Isanga family
JF-Expert Member
- Feb 25, 2015
- 17,080
- 33,076
Mkuu biashara nadhani ni matangazo yako pia ili uweze kufanya biashara ya uhakika na pia na uharaka zaidi ila usikope hela za Bank harafu upeleke SA kununua mzigo maana pana mipaka mingi muda mwingine utashindwa kulipa marejesho kwa sababu mzigo haujafika kwa wakati..Mkuu hongera sana kwa kutoa information zenye faida na kujibu maswali yenye vision.
Ila bado niko na maswali zaidi ya kuuliza japo wadau wengine wameshauliza.
1.Je kwa mtu anayeanza biashara hii ya chocolate na cosmetics inatakiwa minimum capital iwe kiasi gani?
2.Je mtu anaweza akaanza kwa kwenda kufuata mzigo South Africa bila kuandaa soko maalumu Tanzania?Je hizi bidhaa ni hot cake kiasi kwamba hata nisipoandaa soko nikija nazo nitakuwa na uhakika wa kuziuza on time?
3.Je usalama uko vipi South Africa kwa mfanyabiashara anayekwenda kuchukua mzigo?
4.Je kuna cargo agents ambao wanaweza kuzisafirisha bidhaa hizo kwa ndege ili mtu akienda kukusanya mzigo anamkabidhi Cargo agent kisha anarudi kwa bus wakati mzigo wake umeshatangulia kwa ndege?
Chochote ni bidhaa zenye uzito kidogo hautapata faida ukipakia kwenye ndege waliofanikiwa ni wale wenye Canter yake harafu anaenda kupakia mwenyewe mzigo akiwa na dereva wake na yeye pia anaendesha wakifika Tanzania wanazunguka mkoa kwa mkoa wanamalizia Dodoma tuu hapo...
Kwa mazingira ya wafanyabiashara usalama upo ndio maana watu wengi wanafata bidhaa JHb na pia yapo maeneo yenye hotel salama unafanya biashara zako na kurudi salama kabisa..
Sijaelewa mnaposema mtaji kiasi gani maana wapo wanaohitaji kubeba box zake 200 za Chochote au Kontena zima au fusso ukajaze hapo ndio wewe useme nikiwa na kiasi gani ntanunua mzigo wa kiasi gani mpaka naufikisha Tanzania kwa kulipa kila kitu...Mtaji mkubwa sio solution ya biashara wewe na mbio zako kukimbia na kuuza kwa haraka na kutokopesha mali kwa watu wasio waaminifu bora ubaki na mali yako kuliko kutake risk kwa watu wataokukwamisha...
Chocolate ina soko sana Tanzania hivi vitu ukiambiwa jaribu kwenda kwenye supermarket yeyote ulio jirani yako yenye hizo bidhaa uliza kama unaweza ukawapa uone muitikio wao na aina za Chocolate maana zipo aina tofauti tofauti ni wengi wanafanya hii biashara na msitegemee watakuja kuwaambia hapa hata kama wapo humu...mimi niliwahi pata order kipindi fulani niliona ina faida na SA vipo vingi mpaka oil ya Castrol pia pale pana kiwanda na wana bei nzuri ambayo ukileta Tanzania unauza kwa jumla vizuri tuu na huku umelipia kodi kwa hizo biashara za nje sumu yake ni kukwepa kodi ukikwepa Kodi harafu TRA wakachukua mzigo hautaweza kuja kusimama ni kupambana kulipa kodi ili usisumbuliwe na wahuni Road au unapouza bidhaa zako...
Bidhaa za SA nyingi zinajitajika sana nchi zetu hizi unaweza kwenda sokoni ukauliza bidhaa ambazo ni adimu harafu ukakimbia kama unataka kuuza kwa haraka hasa hasa ni Kariakoo ndio wanajua bidhaa zilizopo sokoni au hakuna...