Kwa Kampala Uganda;
wengi wa TZ hufuata nguo hasa za kike, na viatu. Maduka mengi ya nguo yapo Kampala maeneo yanayozungukia New & Old Kampala Taxi Park hasa mitaa ya Nakivubo, Namgoba, Namirembe n.k.
Usafiri ni kwa basi na kampuni mashuhuri ni FRIENDS Express ambao wana route ya DSM-KPLA, MZA-KPLA. Kutokea Dsm-Kampala ni kama 80,000/= na kutokea Mza-Kampala ni 40,000/=.
Usafiri wa mizigo ni kutumia basi, na kutoka DSM-KPLA ni siku 2, na kutokea Mza-KPLA ni masaa kama 14.
Usumbufu upo mpakani hasa kama ni mgeni kwa kuwa kodi ya mpakani sharti upatane na kondakta kulingana na atavyokukadiria mkiwa pale Terminal kabla ya safari. Ukileta ujuaji zaidi sharti akuchomeshe kwa maafisa wa TRA pale Mutukula, ila ukipatana nae wewe hata hutazungumza na maafisa wa TRA.
Sehemu za kulala kama upo na mwenyeji zipo affordable kwa maana kwamba mnaweza kuchangia chumba kimoja (hawana usumbufu wa kuzuia kulala jinsia moja) na vyumba vya watoto wa wakulima vipo vya hadi 30,000 Tsh kwa kuchangia wawili.
Passport ya dharura inaweza kutumika kuingia na kutoka UG.
Ni vizuri unapoenda kwa mara ya kwanza kupata mwenyeji ili kukufahamisha mambo mengine machache na hasa ukadiriaji wa kodi wa kondaktaz.
Epuka kuzoena na mtu usiyemjua uwapo UG na kumkaribisha kwa room yako labda tu kama unatoka naye huko unakotoka.