Complex
JF-Expert Member
- Mar 20, 2013
- 4,119
- 4,779
Kwa bahati mbaya ni kwamba ubora wa bidhaa na gharama ya bidhaa ni directly proportional.binafsi ninachojali ni bidhaa bora na ya bei reasonable, regardless of nani ameleta au nani anauza.
Nimetolea mfano hapo juu wa kifaa kama Blender. Ubora wa Blender unachangiwa kwa kiwango kikubwa na motor. Motor ikiwa nzuri, basi blender itasifiwa kuwa inafanya kazi vizuri, imedumu nk.
Sasa kwa motor, ili iwe nzuri ni lazima iwe imesukwa na nyaya za material mazuri. Hapa nazungumzia copper. The more the purity of the copper wires windings, the better the quality ya motor husika. Na blender ambazo zimetengenezwa na hizi motor kimsingi huwa ni ghali.
Sasa si wafanyabiashara wote wanaweza ng'amua issues za copper, steel na aluminium. Hivyo kwa kujua ama kutokujua, mfanyabiashara ataenda tengenezesha blender ya nyaya za kawaida, atakuja waaminisha watu blender ni nzuri. Na atauza bei ya chini. Madhara yake ndiyo kama niliyoyaweka hapo juu ktk post zilizopita.