DOKEZO Wafanyakazi Hospitali ya K's - Mbeya wana hali mbaya, Wamiliki nao hawajali na wanawajibu kwa nyodo

DOKEZO Wafanyakazi Hospitali ya K's - Mbeya wana hali mbaya, Wamiliki nao hawajali na wanawajibu kwa nyodo

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Hawa k'S Wana ajiri watu ambao hawana professional yeyote

Kuna jamaa alisoma HKL lakini ni doctor pale

Unategemea huyu akiacha kazi ataajirika wapi?

[emoji28][emoji28] taratibu basi ankali mbona unatupanga hivi. HKL akawe Daktari? Sio kihivyo ankali
 
[emoji28][emoji28] taratibu basi ankali mbona unatupanga hivi. HKL akawe Daktari? Sio kihivyo ankali
Mkuu unabisha nini?

Kuna jamaa kasoma ivumwe secondary advance level ni daktari K'S

Na ivumwe hamna comb ya sayansi

Na huyo jamaa alisoma education Ruco aka disco first year
 
Nakumbuka mwaka jana niliona kuna memba mmoja wa JF aliandika kuhusu huduma mbovu zinazotolewa na Hospitali ya K’s iliyopo Mbeya, sikuwa nimeweka umakini sana lakini kilichotokea wiki hii ndio nimeona kweli hiyo hospitali ni ya kidwanzi.

Wiki moja iliyopita nilifika hospitalini hapo si kwa lengo la kutibiwa bali kumsalimia ndugu yangu ambaye ni mtumishi wa Hospitali ya K’s kwa miaka kadhaa sasa.

Baada ya stori zetu za hapa na pale nikabaini kuwa mshkaji hana furaha na sura yake ni kama imekosa nusu, nikamdadidi tatizo nini hakuweza kuniambia, akasema tutazungumza baadaye, kwa kuwa nilikuwa ni mwenyeji wake kwa wiki nzima haikuwa tabu.

aadaye jamaa alinisimulia mambo mengi hasa jinsi watumishi wa hospitali hiyo wanavyopata tabu hasa kiuchumi na kunyanyasika.
Nadhani litakuwa jambo zuri nikimnukuu yeye mwenyewe japokuwa naweza kutoandika moja kwa moja kwa maana ya neno kwa neno alilosema lakini ukimaliza kusima ujumbe utakuwa umeeleweka na kama ni hatua basi Serikali au taasisi husika ziingilie kati kuwasaidia ndugu zetu hao.

“Hospitali ya K’s ina jina kubwa hapa Mbeya lakini ukweli ni kuwa kinachoendelea ndani ni aibu sana, kwanza hapa ninavyokwambia tunadai mishahara ya miezi 9 na huu Juni unaenda kuwa wa 10.

“Mara ya mwisho tulilipwa Februari 2023 lakini nyuma ya haoo kuna mishahara mingine ambayo tunadai, tukiuliza wanatuambia watalipa, mara NHIF hawajalipa, kwa ufupi blabla zinakuwa nyingi.

“Kuna kipindi madaktari waligoma kwa kutolipwa stahiki zao, lakini wakapewa majibu ya shombo kutoka kwa viongozi wa juu wakiwemo wamiliki wenyewe.

“Ilifika hatua jamaa wakaanza kujibu kwa nyodo kuwa hata tukiondoka wao wanaweza kubaki na watoto wao ambao ni madaktari tuko nao hapa, watafanya kazi kama kawaida.

“Kuna muda inafikia watu wanafukuzwa kazi kwa makosa ya ajabuajabu ilimradi tu wasiweze kudai maslahi yao, pia kuna washkaji wengi tu wameacha kazi hapa kutokana na mambo kutoeleweka.

“Kwa ufupi Wafanyakazi tuna hali mbaya na sisi ndio tunaodili na afya za watu, unadhani hapo kuna umakini kweli?”

Hiyo ni sehemu ya maelezo ya ndugu yangu, naomba Serikali iingiilie kati kuwasaidia wana hali mbaya ndugu zetu ambao wanadili na afya za watu, unadhani hapo tutegemee nini?

==================

Updates...
Walipotafutwa kujibu madai hayo kwa nyakati tofauti, Afisa Uhusiano wa Hospitali ya K’s, Suma Kabuje na Meneja wa K’s wote walisikiliza hoja kisha wakaomba muda kabla ya kujibu lakini bado hawajapatikana kutoa ufafanuzi.

Pia soma : Hospitali ya K’s Mbeya mna huduma mbovu
Hiyo ni hospitali binafsi, wasipokulipa mshahara wa mwezi mmoja tu, unakuwa unafanya nini zaidi ya kuachana nao. Lakini pia msisahau, hata hizi hospitali na taasisi za serikali, zingekuwa zinalipa mishahara toka kwenye kapu lake, watu wasingelipwa mishahara miaka. Tunapenda sana kulipwa ujira kwa output zisizoonekana.
 
Mkuu unabisha nini?

Kuna jamaa kasoma ivumwe secondary advance level ni daktari K'S

Na ivumwe hamna comb ya sayansi

Na huyo jamaa alisoma education Ruco aka disco first year
Sawa mkuu, Alishawahi Kukuhudumia huko hosp kama Daktari? Kamą ni Hivyo basi unaweza ukatoa taarifa kwa mamlaka husika za usimamizi.
Kumbuka Sio Wote wanaofanya Kazi Hospitalini ni Wanataaluma hivyo ya Afya.
 
Hiyo ni hospitali binafsi, wasipokulipa mshahara wa mwezi mmoja tu, unakuwa unafanya nini zaidi ya kuachana nao. Lakini pia msisahau, hata hizi hospitali na taasisi za serikali, zingekuwa zinalipa mishahara toka kwenye kapu lake, watu wasingelipwa mishahara miaka. Tunapenda sana kulipwa ujira kwa output zisizoonekana.
Mkuu, Kama wafanyakazi wake Hawana Output Kwanini asiwasimamishe Kazi? Atafute Wanaoleta Tija kwa taasisi.
Lakini Kitendo cha Kubakia Kazını Bila Kulipwa ujira wao sio sawa.
 
Itakua na wewe ni miongoni mwa watu waliofukuzwa kwa wizi so umeona ulete majungu,ks hospital mbeya is the best,maabara yao ni kati ya maabara mora kabisa katika vipimo
Naona wanekutuma kujibu mkuu

Tetea ugali chief tuko Nyuma yako
 
Mungu ni mwema niliwahi kutibiwa hapo K"s hospital, what a memory sitasahau madhara ya SP hadi Leo sipatani na mafuta yenye sulphur.

Tuache utani Mbeya mishikaki ni mitamu sana, kidogo na pale Njombe stendi.

Soko la uhindini enzi hizo ugali mishikaki nawaombea like soko lirudi, uhindini imechakaa, imezubaa.
 
Mkuu unabisha nini?

Kuna jamaa kasoma ivumwe secondary advance level ni daktari K'S

Na ivumwe hamna comb ya sayansi

Na huyo jamaa alisoma education Ruco aka disco first year
Mkuu sio kila anayevaa koti jeupe ni daktari, inawezekana ulimuona muhudumu wa restaurant amekatiza hospital ukajua ni daktari 😅😅😅
 
Back
Top Bottom