Wafanyakazi wa ndani kulindwa na sheria mpya

Wafanyakazi wa ndani kulindwa na sheria mpya

kbm

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2012
Posts
5,224
Reaction score
1,677
Serikali kupitia Wizara ya Kazi na ajira iko katika mchakato wa kuanzisha sheria ya mkataba wa wafanyakazi wa majumbani.
Mkataba huo utasimamia na kuteteahaki, maslahi, afya na usalama, mazingira ya utendaji kazi, pamoja na uingizwaji katika makato ya hifadhi ya mifuko ya jamii kwa wafanyakazi hao.
Hatua hiyo imefuata mkutano wa kimataifa wa mkataba namba 189 wa kazi zenye staha kwa wafanyakazi wa majumbani uliofanyika Geneva, Uswis mwaka 2011.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana katika ofisi za Shirika la Kazi la Umoja wa Mataifa (ILO), Mkurugenzi wa Ajira, Ally Msaki, alisema serikali imeandaa mpango kazi kwa kuazna na uzinduzi wa dodoso zitakazotumika kufanyia utafiti wa sheria hiyo.
Alisema utafiti huo utaanza Juni maka huu hadi Julai mwakani na pindi utakapokamilika, itapelekwa bungeni kama muswada na baadayekupitishwa na kuwa sheria.
Kwa mujibu wa ripoti ya takwimu zaILO ya mwaka 2010, bara la Afrika lina wafanyakazi wa ndani milioni tano na asilimia 70, kati yao ni wanawake.
Kadhalika katika takwimu za mwaka huu zinaeleza kuwa wafanyakazi wa ndani Tanzania Bara ni asilimia 1.2 ya soko la ajira na asilimia 0.7 kwa Zanzibar.
Ripoti pia inaeleza kuwa miongoni mwa wafanyakazi hao wa ndani wanafanya kazi katika mazingira magumu pasipo kupewa ujira wao sahihi.
Mkurugenzi wa ILO Kanda ya Afrika Mashariki na Kati, Alexio Musindo, alisema kuanzishwa kwa mkataba namba 189 ya mwaka 2011 kutapelekea kuwapo kwa uhuru wa mfanyakazi wa ndani, masaa ya maalum za kufanya kazi, uboreshwaji wa mazingira ya kazi pamoja na kulipwa kwa wakati.
Alisema mpaka sasa Maurituis pekee ndiyo inayoitumia sheria hiyo.
CHANZO: NIPASHE
 
Serikali itafanya jambo jema kama italifanikisha hilo kwani itaweka na umri muafaka wa mtu kuajiliwa kuwa mfanyakaz wa ndani kwa sasa wafanyakaz wengi wa ndani ni watoto wadogo ambao wengi wao wanakosa ata elimu ya msingi na kufanya kaz katika mazingira magumu na mda mwingine mishahara inaishia kupata milo tu.


Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
Itasaidia sana mana hawa dada zetu wanachukua asilimia kubwa ya maisha yetu we have to treat them fairly kibinaadamu zaidi as they are human bng ka cc. Sa imagne wwe ofcn bos wako akupelekeshe ovyo hope hutofurahi.nawachukia watu wngne wanaochukulia eti dada sio ndugu yako anaondoka muda wwte! Dada ni zaidi ya ndugu jaman tuwaheshmu na kuwathimn na tuswazalau eti kisa hajasoma jamn unaona wa kumbuluta ovyo wengne wanawasingizia dada wez eti kila ktu kikipotea ndan ni dada wakat sa nyngne sio jaman mabosi kuwen na utu na ubinadamu just put year self on her shoes je ungeweza? Hiyo sheria ije tuu naunga mkono hoja

Sent from my BlackBerry 9360 using JamiiForums
 
Back
Top Bottom