Wafanyabiashara wa Kariakoo wagoma kuhama kupisha Wawekezaji

Wafanyabiashara wa Kariakoo wagoma kuhama kupisha Wawekezaji

Hapo lilipo jengo la n. h .c palikuwa hivyo maboresho yakafanyika sasa ni maofisi na limechukuwa watu wengi zaidi wapishe maendeleo zama za kukataa kila kitu zimeisha
 
Ukishakuwa mpangaji hasa wa hizi nyumba unafika wakati unajisahau unaona kama yako vile vile sasa mtu kakaa miaka 60 yote hiyo alojisahau na kuona wenye vyumba viwili buza sio wa maana si angekuwa kashatafuta kwake au sehemu nyingine ya kufall back ukishakuwa mpangaji ni kujiandaa siku yoyote kupewa notisi ya kisheria yaani wanategemea huruma tu ya shirika ila hawana chao kisheria siku 90 zikifika.
 
Unaweza kuelezea makusanyo ya sasa ya NHC kwenye hayo majengo kupitia kodi ya pango. Na watakachopata baada ya hapo.

Si ajabu mradi wenyewe wakishavunja hayo maeneo mwekezaji ana miaka 20 ya kurudisha hela zake kabla ya NHC kupata chochote sasa hapo kuna faida gani ya serikali.

Hizi ndio baadhi ya PPP zenyewe ni ufisadi mtupu wa kuchukua prime areas kirahisi kwa uongo wa uwekezaji.

Halafu taasisi ambayo inadaiwa karibu tsh 2 trillion inaweza afford kupoteza mapato yake kishamba; baadae huo mzigo wamrushie mlipa kodi.
Una hoja usikilizwe.
 
yaani wamepewa notice miezi mitatu, na kodi wasilipe, kwahiyo wao ile kodi ya miezi mitatu ambayo wangelipa wakaamua kula chips, na wakiondolewa wanasema wanaonewa. hao ni wa kufunga kabisa.
 
tatizo la hili, wanaweza kuondoka alafu hayo majengo yasifanyiwe chochote kile, yani yasiboreshwe
 
Ttz hii nchi imefika hatua ya kwamba ni ngumu kujua yupi yupo sahihi kati ya mlalamikaji na mlalamikiwa unabaki tu kuangalia mwisho wake ni upi
Kabisa mkuu, na shida ni kutokuwepo kwa uwazi katika hii mikataba tunayoingia na sera zisizoeleweka. Ngoja tuone mwisho wake
 
Hizi nyumba za nhc zishakua za watu binafsi, unalipa Kodi milioni Moja kwa mtu ye anapeleka 250k serikalini, wazivunje zote tu
Lol ndo tulipofikia kama nchi....


Na utaratibu wa kulipa kodi miezi sita, kuwalipa dalali mwezi mzima...unasababisha utafutaji wa vyumba vya kupanga na nyumba kuwa mgumu nchi hii

Sent from my SM-A032F using JamiiForums mobile app
 
I wish hao wawekezaji wanunue zile nyumba za NHC pale Bukoba wajengo majengo ya maana...

Maana nyumba za NHC Bukoba zinauchakaza mji...

Sent from my SM-A032F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom