Wafugaji wa mbwa kibiashara au ulinzi tukutane hapa

Anaweza kuwa nini sasa! Maana nilitarajie useme na mbwa wa jamii gani?
mkuu huyu Tundapori anafahamu sana aina ya mbwa, amenifundisha mengi sana kuhusu mbwa, tulikutana kwenye uzi flani miaka ya nyuma
 
mkuu nitajaribu kuulizia, kuna mfugaji flani alikuwa nao wakubwa mno, bahati mbaya alifariki na mradi kuyumba
Ndiyo natafuta Malinois wazuri na wakubwa.
 
mkuu nitajaribu kuulizia, kuna mfugaji flani alikuwa nao wakubwa mno, bahati mbaya alifariki na mradi kuyumba
Belgian shepherds sio wakubwa kiivo, wana umbo dogo hata kuliko GSD, natafakari hapo uliposema "wakubwa mno".
 
Belgian shepherds sio wakubwa kiivo, wana umbo dogo hata kuliko GSD, natafakari hapo uliposema "wakubwa mno".

Uko right kabisa mkuu ila Belgian Malinois (BM) wanavumilia mikikimikiki na dhoruba.

Hawachoki kama GSD.

Tofauti kubwa ya BM na GSD ni umbile zaidi. Na kwa familia yenye watoto GSD wanafaa zaidi kuliko BM.

BM wanapenda kupigishwa mazoezi na mituringa mikali na ukifunga BM uwe mtu very active kwa mazoezi. Wasipopata mazoezi makali wanakuwa vichaa kabisa.
 
ahaa kumbe!
mkuu unaweza kutoa somo jinsi unayvoandaa msosi wao na ratiba ya matibabu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…