Wafanyabiashara weusi Tanzania, pelekeni watoto India wasome shahada za family business ili mkifa biashara zisife

Wafanyabiashara weusi Tanzania, pelekeni watoto India wasome shahada za family business ili mkifa biashara zisife

YEHODAYA

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2015
Posts
36,902
Reaction score
52,001
Biashara nyingi za wafanyabiashara ngozi nyeusi hufa mwanzilishi akifa tofauti na za wahindi,waarabu na wapemba
Wahindi ndio wanaongoza duniani kwa uwezo mkubwa wa familia kuweza kuendesha biashara.

Nashauri wafanyabiashara wa ngozi nyeusi wapeleke watoto vyuo vikuu vya India wakachuke degree za family business. Kule wanazo kuanzia degree ya kwanza, ya pili hadi PhD

Napendekeza India sababu ndio wenye ufahamu mkubwa kwenye uendeshaji wa family business.Mainchi mengine kama ulaya na Marekani wao uzoefu wao mkubwa hauko kwenye family business uko kwenye corporate business zile za kusajili masoko ya hisa na kuuza hisa sokoni.

Mtoto akisoma family business degree mzazi hata akifariki anakuwa anajua nini cha kufanya.

Nimechoka mazishi ya biashara za Waswahili ngozi nyeusi kuwa akifa tu mwanzilishi na biashara inakufa hata iwe kubwa vipi.
 
Je , degree ya family business Ni bora kuliko hands on experience kwenye hiyo family business? Biashara zinatofautiana.
Ndio maana nikasema wafanyabiashara wapeleke watoto wao Sababu hands on experience wanaipata hapo kwenye biashara za wazazi wakiongeza na knowledge ya chuo inawapa competitive advantage makampuni makubwa kama Azam watoto wamesomeshwa sana na ndio wanaendesha kampuni kwa ufanisi mkubwa.
 
Huku sisi akifa huwa tunagawana cha aliekufa!..
And That's the business
Uko sahihi familia za kiswahili ngozi nyeusi mwenye biashara akifa wanafanya vikao vya mirathi vya kugawana mali badala ya kukaa kuongelea jinsi gani waiendeshe isonge mbele wawe wanagawana faida!!! Wao wanawaza kugawana tu!!
 
Hata wakisoma kazi bure..
-Baba ana acaunt kumi za bank zote hazijulikani na familia

-Baba ana biashara nyingine zaidi ya tatu zote hazijulikani na familia moja tu ndiyo inayo julikana na famili

-Baba wa kiafrica anaamini hakuna anaeweza kuendesha biashara yake tofauti na yeye

-Baba wa kiafrica haamini watoto wake mda wote anahisi kuibiwa..

Baba wa kiafrica haamini mawazo ya mtu mwingine zaidi na mawazo yake


wacha tu zife
 
Mimi hii degree ndio naisikia leo
Ziko kibao tena zipo miaka mingi tu ila Tanzania na nchi nyingi za kiafrika vyuo havifundishi hizo degree naona havioni umuhimu na hii imechangia sana family business nyingi za kiafrika kufa mwanzilishi akifa.India zipo tena miaka tu
 
Upumbavu tu hapa umeandika..

Mbona huyo Mo na watoto wa Bakhressa hawajasoma hizo family business bachelor na wamesoma US na UK??

Mzazi mshirikishe mtoto wako kwenye biashara zako tangia akiwa mdogo na uweke succession plan. Lakini pamoja na yote hayo msisitize asome kwa bidii ili aje asimamie hizo biashara. Hata akisoma Udom kama utakuwa umeweka msingi imara tangia mwanzoni hawezi kufeli
 
Upumbavu tu hapa umeandika..

Mbona huyo Mo na watoto wa Bakhressa hawajasoma hizo family business bachelor na wamesoma US na UK??
Kwenye business kuna area nyingi kuna marketing,finance, planning , production nk angalia hao watoto wa bakhresa walivyojipanga wamesoma maeneo tofauti tofauti lakini relevant kwa uendeshaji kampuni

Ikifika finance anasimama kipanga wa finance nk

Mimi nimetoa wapi wafanyabiashara waswahili waanzie wachukue degree za family business kampuni inavyokua waweza wengine kuanza kusomra specic areas ili kampuni iwe na watoto experts kwenye nyanja mbalimbali ndani ya kampuni

Mmi nashauri wapi waanzie kama sehemu ya kuanzia kwenye succession plan ku wa empower watoto kwa knowledge ya family business toka uhindini kwa wazoefu wa hizo biashara za fanilia
 
Back
Top Bottom