Wafu walio hai na siri za kuzimu zilizofichwa kwenye ulimwengu wa roho

Asante sana. Huu ndio ufahamu ninao utaka. Asante sana lakini nina swali moja zaidi: Ikiwa roho haihitaji ubongo ili kufikiri, kukumbuka na kutambua, kwa nini uharibifu wa sehemu mbalimbali za ubongo unaweza kubadilisha kabisa kumbukumbu, utu, lugha, hisia na hata utambulisho wa mtu? Je, hilo halimaanishi kwamba kile tunachokiita “nafsi/utambuzi” kinategemea ubongo kuliko tunavyodhani? Shukrani.
 
Kuzimu ni wapi?
Neno "Kuzimu" linamaanisha makao ya kiroho ya watu waliokufa au kaburi la jumla la wanadamu, na haliwakilishi eneo lolote halisi la kijiografia duniani.

Katika tafsiri ya asili ya Kiebrania na Kigiriki (Sheoli na Hadesi), neno hili lilitumika kumaanisha hali ya kutokuwepo kwa uhai ambapo wafu wote—wema na wabaya—huenda baada ya kufa bila kujali matendo yao.
 
utambuzi wetu unategemea ubongo kwa asilimia kubwa sana, kwani uharibifu wa neva hubadilisha kabisa kumbukumbu, lugha, na utu wa mtu kama inavyoonekana kwa wagonjwa wa Alzheimer's au majeraha ya kichwa.

Upande wa sayansi ya neva na msimamo wa kimaada (Materialism), jambo hili linaonyesha kuwa kile tunachokiita "nafsi" au "utambuzi" si kitu cha kiroho kinachojitegemea, bali ni zao la moja kwa moja la michakato ya kemia na umeme ndani ya seli za ubongo...!
hivyo ubongo ukiharibika au kufa, utambuzi nao unabadilika au kutoweka.
 
Mshana Jr
Mhubiri 12:7
Nayo ROHO humrudia MUNGU....
Unaweza kufafanua hili fungu tafadhali....

The LORD is my shepherd!
Fungu unalolitaja linatoka katika Kitabu cha Mhubiri 12:7, linalosema: "Nayo mavumbi kuirudia nchi kama yalivyokuwa, Nayo roho kumrudia Mungu aliyeitoa."

Fungu hili ni muhimu sana na linajibu moja kwa moja mjadala wetu uliopita kuhusu jinsi mwili (ubongo) na utambuzi (roho) vinavyofanya kazi pamoja, na nini hutokea wakati wa kifo.

Ili kulielewa vizuri, ni lazima kwanza tuangalie kanuni ya uumbaji katika Mwanzo 2:7, ambapo Biblia inasema Mungu alitengeneza mwili kwa mavumbi ya ardhi, kisha akaipulizia pumzi ya uhai (roho), na mtu akawa nafsi hai.

Kifo ni mchakato wa uumbaji huo kurudi kinyumenyume, nao unafafanuliwa katika mambo haya..!

Kuvunjika kwa "Muunganisho" (Mwili na Roho Kutengana)Mhubiri anaonyesha kuwa mwanadamu amefanywa kwa vitu viwili vikuu vinavyokutana:

mwili wa kibaolojia (mavumbi) na nguvu ya uhai inayotoka kwa Mungu (roho).

Mtu anapokufa, ule muunganisho unakatika. Mwili uliokuwa ukitunza kumbukumbu na utu kupitia ubongo unarudi udongoni.
Ile nguvu iliyokuwa inaupa mwili uhai (roho) inarudi kwa Chanzo chake, ambaye ni Mungu
 
akili ni zawadi kuu tuliyopewa ili iwe chombo cha kuchakata, kujifunza, na kupanua upeo wa maarifa mapya kila siku. Uwezo huu wa kufikiri kwa kina, kuhoji mambo, na kutafuta majibu ndio unaomtofautisha mwanadamu na viumbe wengine wote duniani.

Kubisha bila ithibati ama kwa hadithi za kubahaisha ni ukosefu mkubwa wa akili na maarifa
 
Kuna tambiko wameambiwa watoe kondoo jike na dume mkuu kondoo ina maana gan kwenye ulimwengu wa roho?
Kutuliza hasira na kuleta amani.. Ikiwa kuna laana, ugomvi, au mikosi inayofuatilia familia, kondoo hutumika kama "kichocheo cha amani" ili kutuliza nguvu hasi au hasira ya mizimu/roho.

Upatanisho na Utakaso:
Upole na usafi wa kondoo hutumiwa kufuta makosa au makosa yaliyofanywa na wanadamu dhidi ya ulimwengu wa roho.

Maana ya Kondoo Jike (Mwanamke/Uzazi)
Kondoo jike anawakilisha nguvu ya kike ya kiroho (Feminine Energy). Kwenye tambiko, uwepo wake unamaanisha kuunganisha na kuendeleza uzao
 

Adam aliposhindwa kujibu swali hili “Adam, upo wapi?” Ndilo lkliloleta haya yote. Mpaka leo chanzo kinamuita mwanadamu na hatujawahi kujibu. Tukapoteza uhusiano na chanzo cha asili yetu, imsababisha roho za walioondoka kukwama hivyo inabidi wale mwanga kupitia ndugu zao.

Swali jingine Kaini akaulizwa “ Yupo wapi Habil ndugu yako?” Akashindwa kujibu pia. Tukapoteza uhusiano kati yetu wenyewe tukazidi kupotea mpaka leo
 
Kidini kuwa mfu ni kuwa dhambini ...watakatifu waliokufa hawapo kuzimu kwa sababu kuzimu ni hapa tunapoishi sasa tukiwa hai ndiyo maana mwisho wa kiumbe kuhesabiwa dhambi ni siku ya kufa kwake kama kuna maisha ya kuzimu kwanini dhambi zikomee kifo na kwa nini kutubu kukomee kifo hao wanaoishi kuzimu yaani marehemu kama msemavyo nyinyi kwanini wasitubie dhambi huko walipo kwa jina la Yesu maana bado siku ya kihama ambayo ni mwisho wa msamaha wa Mungu ..Yesu ana sema waache wafu wazike wafu wao ..hivyo aliye hai mwenye dhambi huyo ni mfu na aliye fia dhambini huyo ni mfu kwa mujibu wa biblia na injili.
 
Haya mambo yote yapo lakini ni ngumu kueleza mtu akakuelewa labda akaone mwenyewe.

Nakupa uzoefu wangu ambao binafsi nimepitia na kuona pia.Kwanini ntakwambia roho ni kitu real.Kuna swali niliuliza kwa mleta mada kwamba inawezekana vipi unamjua mtu alikuwa tuseme Singida lakini ukienda Kigoma unamkuta mtu huyo huyo na ulimuacha Singida?(Jibu lake ni kwamba roho au nafsi yake haipo naye tena).Hiki kitu nimekishuhudia nikiwa na akili zangu timamu.

Jehanamu,kuzimu,heaven hivi vyote ni vitu real.Ntakupa tena mfano mwingine.Katika harakati zangu za maisha niliwahi kukutana na majini(uhalisia ni kwamba huwezi kuyaona kama ambavyo sisi binadamu tunaonana).Hii inakupa picha kwamba kuna maisha nje ya hii dunia tunayoweza kuona.Ndio maana katika falsafa kuna kitu wanaita physical world(which is seen) and spiritual world(which is not seen)

Mbali na hivyo,wanafalsa hao hao wamekwambia binadamu ana sehemu ya physical body(hii tuliyo nayo ambayo inaonekana) na spiritual body(ambayo hiko ndani yetu inayotawala mawazo na matendo yetu)

Kiufupi heaven is real and hell is real(nina experience kibao za kukuonyesha hivi vitu vipo japo unaweza usiamini ukaona ni story zizile ambazo huwa unazisikia lakini kwangu ni tofauti maana naongelea vitu nilivyopitia mimi)
 
Unakuwa ulivyo kuwa kabla ya kuzaliwa hadi nguvu za asili (Mungu)zikupeleke zitakapo zenyewe sawa sawa na mapenzi yake
Mhubri 12:7
anasema ROHO humrudia MUNGU....
na chanzo cha mwanadamu ni MUNGU kama ilivyo kwa mimea ilivyotoka ardhini.....na inarudi ardhini.... Hiyo hali ya kuwa kabla hatujazaliwa inakuwaje? Maana watoto hua wanacheza tumboni, maana mtu mfu hajui neno lolote ....karibu mkuu!
 
Wewe haya yote umeyaandika tokea wapi, yani umeyajuaje? Maana ni kama uko zako kuzimu una report! 🤣
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…