kigamboni ipo bega kwa bega na haijawatupa, kwani kuna mpango mahasusi kwa ajili ya kuwatafutia maeneo watakayoweza kufanyia biashara bila usumbufu wowote.

"Niwaambie tu kupitia vikao vya Halmashauri tayari tumepitisha mpango mahususi kwa ajili yenu, wa kuwatafutia maeneo mengine mazuri mtakayoweza kufanyia shughuli zenu za kila siku, na ndio itakuwa sehemu yenu ya kujipatia kipato lakini itawafanya muinue uchumi wa wa Nchi, kwa sasa tumieni maeneo tuliyowapa kwa muda huku huku tukiandaa utaratibu mzuri zaidi" alisema Msawa.