Koffi Annan
JF-Expert Member
- Dec 23, 2018
- 1,771
- 5,087
Wafanyabiashara wa mbogamboga Soko la Ilala wamelia kupata hasara baada ya gari iliyokuwa imebeba mizigo yao kutoka Gairo mkoani Morogoro kukamatwa nje ya soko hilo.
Mwenyekiti wa Wafanyabiashara hao, Thomas Hezron amesema gari hiyo ilikamatwa na mawakala wa vipimo kwa mazao ya shamba mkoa wa Ilala baada ya kuonekana kwamba uzito kwa kila gunia kuzidi, leo jijini hapa.
"Kwa kawaida mizigo yetu tunauza kwa fungu na sio kwa kilo, sasa tumeshangaa kuambiwa mizigo yetu imezidi uzito," amesema Hezron.
Hezron amesema walipata ridhaa ya kupewa mizigo yao saa mbili asubuhi muda ambao hawawezi tena kupata wateja kwani huwa wanafanya biashara hiyo kuanzia saa 9 usiku mpaka saa 12 asubuhi.
Hata hivyo wafanyabiashara hao waligomea kushusha mizigo yao hata baada ya Mamlaka ya Vipimo kuiachia gari hiyo huku wengine wakidai kulipwa fidia na mamlaka hiyo kwa kuchelewesha kuruhusu mzigo na kusababisha hasara hiyo.
Naye Fatihia Kawiche ambaye ni mfanyabiashara wa mbogamboga katika soko hilo amesema hawajui hatima yao kwani mboga zao hazina wateja tena na hawajui pa kizipeleka.
"Mimi nina mtoto wa miezi 10, nimemuacha nyumbani saa saba usiku, nikijua nitakuja hapa nifanye biashara na kurudi nyumbani, lakini mpaka sasa sielewi hatima yangu," amesema Kiwiche.
Kiwiche amesema walifika ofisi ya Mkuu wa Mkoa na kuambiwa warudi katika ofisi za Vipimo vya Mazao ya Shamba hapo Ilala ili kuruhusiwa kupewa mizigo lakini amesema uamuzi huo ulikuwa hauna msaada tena kwani tayari ni hasara kwao.
Martha Samburu, mfanyabiashara wa soko amesema utaratibu wa kupima mboga katika mizani ni mpya na yeye ameshangaa kuona utaratibu huo.
"Nina miaka 30 katika kazi hii, lakini sijawahi kuona utaratibu huu. Sijawahi kuona gunia la mboga kupimwa uzito, na hatujawahi kupewa taarifa hizi wala elimu yoyote, lakini leo kwa ghafla wameamua kufanya hivyo," amesema Samburu.
Crédit: Instagram