Hali ilivyo eneo la Lulembela wilayani Mbogwe mkoani Geita asubuhi ya leo Alhamisi Septemba 12, 2024 ambapo hadi sasa wafanyabiashara hawajafungua maduka yao wakidai kuhofia kukamatwa na polisi.
Mzizi wa hofu hiyo ni vurugu zilitokea jana baina ya wananchi na polisi na kusababisha watu wawili kuuawa.
Taarifa iliyowekwa na Msemaji wa Jeshi la Polisi jana Jumatano, David Misime kwenye inasema katika vurugu hizo waliopoteza maisha ni mwanaume mmoja ambaye jina lake halijafahamika anayekadiriwa kuwa na miaka 18 -20 na mwanafunzi wa kidato cha nne wa Shule ya Sekondari Lulembela, Theresia John (18) ambaye nyumba yao inatazamana na kituo cha polisi
Misime amesema chanzo cha vurugu hizo ni baada ya watu wawili kuonekana wakiwa wamebeba watoto wawili na wananchi waliokuwa kwenye mnada wa Lulembelea kuwahisi kuwa ni wezi wa watoto na kuanza kuwashambulia