DOKEZO Wafanyakazi wa Joshmal Hotel (Arusha) hatujalipwa mishahara wala kuwekewa NSSF kwa muda mrefu

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Naandika ujumbe huu kwa niaba ya wafanyakazi wenzangu wa Joshmal Hotel, Arusha, ili kuwasilisha changamoto kubwa tunayokabiliana nayo mahali pa kazi.

Sisi wafanyakazi tumekuwa tukifanya kazi kwa muda wa zaidi ya miezi sita hadi mwaka mmoja bila kulipwa mishahara yetu. Zaidi ya hayo, hatujawahi kuwekewa michango ya NSSF tangu tulipoanza kazi, hali ambayo inaendelea kwa zaidi ya miaka mitatu sasa.

Kutokana na hali hiyo, baadhi ya wafanyakazi wamelazimika kuacha kazi na kutafuta vibarua vingine ili kuweza kujikimu kimaisha, baada ya kubaini kuwa mwajiri wetu hana mpango wa kulipa mishahara yetu wala kushughulikia madeni tunayodai.

Kwa sasa, tupo zaidi ya wafanyakazi 15 tunaodai haki zetu za msingi za ajira. Cha kusikitisha zaidi ni kwamba hali hii si ya mara ya kwanza kutokea, kwani tulipoanza kazi tulikuta pia kuna madai ya wafanyakazi waliotutangulia, ikiwa ni pamoja na stahiki zao za NSSF na mishahara isiyolipwa.

Hali hii inatoa picha kuwa kuna tatizo la muda mrefu la kutolipa wafanyakazi stahiki zao, jambo linaloathiri maisha ya wafanyakazi na kuonekana kama unyonyaji wa nguvu kazi bila kuzingatia sheria za kazi.

Tunaomba msaada wa kupaza sauti ili haki yetu iweze kupatikana. Kwa dhati kabisa, tumedhulumiwa haki zetu za msingi kama wafanyakazi.

Tunaiomba Wizara ya Kazi na wadau wengine husika waingilie kati suala hili kwa haraka ili kuhakikisha haki za wafanyakazi zinalindwa na sheria za kazi zinazingatiwa ipasavyo.

ynz9ahfqnn2j1kxmzdhr.jpg
 
Unaweza kuacha kazi, boss makini hawezi kulipa watu useless, may be ameona hakuna mnachoingiza zaidi ya makelele, na hakuna mtu asiyeliowa miezi 6 na akaendelea na kazi labda hawe mwizi.
 
Ninyi ni wezi ,miezi sita na bado mnaenda kazini ? ,umasikini wa akili huu
 
kwa NSSF walivyo wa moto sasa hivi walitakiwa kuwa mahakamani kwa sababu kuna Task Force inayozunguka kutafuta waajiri kama hawa, Nendeni Idara ya kazi Arusha mpeleke kilio chenu na vile vile piteni kwa mkuu wa wilaya, mkifukuzwa kazi mnaenda kumalizana nae CMA
 
Naandika ujumbe huu kwa niaba ya wafanyakazi wenzangu wa Joshmal Hotel, Arusha, ili kuwasilisha changamoto kubwa tunayokabiliana nayo mahali pa kazi.

Sisi wafanyakazi tumekuwa tukifanya kazi kwa muda wa zaidi ya miezi sita hadi mwaka mmoja bila kulipwa mishahara yetu. Zaidi ya hayo, hatujawahi kuwekewa michango ya NSSF tangu tulipoanza kazi, hali ambayo inaendelea kwa zaidi ya miaka mitatu sasa.

Kutokana na hali hiyo, baadhi ya wafanyakazi wamelazimika kuacha kazi na kutafuta vibarua vingine ili kuweza kujikimu kimaisha, baada ya kubaini kuwa mwajiri wetu hana mpango wa kulipa mishahara yetu wala kushughulikia madeni tunayodai.

Kwa sasa, tupo zaidi ya wafanyakazi 15 tunaodai haki zetu za msingi za ajira. Cha kusikitisha zaidi ni kwamba hali hii si ya mara ya kwanza kutokea, kwani tulipoanza kazi tulikuta pia kuna madai ya wafanyakazi waliotutangulia, ikiwa ni pamoja na stahiki zao za NSSF na mishahara isiyolipwa.

Hali hii inatoa picha kuwa kuna tatizo la muda mrefu la kutolipa wafanyakazi stahiki zao, jambo linaloathiri maisha ya wafanyakazi na kuonekana kama unyonyaji wa nguvu kazi bila kuzingatia sheria za kazi.

Tunaomba msaada wa kupaza sauti ili haki yetu iweze kupatikana. Kwa dhati kabisa, tumedhulumiwa haki zetu za msingi kama wafanyakazi.

Tunaiomba Wizara ya Kazi na wadau wengine husika waingilie kati suala hili kwa haraka ili kuhakikisha haki za wafanyakazi zinalindwa na sheria za kazi zinazingatiwa ipasavyo.

View attachment 3602820
Yaani jengo lote hilo lina wafanyakazi 15 tu? Namshauri auze jengo akafanye biashara nyingine ,yaani kulipa mishahara/NSSF staffs 15 hawezi? Yaani kuwalipa milioni 9 hao wafanyakazi hawezi kwa mwezi? Pesa ya kujenga alitoa wapi?
 
Back
Top Bottom