Wafuasi wa Askofu Mwaikali wasusa ibada Mbeya

Wafuasi wa Askofu Mwaikali wasusa ibada Mbeya

Hili kanisa lijipange vizuri namna ya kuendesha mambo yake.Kila mara linakuwa na migogoro hadi unashindwa kuamini kama kweli linafanya kazi ya mungu.
Tatizo wanyakyusa wana EGO sana mbona huku mikoa mengine, kanisa liko shwari
 
Hao wananchi wanaomfuata huyo Mwaikali walifuata nini huko kanisani ambapo huyo Mwaikali hayupo?

Si wangeenda kwenye hilo kanisa alipohamia? Wawaache wengine wasali kwa amani?
Dawa yao mabomu ya machozi tu mbuzi hao
 
KKKT imejaa maaskofu wajuaji.

Tatizo ni kutokuwa na mfumo mmoja makini wa usimamizi (strong centralised administration). Kila dayosisi ina utawala wake na katiba yake.

Askofu mkuu ni wadhfa wa heshima tu unaotolewa kwa mzunguko (rotational basis). Hivyo kila askofu wa dayosisi ni mfalme katika eneo lake. Na kama kawaida hawa “watumishi” karibu wote ni watu wenye makuu wasiokuwa na kiasi. Bila udhibiti wanaweza kushangaza sana.
 
Kanisa ni moja tu takatifu la mitume, msihangaike enyi waamini enendeni kataka kanisa linalofuata misingi na mafundisho yaliyoachwa na Kristo mwenyewe.

Waprotestanti msinipofoe jama [emoji2][emoji2].
Huyo yesu aliacha mitume ipi? Na kama aliacha mitume basi haihusiani na ukatoric, maana ktk biblia hakuna sehem yeyote inayotoa ufafanuzi wa kanisa kama dhehebu/dini bali kanisa/hekaru ni mtu mwenyewe.

Anyway amka ktk ujinga hilo kanisa unalosifia liliuwa babu zako na wajomba zako kuwabaka adharani, ni vile viongozi wenu wa dini hawatak kuwaeleza ukweli ili msije mkakimbia wakose sadaka za kuendesha uchumi wa vatican na freemason kiujumla.
 
Kanisa ni moja katoliki takatifu la mitume.
Hii ni kampuni mkuu na si kanisa na ndio maana huendeshwa kidikteta kutoka Roma ,eti askofu au upadrisho lazima atoe Papa kule Roma wakati wala hata anayempa uaskofu na hata waumini wake hawajui
 
Kanisa ni moja katoliki takatifu la mitume.
Wewe. Katoliki ishabadilishwa na kuchanganywa na siasa na kuacha kabisa Yale Mungu anataka. Soma vizuri vitabu vya Ufunuo na Daniel.
 
Huyo yesu aliacha mitume ipi? Na kama aliacha mitume basi haihusiani na ukatoric, maana ktk biblia hakuna sehem yeyote inayotoa ufafanuzi wa kanisa kama dhehebu/dini bali kanisa/hekaru ni mtu mwenyewe.

Anyway amka ktk ujinga hilo kanisa unalosifia liliuwa babu zako na wajomba zako kuwabaka adharani, ni vile viongozi wenu wa dini hawatak kuwaeleza ukweli ili msije mkakimbia wakose sadaka za kuendesha uchumi wa vatican na freemason kiujumla.
Sina babu wala mjomba alieuwa na hili kanisa pendwa duniani.

Sio ujinga hili ndilo kanisa lisilo na mawaaa.

Na sijasema Yesu aliacha kanisa , bali nimesema kanisa linafuata mafundisho ya Yesu mwenyewe.
 
Ndio maana inaniwia vigumu kuenda kanisani siku hizi.

Mchungaji anafundisha waumini Amani, upendo na kisamehe,

Cha kushangaza wao kwa wao hawamtaki kusameheana mpaka kufikia kufukuzana

Ikifika jpili Mimi na familia yangu tunakusanyika na kusali nyumbani tu.
 
View attachment 2265568
Mbeya. Baadhi ya waamini wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Konde usharika wa Ruanda, wanaomuunga mkono Askofu Edward Mwaikali aliyeondolewa katika kanisa hilo, wamesusia ibada kwa kile kinachoendelea juu ya mgogoro katika kanisa hilo.

Hatua hiyo imekuja baada ya Askofu Mwaikali ambaye sasa ametangaza kuhamia Kanisa la Kilutheri la Afrika Mashariki (KKAM), kukabidhi baadhi ya mali za kanisa hilo.

Katika ibada ya leo Jumapili Juni 19, kanisani hapo iliendeshwa na Askofu mstaafu, Dk Israel Peter Mwakyolile ambaye amesisitiza kutubu akisema kuwa wachungaji wametenda dhambi kubwa na waathirika ni waamini ambao hawana hatia.

"Mungu atusamehe sana, Dk Mwaikali na sisi wengine, wachungaji wametenda dhambi kubwa badala ya kutengeneza wamebomoa kwani tumepoteza watu wengi tunaporudi nyumbani tutafakari upya," amesema Dk Mwakyolile ambaye ametokwa na chozi wakati akizungumza madhabauni.

Mwananchi ambayo ilikuwa kanisani hapo, imeshuhudia makundi ya waamini wakiwa baadhi wamekaa kwenye viti nje ya kanisa wengine wakiwa wamesimama kwa makundi makundi wakionekana kupanga mipango yao.

Pia kama haitoshi, wapo ambao walifika kanisani hapo lakini ni kama hawakuelewa mwenendo na kuamua kuondoka kabla ya ibada kumalizika.

Source:mwananchi digital
upuuzi mtupu jinga hao nani kawambia imani ipo ktk kumfata mtu au hekalu?Makanisa mengi yanamwongozo wa utatuzi wa migogoro ndani ya taratibu za kanisa.Ujuha tu.
 
Mitume ndio hao wakina saints nani sjui mizungu mitupu? Babu zenu maelfu waliuwawa sababu ya hilo genge unaloliita la mitume

Wake up , kanisa ni wew mwenyew wala sio dhehebu au genge la dini, someni biblia vizuri enyi wavivu wa kufikiri
Kwamba hauwafahamu mitume 12 wa Yesu? Watakatifu wanahusikaje? Wapo watakatifu wengi tu kina Mt Kizito Mt Bakhita Mt Karoli Lwanga n.k au unamaanisha nini?
 
Huyo yesu aliacha mitume ipi? Na kama aliacha mitume basi haihusiani na ukatoric, maana ktk biblia hakuna sehem yeyote inayotoa ufafanuzi wa kanisa kama dhehebu/dini bali kanisa/hekaru ni mtu mwenyewe.

Anyway amka ktk ujinga hilo kanisa unalosifia liliuwa babu zako na wajomba zako kuwabaka adharani, ni vile viongozi wenu wa dini hawatak kuwaeleza ukweli ili msije mkakimbia wakose sadaka za kuendesha uchumi wa vatican na freemason kiujumla.
Nadhani akili yako haiko sawa
 
Hii ni kampuni mkuu na si kanisa na ndio maana huendeshwa kidikteta kutoka Roma ,eti askofu au upadrisho lazima atoe Papa kule Roma wakati wala hata anayempa uaskofu na hata waumini wake hawajui
Kanisa ni moja takatifu Katoliki la Mitume.

"Nami nakuambia wewe ndiye Petro na juu ya Mwamba huu nitalijenga kanisa langu milango ya kuzimu italijaribu lakini haitashinda nami nimekupa mamlaka na funguo lolote utakalolifunga duniani na mbinguni limefungiwa na lolote utakalofungua duniani mbinguni limefunguliwa"

Unaposema udikteta kwa hiyo Yesu alikuwa dikteta kuchagua mitume 12 mwenyewe bila kishirikisha wafuasi? Usiwe MJINGA.Mamlaka ya Askofu au Askofu mkuu hayatoki kwa mwanadamu bali kwa yule aliyempa funguo.Lazima aheshimiwe! Usilete demokrasia za wanadamu kwa Mungu!
 
Back
Top Bottom