Wafanyakazi 12 wa Azam Tv wapata ajali mlima Kitonga. Walikuwa wanaelekea jijini Mbeya kurusha matangazo ya NBC premier league

Magari ya Azam TV na madereva wao wachunguzwe.

Magari yao yanapata ajali mara kwa mara na zinakuwa mbaya na au zinatokea maaeneo hatari.

Kuna uwezekano madereva hawana ujuzi wa 'udereva wa kujihami' ambao kila dereva haswa wa 'Passenger Service Vehicles (PSV)' anatakiwa awe nao.
 
Pole kwao, majeruhi wapone haraka. Tahadhari muhimu na udereva makini unahitajika maeneo hatari.
 
Najua kiusalama sio nzuri sana kuruhusu watu wawe wana overtake wakati wa kupanda mlima kitonga ila pia sio salama kwa gari ndogo kulazimisha ikae nyuma ya lori. Imagine lori linaenda kwa speed kama 10kph na huruhusiwi kuliovertake. Unaona kabisa lori linaelekea kushindwa kupanda mlima ila ukiovertake tuu unakutana na askari unakula fine tena hata hawajiulizi kwanini umeovertake. Ajali kama hii ya hiace ya Azam kusukumwa na lori pale kitonga isingetokea kama dereva angeamua kulipita hili lori ambalo lilikua linarudi riverse na kuibada hii hiace.

View attachment 2118465
Mkuu, unaweza ku-overtake tu. Usikubali kuweka roho yako rehani kwa kuogopa kuvunja sheria. Mimi nilifanya hivyo mwezi uliopita, hapo hapo Kitonga. Nilikuwa napanda huo mlima, nikiwa na 4X4, mbele yangu kulikuwa na lori ambalo niliona kabisa lina matatizo. Spidi ilikuwa ni ndogo, na kuna wakati linasimama kabisa kwa kushindwa kupanda Mlima, nikaona kabisa hii ni hatari. Nikaamua kulipita, na hata dereva wa lori akanipa ishara nimpite. Kumbe kule mbele kuna trafiki wamepaki gari yao, wakiaangalia watu wanaopiga overtake mlimani. Nilipofika walipo, wakanipiga mkono, nikasimama. Trafiki mmoja wao akaniambia kuwa nimefanya kosa kupiga overtake. nikamwambia hapana, ile ni hatari, lile gari ni bovu, linashindwa kupanda mlima, ni hatari kuwa nyuma yake. Na akitaka, tusubiri pale wote mpaka lifike, alione mwenyewe kwa macho yake. Akaelewa, na kuniruhusu tu niondoke zangu.
 
Tatizo la askari wetu wa barabarani ni uelewa mdogo na kuendekeza rushwa ndogondogo. Kuna sehemu zingine kwa mjibu wa sheria hurusiwi kulipita gari la mbele yako lakini ki usalama unatakiwa kulipita, cha ajabu polisi wetu akiona hivyo ni fursa ya yeye kupata rushwa, hata uongee vipi hakuelewi. Binafsi kitonga huwa naovetake kwa usalama wangu.
 
Azam Media Limited (AML) inautaarifu umma kuwa wafanyakazi wake 12 waliokuwa wanakwenda mkoani Mbeya kwa ajili ya kazi ya kurusha matangazo ya mechi za Ligi Kuu ya NBC wamepata ajali baada ya gari lao kusukumwa na lori lililokuwa likirudi nyuma kwa dharula katika Mlima Kitonga.

Ajali hiyo imetokea mchana wa leo Jumapili, Februari 13, 2022.

Kwa msaada mkubwa wa ofisi ya mkuu wa Mkoa, kikosi cha Polisi Mkoa wa Iringa na Mganga mkuu wa Mkoa, majeruhi wamechukuliwa na matabibu wa Mkoa wa Iringa kwa matibabu.

Uongozi wa Azam Media Limited unawashukuru wote waliotoa msaada wa hali na mali na kuwaomba Watanzania wote kuwaombea majeruhi nafuu ya mapema.

Imetolewa na
Azam Media Limited
13, Februari 2022

View attachment 2118441

02A50002-25DB-4893-A921-31DDF03D4F7A.jpeg
 
Huu mlima huu!! Nasikia kuna mlima mwingine huko, Ushoto sorry Lushoto nao unatisha.
===
Ugueni poleni majeruhi, na nawaombea kwa Mungu mpone haraka.
 
kampuni kubwa bado mnapandisha watangazaji wenu kwenye magari na madereva wabovu wazembe na ndege mbeya zinaenda kilasiku
 
Azam Media Limited (AML) inautaarifu umma kuwa wafanyakazi wake 12 waliokuwa wanakwenda mkoani Mbeya kwa ajili ya kazi ya kurusha matangazo ya mechi za Ligi Kuu ya NBC wamepata ajali baada ya gari lao kusukumwa na lori lililokuwa likirudi nyuma kwa dharula katika Mlima Kitonga.

Ajali hiyo imetokea mchana wa leo Jumapili, Februari 13, 2022.

Kwa msaada mkubwa wa ofisi ya mkuu wa Mkoa, kikosi cha Polisi Mkoa wa Iringa na Mganga mkuu wa Mkoa, majeruhi wamechukuliwa na matabibu wa Mkoa wa Iringa kwa matibabu.

Uongozi wa Azam Media Limited unawashukuru wote waliotoa msaada wa hali na mali na kuwaomba Watanzania wote kuwaombea majeruhi nafuu ya mapema.

Imetolewa na
Azam Media Limited
13, Februari 2022

View attachment 2118441
AZAM acheni kuajiri madereva wa daladala za Buguruni / Kariakoo kwani hawajui kanuni za udereva, wao bora liende mbele tu.
 
Kafara hizo..kufanya kazi kwenye kampuni binafsi kuna mambo mengi sana yakutisha.
 
Najua kiusalama sio nzuri sana kuruhusu watu wawe wana overtake wakati wa kupanda mlima kitonga ila pia sio salama kwa gari ndogo kulazimisha ikae nyuma ya lori. Imagine lori linaenda kwa speed kama 10kph na huruhusiwi kuliovertake. Unaona kabisa lori linaelekea kushindwa kupanda mlima ila ukiovertake tuu unakutana na askari unakula fine tena hata hawajiulizi kwanini umeovertake. Ajali kama hii ya hiace ya Azam kusukumwa na lori pale kitonga isingetokea kama dereva angeamua kulipita hili lori ambalo lilikua linarudi riverse na kuibada hii hiace.

View attachment 2118465

1. Umewahi kupita Kitonga?

Maana naona ume comment kwa Mbwembwe kabisa!
 
Mkuu, unaweza ku-overtake tu. Usikubali kuweka roho yako rehani kwa kuogopa kuvunja sheria. Mimi nilifanya hivyo mwezi uliopita, hapo hapo Kitonga. Nilikuwa napanda huo mlima, nikiwa na 4X4, mbele yangu kulikuwa na lori ambalo niliona kabisa lina matatizo. Spidi ilikuwa ni ndogo, na kuna wakati linasimama kabisa kwa kushindwa kupanda Mlima, nikaona kabisa hii ni hatari. Nikaamua kulipita, na hata dereva wa lori akanipa ishara nimpite. Kumbe kule mbele kuna trafiki wamepaki gari yao, wakiaangalia watu wanaopiga overtake mlimani. Nilipofika walipo, wakanipiga mkono, nikasimama. Trafiki mmoja wao akaniambia kuwa nimefanya kosa kupiga overtake. nikamwambia hapana, ile ni hatari, lile gari ni bovu, linashindwa kupanda mlima, ni hatari kuwa nyuma yake. Na akitaka, tusubiri pale wote mpaka lifike, alione mwenyewe kwa macho yake. Akaelewa, na kuniruhusu tu niondoke zangu.
Hao jamaa ni mandezi sana wanavizia kwa juu maana wanajua kwamba lazima uovertake maana malori hayawezi panda mlima huo vizuri...
 
Back
Top Bottom