Wafanyabiashara wanaochukua bidhaa Afrika Kusini na Uganda

EJM_

JF-Expert Member
Joined
Jul 8, 2011
Posts
3,836
Reaction score
2,100
Habari wadau, wale wenzetu wanaofanya biashara ya kuchukua bidhaa kutoka Afrika Kusini na Uganda, wanaweza kutupa uzoefu Kidogo juu biashara hiyo;
Aina ya bidhaa zinazopatikana huko ambazo ndizo zenye soko kubwa hapa kwetu
Maeneo maalum kwenye nchi hizo ambapo bidhaa husika hupatikana
Usafiri na namna ya kusafirisha bidhaa hizo

Tupeane uzoefu

Asante
 
Ningeomba kujua iwapo ninasafiri na mzigo kwa Basi tokea Afrika Kusini ni changamoto gani ninazitarajia ktk Nchi likopitia hilo Basi?
Hakuna bus linalotoka moja kwa moja South Africa to Tanzania ila yapo yanatotoka south To Malawi pia Malawi To Tanzania direct then Zambia to Zimbabwe na Zimbabwe To South Africa,ukipitia Zambia ni bora zaidi maana Malawi ni wasumbufu sana na kila baada ya km50 kuna geti,ukipitia nchi zingine kama mzigo wako ni mkubwa utalipia Bond then utarudishiwa pesa yako wakati unatoka lkn kwa Malawi hawatakubali watakulazimisha ulipe ushuru Hakuna nchi ya kijinga duniani Kama Malawi
 

Nauli za basi kwa kupitia Zambia ni kiasi gani mkuu?
 
150,000 haizidi hapo. Na ofisi za hayo Mabasi utapata kariakoo

Okay, hii ni mpaka Zambia [emoji1268] na za kufika South Africa [emoji1221] au hii ndio moja kwa moja?
 
Nauli za basi kwa kupitia Zambia ni kiasi gani mkuu?
Nauli kamili hadi sauz ni kama laki tatu.ukifika sauz itabidi ukae hoteli angalau kwa siku 2.halafu urudi kwa laki tatu tena.ukijumlisha na gharama za paspot utakua umepunguza visenti vingi.mimi nilifikir utafute kampuni au mtu akununulie kisha akutumie.ungeweza anza kias kidogo upime biashara
 

Nadhani hili ni wazo zuri
 
Kwa Kampala Uganda;
wengi wa TZ hufuata nguo hasa za kike, na viatu. Maduka mengi ya nguo yapo Kampala maeneo yanayozungukia New & Old Kampala Taxi Park hasa mitaa ya Nakivubo, Namgoba, Namirembe n.k.
Usafiri ni kwa basi na kampuni mashuhuri ni FRIENDS Express ambao wana route ya DSM-KPLA, MZA-KPLA. Kutokea Dsm-Kampala ni kama 80,000/= na kutokea Mza-Kampala ni 40,000/=.
Usafiri wa mizigo ni kutumia basi, na kutoka DSM-KPLA ni siku 2, na kutokea Mza-KPLA ni masaa kama 14.
Usumbufu upo mpakani hasa kama ni mgeni kwa kuwa kodi ya mpakani sharti upatane na kondakta kulingana na atavyokukadiria mkiwa pale Terminal kabla ya safari. Ukileta ujuaji zaidi sharti akuchomeshe kwa maafisa wa TRA pale Mutukula, ila ukipatana nae wewe hata hutazungumza na maafisa wa TRA.
Sehemu za kulala kama upo na mwenyeji zipo affordable kwa maana kwamba mnaweza kuchangia chumba kimoja (hawana usumbufu wa kuzuia kulala jinsia moja) na vyumba vya watoto wa wakulima vipo vya hadi 30,000 Tsh kwa kuchangia wawili.
Passport ya dharura inaweza kutumika kuingia na kutoka UG.
Ni vizuri unapoenda kwa mara ya kwanza kupata mwenyeji ili kukufahamisha mambo mengine machache na hasa ukadiriaji wa kodi wa kondaktaz.
Epuka kuzoena na mtu usiyemjua uwapo UG na kumkaribisha kwa room yako labda tu kama unatoka naye huko unakotoka.
 

Shukran sana mkuu, hizi details zitawasaidia wengi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…