Wafuasi wa Askofu Mwaikali wasusa ibada Mbeya

Wafuasi wa Askofu Mwaikali wasusa ibada Mbeya

Nyinyi KKT maaskofu wenu na viongozi wengine wa kiroho wasiwe wanaoa.

Askofu anafamilia na amepanga kusomesha watoto wake ulaya na kumnunulia mama watoto gari ya pili nyinyi mnamfukuza. Ni ngumu kukubali sababu hapo anaiwazia familia na pengine anashawishiwa na mama watoto kutokubali kufukuzwa ili aendelee kuitwa mama askofu.

Ni mtazamo tu lakini, Oneni kwa wenzenu Roman Catholic ni amani tu.
Ila una hoja nzuri Kuna haja wasioe ili wasiwaze mali muda wote kam magar na kusomesha ulaya na kuishi kitajiri hapana Roman Catholic mmeona mbali kwa hili

Kkkt Kuna migogoro Sana tokea nazaliwa hata kanisan kwetu kipindi Cha 1995 walizichapa hadharani
 
View attachment 2265568
Mbeya. Baadhi ya waamini wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Konde usharika wa Ruanda, wanaomuunga mkono Askofu Edward Mwaikali aliyeondolewa katika kanisa hilo, wamesusia ibada kwa kile kinachoendelea juu ya mgogoro katika kanisa hilo.

Hatua hiyo imekuja baada ya Askofu Mwaikali ambaye sasa ametangaza kuhamia Kanisa la Kilutheri la Afrika Mashariki (KKAM), kukabidhi baadhi ya mali za kanisa hilo.

Katika ibada ya leo Jumapili Juni 19, kanisani hapo iliendeshwa na Askofu mstaafu, Dk Israel Peter Mwakyolile ambaye amesisitiza kutubu akisema kuwa wachungaji wametenda dhambi kubwa na waathirika ni waamini ambao hawana hatia.

"Mungu atusamehe sana, Dk Mwaikali na sisi wengine, wachungaji wametenda dhambi kubwa badala ya kutengeneza wamebomoa kwani tumepoteza watu wengi tunaporudi nyumbani tutafakari upya," amesema Dk Mwakyolile ambaye ametokwa na chozi wakati akizungumza madhabauni.

Mwananchi ambayo ilikuwa kanisani hapo, imeshuhudia makundi ya waamini wakiwa baadhi wamekaa kwenye viti nje ya kanisa wengine wakiwa wamesimama kwa makundi makundi wakionekana kupanga mipango yao.

Pia kama haitoshi, wapo ambao walifika kanisani hapo lakini ni kama hawakuelewa mwenendo na kuamua kuondoka kabla ya ibada kumalizika.

Source:mwananchi digital
Mwandishi Wa Mwananchi katika mgogoro huu yeye amekoa akichichea na kuuukuza mgogoro ....Waumini wanatokea majumbani kwao kuja kanisani.. kama Kanisa lilijaa mwandishi amerimia live so gani kusema Waumini wamesusia ibada?

Sent from my SM-J700F using JamiiForums mobile app
 
Itakuwa hvyo waaandishi wameongeza chumvi
 
Hili kanisa lijipange vizuri namna ya kuendesha mambo yake.Kila mara linakuwa na migogoro hadi unashindwa kuamini kama kweli linafanya kazi ya mungu.
Tangulini makanisa yanafanya kazi ya Mungu hao ni wafanya biashara
 
Mitume ndio hao wakina saints nani sjui mizungu mitupu? Babu zenu maelfu waliuwawa sababu ya hilo genge unaloliita la mitume

Wake up , kanisa ni wew mwenyew wala sio dhehebu au genge la dini, someni biblia vizuri enyi wavivu wa kufikiri
Unajichanganya. Unawalaamu wazungu, halafu hapo hapo unaikubali Biblia waliyoileta hao hao wazungu. Hujui unataka nini!
 
Mwandishi Wa Mwananchi katika mgogoro huu yeye amekoa akichichea na kuuukuza mgogoro ....Waumini wanatokea majumbani kwao kuja kanisani.. kama Kanisa lilijaa mwandishi amerimia live so gani kusema Waumini wamesusia ibada?

Sent from my SM-J700F using JamiiForums mobile app
Wewe ulikuwepo?
Muandish ameripoti kilichojiri ww unalwta hisia binafsi..
 
Bibi hawa wachunguji wa KKKT wanamhubiri Mungu gani? Poleni waumini maana mnachungwa na mashetani.Acheni kutoa sadaka muone hao wachungaji wenu watagombea nini
 
Back
Top Bottom