Wafanyabishara walalamika ucheleweshaji wa ujenzi wa Machinga Complex Dodoma kikwazo cha kufanya biashara

Wafanyabishara walalamika ucheleweshaji wa ujenzi wa Machinga Complex Dodoma kikwazo cha kufanya biashara

tonicimmobility

JF-Expert Member
Joined
Jun 17, 2025
Posts
493
Reaction score
1,040
Zaidi ya wafanyabiashara 374 wa mbogamboga, wakiwemo wauza nyanya waliokuwa wakifanya biashara mbele ya Soko la Wazi la Machinga Complex jijini Dodoma, wameiomba serikali kuharakisha ujenzi wa marumaru (pavement) katika eneo hilo.

Wamesema ucheleweshaji wa mradi huo umeathiri kwa kiasi kikubwa shughuli zao za kiuchumi, kwani waliondolewa kwenye maeneo yao ya awali ili kupisha kazi ya ujenzi, lakini mpaka sasa mradi umesimama bila maendeleo.

Soma pia:


“Tuliambiwa tuondoke kwa muda mfupi tu ili wakamilishe kazi ya kuweka marumaru, lakini mpaka sasa kimya. Eneo letu limejaa mchanga na vifusi, wateja hawafiki tena,” amesema Bi. Debora Ndahani, mmoja wa wafanyabiashara.

Kwa sasa, wafanyabiashara hao wamesema mazingira waliyohamishiwa hayana miundombinu rafiki kwa biashara, hali ambayo imepelekea kuyumba kwa kipato chao na kushindwa kujikimu kimaisha.

Aidha, wameiomba Halmashauri ya Jiji la Dodoma kuhakikisha kuwa ujenzi wa pavement unakamilishwa mapema ili warudi katika maeneo yao ya biashara.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa soko hilo, Bw. Nyamageni Kingamkono, amewahakikishia wafanyabiashara kwamba zoezi la kuwarejesha litaanza ndani ya wiki mbili, mara tu vifaa vya pavement vitakapowasili kutoka viwandani.

“Lengo letu ni kuhakikisha wafanyabiashara wanarejea kwenye mazingira bora, salama na rafiki kwa shughuli zao za kila siku,” amesema Kingamkono.
 
Back
Top Bottom