A
Anonymous
Guest
Wafanyabiashara wa Soko la Samaki Feli, lililopo katika Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara Mikindani, tunaomba msaada wa Mkuu wa Mkoa kufuatia ukiukwaji wa taratibu katika ukusanyaji wa ushuru.
Tunakatwa ushuru wa kila siku bila kupewa risiti za malipo kama inavyotakiwa. Tunapodai kupewa risiti hizo, baadhi yetu hutishwa kwamba tunaweza kuzuiwa kuendelea kufanya biashara katika eneo hilo.
Hali hiyo imekuwa ikitupa wasiwasi na kuibua maswali kuhusu uwazi na uwajibikaji katika ukusanyaji wa mapato. Kutokana na hali hiyo, tunamuomba Mkuu wa Mkoa kuingilia kati, kufanya uchunguzi wa kina kuhusu malalamiko hayo, na kuchukua hatua stahiki ili kuhakikisha ukusanyaji wa ushuru unafanyika kwa kuzingatia sheria, taratibu na haki zetu.
Ufafanuzi zaidi, soma ~ DED Mtwara Mikindani: Muuza Samaki anayetozwa ushuru kisha akiomba risiti anatishiwa, aje aripoti tuwabaini wanaofanya hivyo