Wafanyakazi Bulyanhulu kugoma

I’m glad to this point, we are on the same level, ingawa jana ulisema otherwise, lakini, hakijaharibika kitu.

Jana nilisema kuwa wafanyakazi wa Serikali, yaani Federal na state kule US na UK, hawaruhusiwi kugoma, isipokuwa tu migomo inaruhusiwa kwenye Private kama ulizozitaja leo, hivyo vitengo viwili ukigoma unakuwa umejifukuza kazi mwenyewe,

lakini muajiri Private, anaruhusiwa kuwafukuza waajiriwa wake waliogoma na kukataa kurudi baada ya yeye kutoa deadline ya wao kurudi kazini, au kuajiri wengine temporary wakati ameweka offer kwenye table ya UNIONS,


Otherwise, naomba ku-retire sasa, ahsante mkuu!
 
Jana nilisema kuwa wafanyakazi wa Serikali, yaani Federal na state kule US na UK, hawaruhusiwi kugoma, isipokuwa tu migomo inaruhusiwa kwenye Private kama ulizozitaja leo, hivyo vitengo viwili ukigoma unakuwa umejifukuza kazi mwenyewe,

That is not entirely true either, because, state employees, are allowed to strike. Sio Marekani nzima lakini kuna State kama kumi or so, ambazo zinaruhusu hii kitu. Chache that I know on top of my head ni Illinois, Oregon, Pennsylvania and Minnesota. Hii mitaa kitu kisipoeleweka, watu wana-walk out tuu...
 

kisura you sound like HR sehemu fulani hivi
 

Heshima yako Kisura

Nakubaliana na wewe kuwa hii vita sio ya Tanzania peke yake bali ni ya dunia nzima. Tuliwahi kuwa na mjadala hapa JF mpaka tukafikia mahala pa kudhani kuwa watanzania ni wajinga. Anyway, binafsi bado nadhani watanzania wanahitaji uongozi madhubuti wa kutambua na kuunganisha nguvu zao hizi za rasha rasha ili kujikwamua kutoka katika lindu la haya Majangiri au "mapedophiles" wa uchumi wetu.

Mkataba aliosaini Chifu Abushiri ulikuwa na afadhali kuliko huu tunaousoma wa Barrick-Buzwagi. Ndiyo! kwani Abushiri aliambulia kipande cha nguo, na hata ile ardhi aliyowauzia wageni, baadae ilichukuliwa tena na kizazi cha mbele ya Abushiri. Lakini mkataba wa Barrick-Buzwagi unatoa madini yetu karibu na bure kwa hao hao wageni, lakini kibaya zaidi, kamwe, hakuna kizazi kinachoweza kuyarudisha hayo madini ardhini. Tunavirithisha vizazi vijavyo mashimo pamoja na magonjwa ya Saratani yatokanayo na uchafuzi wa mazingira.

Lakini viongozi wetu ambao wanaikodolea mimacho hiyo mikataba iliyowekwa sirini, wanatuambia bila kuona soni katika nyuso zao kuwa tusishangae mkataba wa Barrick-Buzwagi kwani hayo ni maajabu ya Musa. Barrick Bulyanhulu umesheheni maajabu ya Filauni. Wanaosema hivyo sio akina Kyoma bali ni wale walioiweka hiyo mikataba kibindoni. Kwa mantiki hii, binafsi naona njia zilezile zilizotumika kuwaondoa wale walionunua ardhi kutoka kwa Abushiri, ndizo zitumike kuwaondoa Barrick na dada zake.

Haya makampuni yanatumia njia haramu kuwalaghai viongozi wetu wachache ambao ni warafi na waliojilundikizia madaraka makubwa. Wanachukuwa mali asili bila manufaa kwa vizazi vya leo na vile vya kesho. Juhudi zozote za kuwafungashia vilago na kuwapigisha hasara ya kiama + kuwafilisi na kuwaweka Jela viongozi wetu walioshirikiana nao, zinatakiwa kuungwa mkono na kila anayeitakia nchi yetu mema. Ndio maana naona juhudi za migomo ya wafanyakazi zinahitaji uongozi madhubuti wa kupanua wigo wa madai na kubeba sura au vilio vya kitaifa na kimataifa.

Huu sio wakati wa kuangalia kama wafanyakazi wamevunja sheria au la. Sasa tukishagundua kuwa sheria zilizotungwa kihuni zinawapendelea Barrick, tuseme kwa sauti moja kuwa Barrick wana haki? Barrick wana haki gani Tanzania? Wameingia nchini kwetu kiharamu na sheria ya asili inasema haramu ni haramu tu. Katika suala hili ningependa watanzania tuwe na Deontological ethical approach kwamba the end does not justify the means. Hawawezi kuvunja sheria zetu za nchi kwa kughilibiana na viongozi wetu, alafu baada ya mikataba kusainiwa, wanataka wananchi watii huo uchafu.

Ni kweli, baadhi yetu huku mitandaoni yawezekana tukatofautiana na wananchi waliomstari wa mbele, ambao wanaonja makali ya maisha na wanajaribu kuthubutu kupambana na haya majangiri. Nadhani tunakosea kutaka kuvaa kofia ya uamuzi. Bajeti ya Serikali inatamka wazi kuwa madini yanachangia pato la taifa asilimia 5, lakini wakulima wetu wanachangia pato la taifa asilimia 44. Tunaweza kuwafukuza Barrick na tusiteteleke.

Sisi hatupashwi kuwa waamuzi katika suala kama hili. Barrick wanai -molest nchi yetu, hivyo naona kuna umuhimu wa kuangalia ni jinsi gani tunaweza kupenyeza mawazo ya kuifanya migomo kama hii ikajumuisha ajenda zinazo fichua unyama wa haya makampuni na kubadirisha taswira za mgomo kuwa wa kimataifa kwa manufaa ya taifa letu.

An ambitious agenda is required, given what is at stake. I believe it is within our reach through, especially given the growing strength of the global democracy movement that first gained public prominence with the massive protests that derailed the World Trade Organisation in Seattle in 1999. Agenda ziwe na mikakati inayolenga ku-transofm economic structures and establish economic and political democracy.
 

....very good & huge point lakini watu kama kina mwiba na upuuzi wote huu unaoendelea wanadiriki kuja hapa na kutuambia CCM ni chama makini,naamini itafika hiyo point na wananchi watasema na lolote liwe na liwe na watu kuingia mtaani kwa nguvu zote na hapo ndio moto utawaka
 

Bado ninasimaia my word, kuwa Us na UK, wafanyakazi wote wa State zote, na Federal hawaruhusiwi kugoma, hakuna State inaweza kukataa hilo kwa sababu by doing that automatically as a state una-lose some important Federal funds, kama vile driving speed limit, inayotolewa na Federal, ukikaataa as a State, una-lose some Highway Funds kutoka Federal,

Hakuna state inaweza ku-afford ku-lose hizo funds, except NY na LA, na haya yalikuwa makubaliano ya state baada ya depression, katika kuipa Federal power ya kupambana na tatizo hilo la Depression, step ya kwanza ilikuwa kutengeneza bara bara zpote za US na kuhakikisha kuwa unweza kwenda US nzima kwa bara bara, the next ilikuwa kupiga marufuku migomo kazini kwa US nzima kwa State na Federal, kama hizo ten sate zinaruhusiwa kuwa na migomo je ilishawahi kufanyika ili tuongee na mifano kamili?

Siku-walk out kwa sababau sielewi hapana, ninaelewa sana maana ndio hii ishu ya Labor inaangukia hasa kwenye professional yangu niliyoisomea huko US, nikiwa kwenye undergraduate, kwa hiyo sio ninabahatisha, hapana ninailewa kwa undani sana hii ishu ikiwa ni pamoja na kufanya kazi kwa muda mrefu under UNIONS, matatizo ya Barrick na wafanyakazi wake ni matatizo ya UNIONS zetu, ambazo kisheria ziko huru na siasa, ikiwa ni pamoja na serikali, lakini ufinyu wa kufikiri na kutenda wa viongozi wetu wa UNIONS, dnio unaleta hayo matatizo, ikiwa ni pamoja na rushwa, maana lazima viongozi hao walipewa rushwa na barrick, wakati wa kusaini mikataba ya kazi,

Kampuni kama Barrick, huwa zina Director wa Kampuni, anayeitwa Councellor, ambaye kazi yake ni ku-manouver wanasiasa na viongozi wa UNIONS, wakati wakusaini mikataba, na hao wakuu huwa ni wazoefu sana wa Afrika, ingawa wako Europe, tena siku hizi huwatumia wa-South Afrika kwenye ishu kama hizi, na sisi huwa hatujui kitu tunasaini tu baadaye tunakutwa na kilio tunaanza kuwatupia mawe wazungu, kumbe ni matatizo yetu wenyewe, hakuna kampuni yoyote ya kigeni inayoweza kumnyanyasa mtu US au Europe kwa ujumla maana UNIONS huko huwa hawachezi, tujifunze kutoka UNIONS za huko majuu!

Ahsante Mkuu!
 

Pia karibu NE yote, meaning Massachussetts, New Hampshire, Connecticut, Rhode Island na Vermont pia wafanyakazi wa State wanaweza kugoma kama hakieleweki!!!.........inawekwa "pickett line" hapo 24 hours, watu wanakunywa Dunkin Donnuts hata kama kuna Blizzard.
 
........ebo nilisahau Maine. Hizo sheria za baada ya great depression zina loopholes kibao na watu wanapita humo humo. Republicans mara nyingi wanazipa meno hizo sheria na kwa maana hiyo huko "south" kugoma inakuwa issue. Lakini Democrats huwa wana ng'oa hayo meno na kwa maana hiyo North na "the left coast" watu wanagoma kama kawa!!!!.
 
Bado ninasimaia my word, kuwa Us na UK, wafanyakazi wote wa State zote, na Federal hawaruhusiwi kugoma,

Babu mbishi wewe! Lakini wewe endelea tu kusimamia your "word" na kuamini unachotaka, unfortunately, it's not about what you believe, its about what the law states. Truth of the matter is, and, I quote;

"American law continues to regard public sector strikes in a substantially different manner. A strike by employees of the U.S. federal government may still be treated as a crime, and strikes by state and local employees have been explicitly allowed by courts or statutes in only 10 states."

It continues to say;

"State and local workers' strikes are permitted in Alaska, Hawaii, Idaho, Illinois, Minnesota, Montana, Oregon, Pennsylvania, Vermont and Wisconsin" end of quote.

...next ilikuwa kupiga marufuku migomo kazini kwa US nzima kwa State na Federal, kama hizo ten sate zinaruhusiwa kuwa na migomo je ilishawahi kufanyika ili tuongee na mifano kamili?

Well, let's see; I think mfano mmoja ambao kila siku ulikuwa unazungumzwa,ulitokea 2001 or 2002 kule Midwest. I also learned it was Minnesota's largest state employee strike(wenyewe walisema the first in 20years). Wakati huo Governor of State alikuwa Jesse Ventura. Parties involved zilikuwa kama Department of Human Services, and I believe Depart. Of Transportation also walikuwa kwenye mgomo.


Professional yako? Trust me, you and I both, ila wewe naona mwenzangu kidogo uko mis-informed.

Anyway, turudi Tanzania.


Nakubaliana nawe kidogo kwenye kwenye hili la kuwa, tatizo liko upande wetu. Lakini si kwamba umlaumu mfanyakazi aliye-sign contract, kwasababu yeye hana choice. Tatizo liko upande wetu sisi na sheria zetu za kazi. I am not very keen na sheria za kazi Tanzania, lakini I know enough to believe kuwa sheria zetu za kazi inabidi zifanyiwe marekebsho. Sheria zetu za enzi zile zilikuwa hazitubani sana kwasababu makampuni mengi yalikuwa ya serikali, na unajua baba/mama hawezi kumnyanyasa mwanawe, somehow employees got away with that. Siku hizi tuan multi-nationals companies zinaingia, mambo mengi yamebadilika hivyo sheria pia zinabadilika. Sheria zetu za kazi nadhani ziko legelege, na hao (akina Barrick & co) wanaweka terms zitakao-wabenefit wao. Labda swali muhimu ni kujiuliza, hivi kati ya sisi wazalendo pale nchini na hizi multi-national companies, who needs the other more? How much does Tanzania need foreign companies, and how much do foreign corporations need to operate in Tanzania? Ukweli ni kuwa wanatutaka zaidi ndio maana wako Tanzania, then why not work so we can set the rules?

Mwaka jana, China walifanya revolution moja, ambayo nadhani hata sisi tunaweza kutumia hii approach. Walikuja na sheria ambayo nadhani imekuwa in place May of 2007. Hii change ilikuja just months after Wal-Mart was forced to accept unions kwenye stores zake kule China. Wamarekani walikuwa wanajaribu ku-lobby ili sheria hii ibadilishwe, ili tu wao waweze kupata flexibility ya namna moja-somehow, wawe winners, ina maana waendelee kuwa-exploit wafanyakazi. Sheria hii ina-favor wachina and inaipa Unions a collective bargaining power and control over some rules. Na credit kwa kweli inabidi ipewe government, maana ndio imeleta hizi changes. Hii sheria imewakasirisha sana Americans and other global companies, in a way wamekuja na lobbying campaign kujaribu kubadilisha sheria. Lakini, baada ya years of reports of worker abuse, serikali ya China ikaamua kuvipa nguvu vyama vya kutetea wafanyakazi.

Kama Mheshimiwa Kyoma alivyo-state pale juu, hawa Barricks wanatu-molest, wamekuja na favoring a system that has led to widespread labor abuses, kutimua watu makazini on a workers moment's notice eti in the name of employment contracts. Tuamkeni waTanzania, they need us, huko Asia kumesha-saturate, next is Africa, watakuja tu huku Afrika, let us make terms on our benefits for the country and for employees, not them...

Sheria za kazi zinabidi ziwe na uwezo wa kuzipa unions a say in personnel matters, making it more difficult for companies to fire employees katika maswala ya compensation, working hours, leave, work safety and hygiene, insurance, benefits, etc. Sasa halfu tuone jinsi hao wazungu watavyokuja kutu-lobby. Kwa kweli, wizara yet ya kazi must press foreign companies which dominate uchimbuaji madini's among others to do more for workers.

Demands za wafanyakazi wa bulyanhulu are so reasonable. Anyhow, this will happen, mark my words. Mungu ibariki Tanzania.
 

Kwa hiyo haki haiwezi kutendeka. Je tunajifunza nini kwa yale yanayotokea katika nchi za wenzetu hususan Nigeria.

Nani anawaamrisha FFU kwenye mgodi binafsi? Serikali inalipwa kiasi gani kwa kazi za FFU? Je pesa za walipa kodi hazitumiwi vibaya wakati tunaambulia chini ya 3%
 
Najua unaongelewa mgomo wa Barick hapa, lakini nimefurahishwa na point zilizotolewa na Kisura na FMES. Kule kwenye jukwaa la uchumi tulikuwa tunaongelea mambo ambayo yanafanana na kinachoendelea hapa nchini...Weak UNIONS.

Naomba niwakilishe mchango wangu kwa maexpert ili nipate mwanga zaidi. Naona bado tuna hangover ya JUWATA.

 
Huu mgomo umefikia wapi? Walio na taarifa, je wameweza kuajiri wafanyakazi wapya? nini hatma ya wale waliofukuzwa kama wapo? Vipi madai yao?
 
Hongera ujumbe mtamu ila sijui kama unewafikia walengwa, yaani wafanyakazi na viongozi wao katika hivyo vyama vya wafanyakazi, watu bado wako kwenye enzi zile za uchumi dola, hivi sasa ni uchumi huria hivyo vyama vya wafanyakazi makini vyenye uongozi makini na ambavyo ni mali na vinatokana na wafanyakazi wenyewe (muundo na kanuni)vinapaswa kuundwa kwa maslahi ya wafanyakazi. Kwa wale wenye uelewa na ambao tumeona vyama hivyo katika nchi za kibepari! samahani zinazofuata mfumo huria tuendelee kuwaelimisha wenzetu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…