Wafanyabiashara wa malori ya mizigo wamekuwa kero kwa abiria Stendi ya Kilombero

Wafanyabiashara wa malori ya mizigo wamekuwa kero kwa abiria Stendi ya Kilombero

Bushmamy

JF-Expert Member
Joined
Aug 18, 2019
Posts
9,140
Reaction score
15,963
Kituo cha magari madogo ya abiria Kilichopo kilombero jijini Arusha maarufu kama stand ya Kilombero kimezidiwa na wingi wa shughuli nyingi za kiuchumi hususani biashara tofauti na Lengo kuu la kituo hicho cha daladala.

Kituo hicho ndio kitovu cha daladala karibu zote zinazoelekea sehemu mbalimbali ndani ya jiji la Arusha

Magari makubwa ya mizigo toka mikoani yamekuwa yakitumia kituo hicho cha abiria kushusha mizigo yao ya Mananasi, machungwa, viazi nk. hapo na kufanya biashara zao hapo hapo kituoni kitendo ambacho ni usumbufu na ni hatari kwa abiria kwani eneo hilo lilitengwa maalumu kwa ajili ya usafiri wa magari madogo.

Baadhi ya abiria wanaotumia kituo hicho wamesema wanapata usumbufu mkubwa kutokana na kuwa kituo hicho mpangilio maalum maana haieleweki kama ni soko au kituo cha abiria.

IMG-20230301-WA0017.jpg

Wafanyabiashara 1.jpg
Wafanyabiashara 2.jpg
 
Lengo la halmashauri zetu sio upatikanaji wa huduma bora bali wamekua wakusanya kodi tu.

Halmashuri niza kikaisari.
 
Organize waathirikahapo, sukumeni hayo malori nje ya eneo lenu ,atakayebisha choma moto Lori lake,police naona wameshindwa kusimamia sheria, eneo halikutengwa kwa trunks bali magari ya abiria
 
Back
Top Bottom