beth
JF-Expert Member
- Aug 19, 2012
- 3,881
- 6,377
Mahakama kuu Kanda ya Arusha leo Alhamis Desemba 31 imewapa dhamana wafuasi 19 wa Chadema waliokuwa watuhumiwa kwa makosa ya uhujumu uchumi.
Dhamana hiyo imetolewa na Jaji wa Mahakama hiyo Mohammed Gwae baada ya mahakama ya hakimu Mkazi kushindwa kutoa dhamana kutokana na mahakama hiyo kutokuwa na mamlaka ya kufanya hivyo.
Watuhumiwa hao walikuwa wanashitakiwa katika mashauri tofauti namba 69,70 na 71 la Mwaka 2020.
Wafuasi hao akiwepo mwanafunzi Godliving Masawe (22) ambaye alitaraji kujiuga na chuo kikuu baada ya kufaulu kidato cha sita wanadaiwa kutenda kosa la kuundwa genge la uhalifu na kuwashawishi watu kutenda uhalifu katika eneo la bondeni Anex jijini Arusha.
Jaji Gwae alisema Mahakama imeamua kutoa dhamana Kwa watuhumiwa watakaotimiza masharti ikiwa ni pamoja kutoa fedha tasilimu Sh10 milioni au mali yenye hati na isiyohamishika.
Masharti mengine yaliyotolewa na Mahakama Hiyo ni kuwa kila Mtuhumiwa kuwa na Mdhamini mmoja mwenye barua inayotambulisha eneo analotoka ambaye atatakiwa kusaini bondi ya Sh10 milioni.
Watuhumiwa 10 kati ya 19 wamefanikiwa kutimiza masharti ya dhamana na wapo nje kwa sasa lakini wanane kati yao bado hawajafanikiwa kutimiza masharti ya Dhamana hivyo wamerudishwa rumande na zoezi la kutimiza masharti ya dhamana litaendelea.
Kesi hiyo awali ilikuwa chini ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha na kutokana mahakama Hiyo kutokuwa na Mamlaka ya kutoa dhamana katika makosa ya Uhujumu uchumi kesi hiyo ilihamishiwa mahakama kuu Kanda ya Arusha.