Bundi ameendelea kutua na kunguruma kwenye taasisi hii maarufu hapa jijini na iliyojijengea heshima kubwa kwani Kwa kipindi Cha mwezi December mpaka hivi sasa mambo kadhaaa yamejudhihirisha licha ya juhudi za makusudi kuchukuliwa Ili kunusuru hali hiyo.
Kumeshuhudiwa upunguzwaji wa ghafla wa wafanyakazi ikiwemo waalimu Kwa kipindi kifupi ambao haujaenda sawia na ulipwaji wa stahiki zao Kwa wakati ikiwemo mafao pamoja na michango ya hifadhi ya jamii hali kadhalika masalia ya mishahara ambayo haikulipwa wakati wa janga la Uviko. Licha ya juhudi za makusudi za kulipa mishahara ya mwishoni mwa mwaka jana Ili kutuliza hali.
Hali hii inaiweka Taasisi hiyo katika hatari ya kuburuzwa katika Vyombo vya kisheria na kuwekwa hadharani katika Vyombo vya habari.