GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 60,660
- 121,325
Baada ya kuzidiwa na mwenzake katika Ugombeaji wa ' almasi ' kubwa ya Mtaa wa Kariakoo sasa Tajiri wa Mbagala inasemekana ameingia katika ' bifu ' kali na zito la Kibiashara na Tajiri mwenzake huyo wa Kariakoo kiasi cha kupelekea kushawishi ' Mamlaka ' fulani kuzuia uzalishaji wa Vinywaji baridi vya Tajiri huyo wa Kariakoo.
Japo Tajiri huyu wa Mbagala anajifanya kuegemea katika kuzidiwa ' Kete ' na Tajiri wa Kariakoo hasa baada ya kushinda ' Tenda ' ya umiliki wa hiyo ' almasi ' iliyopo Kariakoo ila taarifa za ndani zaidi zinadai kwamba Tajiri wa Mbagala alinza kumchukia mwenzake wa ' Almasi ' ya Kariakoo hasa baada ya Yeye nae kuanza kutengeneza Vinywaji baridi vyenye ladha kama ya Kiwanda cha Tajiri wa Mbagala na kuziuza kwa ama bei ile ile na mwenzake ila ujazo ukiwa ni mkubwa au kuziuza kwa bei ya chini hali ambayo imempunguzia mwenzake Wateja na mapato.
Hivi ninavyo tiririka na kuserereka na huu uzi nimepata taarifa na mmoja wa Chanzo changu kilichopo katika Kampuni ya Tajiri wa Kariakoo kikisema kwamba sasa inaenda wiki ya pili kama siyo ya tatu Kiwanda cha Tajiri huyo wa ' Almasi ' iliyopo Kariakoo kimezuiwa kuzalisha Vinywaji na sababu walizopewa hazina miguu wala kichwa ila ni ' shinikizo ' kutoka kwa Tajiri wa Mbagala kama sehemu ya kummaliza na kumkomoa mwenzake huku akisahau kwamba Tajiri huyo wa ' Almasi ' ya Kariakoo kila siku anazidi tu kuwa Tajiri na hata hivi juzi kati amesikika akitajwa tena na bado akiwa ni Kijana tu.
Inasemekana kwamba endapo hili ' bifu ' zito na la chinichini la Wafanyabiashara Matajiri na maarufu Tanzania halitaingiliwa kati na Waziri Mwijage kuna hatari ya kuja kuathiri Sekta nzima ya Biashara nchini Tanzania hasa ukizingatia kwamba Wawili hao wana ' ushawishi ' mkubwa mno Kijamii japo mmoja wapo Wikiendi iliyopita alikuwa ni mwenye furaha akitokea Zanzibar na mwenzake Yeye wiki iliyoisha tu alinuna na kupelekea hadi Kuogelea kutoka Zanzibar hadi Dar es Salaam ukiachana na Yule Tajiri mwenzao mwingine ambayo hapa katikati ' alihenyeshwa ' na sasa hataki kusikia tena habari za mambo ya Biashara na ametulia zake tu sasa Kimya huku Marafiki zake wakiwa wanahangaika tu kila uchao Kuchota maji yanayojaa na kupambana na Vyura ambao wameweka Kambi ya kudumu katika eneo lao linalopakana na mkondo bahari.
Sijui kwanini Wafanyabiashara wakubwa huwa hawapendani lakini Sisi masikini tunapendana kweli.
Nawasilisha.