Pre GE2025 Wafuasi CHADEMA wavamia nyumbani kwa Mbowe kumlazimisha achukue Fomu ya kugombea Uenyekiti

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Nadhani siasa hizi zimezoeleka zaidi kufanywa na wanaCCM tangu enzi za akina Kingunge (Castory) Ngombale Mwiru. Hivyo kuanza kutumiwa na Mbowe 2024 ni kumrudisha nyuma.

Mbowe ahitaji tena kufanya mambo haya, kwa kuwa nchi nzima inajua ana dhamira ya kuwa Mwenyekiti wa Chadema hadi atakapofia kwenye kiti, haijalishi ni mwaka gani itakuwa.

Jana usiku Mbowe alikuwa na kikao kirefu na waandishi wanne wa habari, wa Global TV, Mwananchi, ITV na Radio One (mmoja bado sijajua wa chombo gani).

Kikao cha kugawana majukumu ya kualika wanahabari kwa siri, ambapo Hussen wa Global TV alipewa kazi ya kualika kwa siri waandishi wa Online TV's, kuwa waandishi wafike kwa Mbowe leo saa nne asubuhi.

Wengine wakipewa jukumu la kualika wanahabari wa radio, vituo vya TV na magazeti. Sasa yote haya ni ya nini? Hakuna jipya kwenye suala la Mbowe kugombea uenyekiti Chadema wala kuwa Mwenyekiti

Haikuhitaji mbinu hizi za kale za siasa za mapenzi ya uongo-uongo ya wananchi kwa mwanasiasa.

Ova
 

Attachments

  • IMG_20241218_144717.jpg
    192.8 KB · Views: 2
Kweli ni mwamba, aliwapiga chenga Polisi kwenda kwenye maandamano lakini wanachama wake wamemkuta bila taarifa. Safi sana!
 
Inaonekana hicho Chama hakina nia ya mabadiriko ya kweli, kina kuwa ni mali ya mtu binafsi sio tena Taasisi

Sijaona utofauti wake na CCM hadi sasa
 
Mtu anaeweza kuleta mabadiliko chanya CDM ni John Heche, siyo Lissu.

Lissu aungane na akina Kibatala kusaidia chama kisheria.
 
Kama kweli Mbowe anataka kulinda heshima yake na ushawishi angeachana na habari za kuendelea kuwa mwenyekiti wa hicho chama.


Ikiwa Tundulissu atakubali kumuachia Mbowe uenyekiti wa Chadema kutakuwa hakuna sababu yeye kuendelea Kuwa Chadema.


Machaguo ni mawili kukiua chama Kwa kumrudisha Mbowe au kumpatia Lissu hiyo nafasi ya uenyekiti.

Sioni sababu zozote za Muhimu za Mbowe kuendelea kuwa Mwenyekiti.
 
hao ni ccm siyo chadema maana ccm ndiyo wanataka mbowe agombee uenyekiti wanamuogopa LISSU
 
Mtu anaeweza kuleta mabadiliko chanya CDM ni John Heche, siyo Lissu.

Lissu aungane na akina Kibatala kusaidia chama kisheria.
Heche pamoja na kusoma Mlimani bado mshamba mshamba

Chadema ni chama Cha swaga πŸ˜„πŸ˜„
 
Hapo ndio utajua yupo upande gani.
Maana hiyo ndio aina ya michakato upande ulee!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…