naongelea wafanyabiashara ngozi nyeusi walivyo hovyo siongelei ngozi nyeupe akina abood Nk watu ngozi nyeupe Hawana shida wanaelewa vizuri mambo ya succession plan kwenye business. Wawe akina Abood, Mo dewji watoto wa bakheresa nk sina shida na watanzania ngozi nyeupe wawe waarabu, wahindi,au wapemba shida yangu waswahili ngozi nyeusi wawe wachaga au kabila yeyote.
Kumbuka haya mambo ya family business ni mapya kwa jamii zetu za kitanzania. 'Family business' kwa wengi ilikuwa mna ng'ombe, mna ardhi. Vijana (wanaume) walikuwa wanarithi hivi vitu, wasichana walikuwa wanachukuliwa kama mali ndo maana wakiolewa mnapata ng'ombe, harithi mali ya baba, akifiwa na mumewe ndo hivo ndugu wanakuja kuchukua walichochuma na marehemu na huenda na yeye akarithishwa kwa ndugu pia.
Mwaka ni 2020 , mambo yamebadilika ILA bado kuna zile akili za aidha kutoshirikisha watoto wa kike/wanawake kwenye mambo ya mali, au ku-exclude mke na watoto wote kwenye mambo ya mali ILI TU , ndugu zako wakija ukifariki wachukue mali. Ndo kitu kinachoumiza jamii zetu hizi, wanaume kuendekeza jamaa kuliko immediate family ( mke, watoto ) hivyo ukifa, kila ulichofanyia kazi kinakufa pia.
Nina uhakika, hata tukiwa na elimu ya kawaida, kama una maono, hauendekezi umalaya (hukupotezea muda, huleta magonjwa na ugomvi baina ya familia , watoto hawatakuheshimu), hauendekezi ndugu na huogopi kusemwa (wabongo ndo tatizo letu , tunafanya mambo membi ku-please wa nje huku nyumbani twaumia), tunaweza kuanza kuona biashara nyingi za kifamilia zikiendelezwa hata mwanzilishi akishatangulia.
Ndio maana huwezi kupeleka mtoto shule tu mradi apate elimu akaajiriwe. Kama wewe una duka lako, jaribu kuwashirikisha watoto wawe na maono na uelewa zaidi. Wakifunga shule, nenda nao shambani, kataliini mbugani muone mahoteli yanavoendeshwa. Chochote kuchangamsha akili awe na maono/inspiration ya kuanzisha vya kwake au kendeleza vya kwenu.
Nimeongea sana !