Mwanantogakulya
Senior Member
- Mar 18, 2025
- 157
- 155
Wafanyabiashara wadogo katika mji mdogo wa Langangabilili, wilayani Itilima, mkoani Simiyu, wameibua kilio kikubwa wakidai kutapeliwa na askari wa taasisi tatu za uhifadhi za serikali waliokuwa wakitekeleza operesheni ya kutokomeza fisi kwa zaidi ya miezi mitatu mfululizo katika eneo hilo.
Askari hao kutoka Mamlaka ya Hifadhi ya Taifa Tanzania (TANAPA), Mamlaka ya Wanyamapori Tanzania (TAWA), na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), wanadaiwa kula, kunywa, kutumia huduma za kibiashara, na hata kukopa fedha kwa wafanyabiashara wadogo—lakini wakaondoka bila kulipa madeni yao.
“Walikuwa wanachukua vocha za simu kila siku. Wengine niliwakopesha pesa, tuliwaamini kwa sababu walikuwa askari wa serikali,” anasema Bi. Janeth Nangwa, Mfanyabishara wa Langangabilili.
Kwa mujibu wa baadhi ya wafanyabiashara, waliowasiliana na askari hao baada ya kuondoka, walijibiwa kuwa hata wao hawajalipwa posho zao za kujikimu, hivyo hawana uwezo wa kurejesha madeni kwa sasa.
Hali hiyo imewaacha wafanyabiashara hao katika hali ngumu, wakihangaika kurejesha mikopo ya mitaji yao na kushindwa kuendelea na shughuli za kiuchumi.
Wadau wa maendeleo mkoani Simiyu wameitaka Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Itilima kwa kushirikiana na wakuu wa taasisi husika, kuchukua hatua za haraka ili kuhakikisha wafanyabiashara hao wanalipwa haki yao.
“Katika taifa linalojitahidi kukuza uchumi wa kati kupitia ujasiriamali mdogo, tukio kama hili linapaswa kushughulikiwa kwa haraka ili kulinda imani ya wananchi kwa taasisi za serikali,” amesema mmoja wa viongozi wa jamii mkoani humo.
Swali kubwa linaloibuka kwa sasa ni: Je, serikali itasikiliza kilio cha watu wa chini, au itaacha kilio chao kimezwe na ukimya wa kimfumo?