Wafanyabiashara wafikishwa Mahakamani kwa Kusafirisha Heroin kilo 58.62

Wafanyabiashara wafikishwa Mahakamani kwa Kusafirisha Heroin kilo 58.62

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
1684559418942.png
Wafanyabiashara watatu, Goodness Remy mkazi wa Salasala, Emmanuel Chigbo Mkazi wa Goba na Paulina Mwanga mkazi wa Kibaha wamefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na Mashtaka ya Uhujumu Uchumi.

Wakili wa Serikali, Frank Michael, ameiambia Mahakama kuwa, washtakiwa walitenda kosa hilo Aprili 19, 2023 eneo la Salasala, Kinondoni jijini Dar es Salaam ambapo walikutwa na Dawa aina ya Heroin.

Upande wa Jamhuri uliomba Mahakama kupanga tarehe nyingine kwasababu upelelezi haujakamilika. Kesi imeahirishwa hadi Juni 1, 2023 na washtakiwa wote wamerudishwa Mahabusu kwa kuwa kesi yao haina dhamana.

MWANANCHI
 
Ukifanya hiyo biashara sasa hvi ni hupendi kuishi uraiani....ila km unapenda bado kuwa uraiani achana nayo kabisa.Ukidakwa unapotea na watu tunakusahau....yote ni tamaa ya pesa za haraka haraka
 
Dah, nawahurumia sana

Japo wanasema ajali kazini ila vijana hii biashara ishakuwa sio hii.
...Hivi wanakamatwaje ? Kama Mtu umeuficha sawasawa mzigo wako na kuchukua tahadhari Zote, unakamatwaje? Mtu anakuwa amekuchomea ? Ama Askari Wetu wamekuwa Mahodari kiasi Hicho ?
 
Back
Top Bottom