KERO Wafanyabiashara ya chakula acheni kurudisha mabaki

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Dar njaa kali, haiwezekani kutupa chakula. Na kwa taarifa yako kwenye mahoteli makubwa ndio tunaongoza kurudisha mabaki na kuyapasha kwenye oven yaani yanakuwa safi sana halafu ni matamu sana.
Mabaki hoyeee!!!
 
Mbagala hapo ile nafika tu nikakuta mchuzi kwenye kibakuli unarudishwa kwenye sufuria afu yale mabaki ya ugali yakawekwa kwenye doo la taka

Hapo hapo nikageuza njia

All in All usithubutu kula chakula cha baridi kamwe

Maana kwa hali zetu za maisha ni ngumu kula Sehemu classic pekee
 

Yaani hawa wafanyabiashara hata akili ya kuvukia barabara hawana ,umefanya la maana sana kutupa ,wengine wanapuliza mfuko kisha wanakuwekea kchambali au pilipili.

Mimi huwa nawachana sana nawaambia unapakaje mate kwenye vidole kisha unashika mifuko ya chakula? Mimi ndiyo maana sitaki kabisa Hg maana sitaki kula miuchafu.

Nashauri Bibi/Bwana afya wawe wanawapa semina za mara kwa mara hawa wafanyabiashara wa vyakula na mama lishe wazingatie sana usafi ,kuna sehemu nyingine hawashiki vitafunwa na mikono wanashika na vile vifaa kama vikolea vya kushikaia au atavaa nylon kisha anazichukua(hawa nawapa big up).

Nawashauri wanaokula kwa mama ntilie au chips chunguzeni maji wanayosuzia sahani ,ukiyaona unaweza ukaghairi kula maji machafu ya kuanzia asubuhi mpaka usiku ni hayo hayo ,hawayamwagi.
 

Yes wauza samaki wa mitaani dagaa mchele ni noma wanashika na mikono michafu na kukufungia ,aiseee ni hatari ,wafanyabiashara wa vyakula wengi 99% hawazingatii usafi.
 
Anatoka pale kukuhudumia.wala hanawi anazoa hivohivo na mkono anakuwekea
Tunajikaza tu.ndo Maisha yetu uswahilini
 
Walevi wengi wa Jiji Huwa wanaenda restaurant flan hivi zisizo na watu wachache na wanapenda kitu ya kuchoma,ukiwa mjanja maeneo hayo yapo kidongo chekundu nyuma.ya jengo zamani la ushirika,jitahidi kula vitu live,ukiwa morogoro tafuta kwa kimario nyuma.ya Msamvu,,ukiwa Arusha wajanja wanaenda kwa Mlomboo,cheza na mziki wa wanywaji wanajua Siri nyingi,kitu cha uchumi wa kati itakusaidia hakuna shortcut kwa life,Tena jifunze unoko wa kusimama hata pembeni wakati kitu kinaandaliwa,usiwaamini hao watu wa chips simama acha mapozi na kujiona.Life is short.
 
Kuna wauza chips zaidi ya mmoja nimewashuhudia wakiulizwa chips ni za moto basi wao wanazipima joto kwa mkono nyuma ya kiganja ...tatizo wengi ya wauza chips ni watu washamba wa vijijini wana tabia za uchafu wa asili wanashindwa kujua jema na baya.
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Yes wauza samaki wa mitaani dagaa mchele ni noma wanashika na mikono michafu na kukufungia ,aiseee ni hatari ,wafanyabiashara wa vyakula wengi 99% hawazingatii usafi.
Watu wanalishwa uchafu mno. Hata wauza matunda yaliyokatwa kama matikiti aise mtu anashika tikiti analikata vipande akimaliza anashika hela na watu hawashtuki kabisa. Ni uchafu sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…