!!!!????Azam wana gundu la ajali sn..pole Kwa waliojeruhiwa
Defensive Driving ni muhimu sanaKipi ni bora kati ya uhai wa gari la nyuma au kuogopa faini??udereva ni pamoja na kujiongeza na sio kuogopa traffic tu
Defensive Driving ni muhimu sanaHivi Azam mmeshindwa kununua gari ?
Yaani utoke ubungo hadi Mbeya na kipanya
Mkuu, unaweza ku-overtake tu. Usikubali kuweka roho yako rehani kwa kuogopa kuvunja sheria. Mimi nilifanya hivyo mwezi uliopita, hapo hapo Kitonga. Nilikuwa napanda huo mlima, nikiwa na 4X4, mbele yangu kulikuwa na lori ambalo niliona kabisa lina matatizo. Spidi ilikuwa ni ndogo, na kuna wakati linasimama kabisa kwa kushindwa kupanda Mlima, nikaona kabisa hii ni hatari. Nikaamua kulipita, na hata dereva wa lori akanipa ishara nimpite. Kumbe kule mbele kuna trafiki wamepaki gari yao, wakiaangalia watu wanaopiga overtake mlimani. Nilipofika walipo, wakanipiga mkono, nikasimama. Trafiki mmoja wao akaniambia kuwa nimefanya kosa kupiga overtake. nikamwambia hapana, ile ni hatari, lile gari ni bovu, linashindwa kupanda mlima, ni hatari kuwa nyuma yake. Na akitaka, tusubiri pale wote mpaka lifike, alione mwenyewe kwa macho yake. Akaelewa, na kuniruhusu tu niondoke zangu.Najua kiusalama sio nzuri sana kuruhusu watu wawe wana overtake wakati wa kupanda mlima kitonga ila pia sio salama kwa gari ndogo kulazimisha ikae nyuma ya lori. Imagine lori linaenda kwa speed kama 10kph na huruhusiwi kuliovertake. Unaona kabisa lori linaelekea kushindwa kupanda mlima ila ukiovertake tuu unakutana na askari unakula fine tena hata hawajiulizi kwanini umeovertake. Ajali kama hii ya hiace ya Azam kusukumwa na lori pale kitonga isingetokea kama dereva angeamua kulipita hili lori ambalo lilikua linarudi riverse na kuibada hii hiace.
View attachment 2118465
Azam Media Limited (AML) inautaarifu umma kuwa wafanyakazi wake 12 waliokuwa wanakwenda mkoani Mbeya kwa ajili ya kazi ya kurusha matangazo ya mechi za Ligi Kuu ya NBC wamepata ajali baada ya gari lao kusukumwa na lori lililokuwa likirudi nyuma kwa dharula katika Mlima Kitonga.
Ajali hiyo imetokea mchana wa leo Jumapili, Februari 13, 2022.
Kwa msaada mkubwa wa ofisi ya mkuu wa Mkoa, kikosi cha Polisi Mkoa wa Iringa na Mganga mkuu wa Mkoa, majeruhi wamechukuliwa na matabibu wa Mkoa wa Iringa kwa matibabu.
Uongozi wa Azam Media Limited unawashukuru wote waliotoa msaada wa hali na mali na kuwaomba Watanzania wote kuwaombea majeruhi nafuu ya mapema.
Imetolewa na
Azam Media Limited
13, Februari 2022
View attachment 2118441
Kwan wakichua Coaster wasingepata ajali?kwa hiyo Azam mlitaka mtoe kafara naona limegoma! watu 12 na kipanya mpaka mbeya kweli! yaan mmekosa hata coaster kama sio uchawi ni nin
AZAM acheni kuajiri madereva wa daladala za Buguruni / Kariakoo kwani hawajui kanuni za udereva, wao bora liende mbele tu.Azam Media Limited (AML) inautaarifu umma kuwa wafanyakazi wake 12 waliokuwa wanakwenda mkoani Mbeya kwa ajili ya kazi ya kurusha matangazo ya mechi za Ligi Kuu ya NBC wamepata ajali baada ya gari lao kusukumwa na lori lililokuwa likirudi nyuma kwa dharula katika Mlima Kitonga.
Ajali hiyo imetokea mchana wa leo Jumapili, Februari 13, 2022.
Kwa msaada mkubwa wa ofisi ya mkuu wa Mkoa, kikosi cha Polisi Mkoa wa Iringa na Mganga mkuu wa Mkoa, majeruhi wamechukuliwa na matabibu wa Mkoa wa Iringa kwa matibabu.
Uongozi wa Azam Media Limited unawashukuru wote waliotoa msaada wa hali na mali na kuwaomba Watanzania wote kuwaombea majeruhi nafuu ya mapema.
Imetolewa na
Azam Media Limited
13, Februari 2022
View attachment 2118441
Najua kiusalama sio nzuri sana kuruhusu watu wawe wana overtake wakati wa kupanda mlima kitonga ila pia sio salama kwa gari ndogo kulazimisha ikae nyuma ya lori. Imagine lori linaenda kwa speed kama 10kph na huruhusiwi kuliovertake. Unaona kabisa lori linaelekea kushindwa kupanda mlima ila ukiovertake tuu unakutana na askari unakula fine tena hata hawajiulizi kwanini umeovertake. Ajali kama hii ya hiace ya Azam kusukumwa na lori pale kitonga isingetokea kama dereva angeamua kulipita hili lori ambalo lilikua linarudi riverse na kuibada hii hiace.
View attachment 2118465
Hao jamaa ni mandezi sana wanavizia kwa juu maana wanajua kwamba lazima uovertake maana malori hayawezi panda mlima huo vizuri...Mkuu, unaweza ku-overtake tu. Usikubali kuweka roho yako rehani kwa kuogopa kuvunja sheria. Mimi nilifanya hivyo mwezi uliopita, hapo hapo Kitonga. Nilikuwa napanda huo mlima, nikiwa na 4X4, mbele yangu kulikuwa na lori ambalo niliona kabisa lina matatizo. Spidi ilikuwa ni ndogo, na kuna wakati linasimama kabisa kwa kushindwa kupanda Mlima, nikaona kabisa hii ni hatari. Nikaamua kulipita, na hata dereva wa lori akanipa ishara nimpite. Kumbe kule mbele kuna trafiki wamepaki gari yao, wakiaangalia watu wanaopiga overtake mlimani. Nilipofika walipo, wakanipiga mkono, nikasimama. Trafiki mmoja wao akaniambia kuwa nimefanya kosa kupiga overtake. nikamwambia hapana, ile ni hatari, lile gari ni bovu, linashindwa kupanda mlima, ni hatari kuwa nyuma yake. Na akitaka, tusubiri pale wote mpaka lifike, alione mwenyewe kwa macho yake. Akaelewa, na kuniruhusu tu niondoke zangu.