Wafanyabiashara weusi Tanzania, pelekeni watoto India wasome shahada za family business ili mkifa biashara zisife

Anaanzia wapi kumshirikisha wakati cha kwanza atakuwa anasimangwa. Soma uwe na vyako.hivi havikuhusu.

Ataambiwa nakulipia ada basi.

Waafrika hatuna mpango wa maendeleo
 
Hivi wewe si ni mshauri huko ccm kwanini usiwaambie waanzishe hizo kozi hapa nchini kwenye vyuo vyetu?

Yaani watu mpaka waende india?

Nyie ndio wale majizi mliokuwa mnachuma fedha za wizi ili mkatibiwe nje ya nchi badala ya kujenga hospitali madhubuti humu humu nchini!

Akili za panya wa Kiafrika!
 
That's the cultural difference! Baba was kiakfrika hata access ya bank account hataki mkewe na watoto wawe nayo, anaona bora akifariki na biashara ifungwe tu kuliko wengine kufaidi mfano, mjane wake Ku enjoy mali zake na mwanaume mwingine, sababu ndo mawazo yake yanampeleka hapo. Control from the grave.

Badilikieni wanaume! Ndo wale wale wanaoachisha wake zao kazi sababu wanataka kuchunga mke, result ni familia inakuwa na income moja badala ya mbili. Akitangulia mbele what happens to his family??

Badilikeni.


 


100% . Family business si lazima kila mwajiriwa awe family, cha muhimu ni wanafamilia kujua kinachotakiwa kuhakikisha biashara inaendeshwa ipasavyo .
Kikubwa Ni mila hazizingatii Ku include mke na watoto kwenye "mambo ya baba" so what's the result?
 
Biashara ni wito na maono, kama nimefanikiwa kuwasomesha basi wakatafute vyao, mi nilifundishwa na nani?

Wacha biashara ife!
Hii roho wengi wenu ndo mnayo. Hakuna degree itakayookoa biashara ya familia kama baba hana nia ya kuiendeleza baada ya kuaga dunia. Hamna nia ya kujenga generational wealth.
 
Mkuu uko sawa but tambua wahindi si kwamba wanawapeleka sana watoto wao India.

Angalia life lao.

1. Muhindi mtoto wake hasome Bording kamwe chunguza utajua.

2. Angalia aina za Masomo wanao soma vyuoni, kama sio IT basi Law, au Marketing, au Accounting, au Procurement au Udakitari na ukikuta anasoma Udakitari basi jua wana Hospitali,Huwezi wakauta wanasoma Arys in History au Mass commincation sijui Maendeleo ya jamii, hizi ni kozi za kibantu
 
Kwa sababu Tanzania na Africa watuanasoma wakaajiriwe
Ziko kibao tena zipo miaka mingi tu ila Tanzania na nchi nyingi za kiafrika vyuo havifundishi hizo degree naona havioni umuhimu na hii imechangia sana family business nyingi za kiafrika kufa mwanzilishi akifa.India zipo tena miaka tu
 
Sio wote wanao soma sema wahindi wengi na Waarabu hubebwa na mazingira.

Mtoto wa Kihindi Familia nzima ni wafanya biashara, Wajomba wafanya biashara, Mashangazi wafanya biasharaz Majorani wafanya biaashara, Marafiki wazazi wao wafanya biashara hapa automatic mtoto lazima aje kuwa mfanya biashara tu.

Tofauti na sisi ambapo sana hata kama baba ni mfanya biashara unakita watu tnao interact nao wengi sio wafanya biashara
 
Hapo kwenye “control from the grave”, panafikirisha sana.
 

Kwa uwezekano mkubwa education haichangii uendeshaji wa biashara ingekuwa inachangia kwa sailimia mia hizo biashara za watu weusi zisinge kufa Ila experience ndio kitu katika swala la uendeshaji wa biashara za familia unaweza mpeleka mtoto india havard na kwengunepo na asiweze endesha biashara, historia inaonyesha kabisa kwa bilionea namba moja wa india [emoji1128]

Bwana ambani mukeshi ambaye baba alimuachisha shule na kuanza kumpa biashara aiendeshe na matunda yakaoneka. Hapa hapa bongo muangalie mohamed abood alikua anaendesha biashara ya baba yake toka alipomaliza shule na baada ya baba yao kufalikialiendesha vema.
 
Naongelea wafanyabiashara ngozi nyeusi walivyo hovyo siongelei ngozi nyeupe akina abood Nk watu ngozi nyeupe Hawana shida wanaelewa vizuri mambo ya succession plan kwenye business.

Wawe akina Abood, Mo dewji watoto wa bakheresa nk sina shida na watanzania ngozi nyeupe wawe waarabu, wahindi,au wapemba shida yangu waswahili ngozi nyeusi wawe wachaga au kabila yeyote.
 
Hii roho wengi wenu ndo mnayo. Hakuna degree itakayookoa biashara ya familia kama baba hana nia ya kuiendeleza baada ya kuaga dunia. Hamna nia ya kujenga generational wealth.

I do not work on generational wealth...
 

Kumbuka haya mambo ya family business ni mapya kwa jamii zetu za kitanzania. 'Family business' kwa wengi ilikuwa mna ng'ombe, mna ardhi. Vijana (wanaume) walikuwa wanarithi hivi vitu, wasichana walikuwa wanachukuliwa kama mali ndo maana wakiolewa mnapata ng'ombe, harithi mali ya baba, akifiwa na mumewe ndo hivo ndugu wanakuja kuchukua walichochuma na marehemu na huenda na yeye akarithishwa kwa ndugu pia.

Mwaka ni 2020 , mambo yamebadilika ILA bado kuna zile akili za aidha kutoshirikisha watoto wa kike/wanawake kwenye mambo ya mali, au ku-exclude mke na watoto wote kwenye mambo ya mali ILI TU , ndugu zako wakija ukifariki wachukue mali. Ndo kitu kinachoumiza jamii zetu hizi, wanaume kuendekeza jamaa kuliko immediate family ( mke, watoto ) hivyo ukifa, kila ulichofanyia kazi kinakufa pia.

Nina uhakika, hata tukiwa na elimu ya kawaida, kama una maono, hauendekezi umalaya (hukupotezea muda, huleta magonjwa na ugomvi baina ya familia , watoto hawatakuheshimu), hauendekezi ndugu na huogopi kusemwa (wabongo ndo tatizo letu , tunafanya mambo membi ku-please wa nje huku nyumbani twaumia), tunaweza kuanza kuona biashara nyingi za kifamilia zikiendelezwa hata mwanzilishi akishatangulia.

Ndio maana huwezi kupeleka mtoto shule tu mradi apate elimu akaajiriwe. Kama wewe una duka lako, jaribu kuwashirikisha watoto wawe na maono na uelewa zaidi. Wakifunga shule, nenda nao shambani, kataliini mbugani muone mahoteli yanavoendeshwa. Chochote kuchangamsha akili awe na maono/inspiration ya kuanzisha vya kwake au kendeleza vya kwenu.

Nimeongea sana !
 
Wala hamna haja ya kusomesha bali kubadili tamaduni. Kama unabiashara basi hakikisha unamfundisha mwanao toka akiwa mdogo kuhusu biashara hiyo. Mfano wenzetu wahindi mtoto anaenda kwenye biashara na baba yake anafanya kazi za dukani /biashara husika akiwa likizo weekend n.k.

Mpaka anamaliza chuo anajua kila kitu kushusu baishara na anaendelea kufanya ile biashara kwa uaminifu bila tamaa wala makuu. Baada ya baba kufikia umri fulani anamuachia mtoto mamlaka yote ya biashara yeye anabaki kuwa mshauri, ikitokea anatangulia mbele ya haki mtoto tayari anajua kila kitu.

Mfumo huu unawezekana lakini kwa vijana wasio na tamaa au kutaka kuishi maisha ya anasa...mfano Mo kaachiwa METL mapema tu na baba zake kina Dewji na yeye itafika mahali atamuachia mwingine. Suala sio degree bali utamaduni na kufikiria kujenga kitu cha kizazi sio kujifikiria wewe peke yako kutaka kutumbua pesa kuishi kifalme bila kujali kizazi chako.
 

Point yangu hapo ni uzoefu na sio kwenda kusoma.
 
Hizi familia zetu ambazo mtoto akishika gari ya baba au akijaribu kukatiza katika biashara ya mshua anapigwa biti anaambiwa asitegemee cha kurithi akapambane atafute cha kwake..... Sijui kama hii elimu wataelewa na ndio maana umasikini ngazi ya kaya unazidi kukua...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…