Wafugaji wa mbwa kibiashara au ulinzi tukutane hapa

Jambo la msingi hakikisha hawachangamani kwa ajili ya kutunza uzao usichanganyike
 
Diiii umetisha mzee
 
vip kuhusu jamii hii ya mbwa Boerboel wenye asili ya Africa kusini?
Haya gharama lakini yana hasara, ysnakula na hayazalishi kipato chochote, huu uzi unahusu UFUGAJI WA MBWA KIBIASHARA
 
Lee hii thread ulishawahi kuiona inakuhusu na ma mbwa wako
 

Aisee, siyo kitu kizuri lakini.

Kuwa na aina tofauti tofauti za mbwa siyo vizuri sana.

Changamoto inakuwa katika swala la kupandana.
Utatakiwe uwe makini sana majike yanapokuwa kwenye ‘Heat’.
Ili jike la GS mfano lisije likapandwa na dume la Rottweiller nakadhalika nakadhalika.
Ukifanya hiyo cross-breedings utakuwa unapata watoto wa mbwa wenye sura za ajabu ajabu mno.

Wewe fikiria mfano upandishe kati ya Boreboel na German Shepherd.
Je, puppies watakuwa na sura gani??!! Na nakuhakikisha kila mnunuzi wa mbwa atakuwa anakukimbia.

Ushauri: Fuga aina moja tu ya breed. Usichanganye breed nyingi katika eneo moja la kufugia.

Ukiamua kufuga zaidi ya breed moja kwenye eneo moja ina bidi ugeuke kuwa Watchman majike yanapoingia kwenye heat. Hii inaitwa kupiga chabo.
Matokeo yake utajikuta unakuwa unanuka harufu kama ya kiwonder cha Tanuru dogo la mikate.

Ila kama utakuwa na huo uwezo wa kusimamia, unaweza kufuga hizo breeds tofauti tofauti. Ila nikujipatia pressure tu bila sababu ya msingi.

Tafuta breed moja tu unayoipenda sana katika moyo wako ufuge.

Na ukweli ni kwamba hata ukiwa nao wengi wa aina moja, wakati wa kupandana inafaa uruhusu wazazi wenye ubora ndo wapandane ili angalau uweze kupata puppies wenye ubora mkubwa na mzuri.
 
Ushari mzuri sana
 
hao mbwa walipigwa marufu nchi nyingi ninavyosikiaga, ni hatari sana.
Kuhusu kufuga koko ni hasara sana kwani huwezi hata kuuza akizaa.
Mimi nilianza kwa kufuga koko nikahamia German na belgian shephard sijawahi kujuta
Unapatikana wapi mkuu nikitaka German
 
Ukiepeleka polisi hawawezi kukufundishia mbwa wako? Hakuna manual ya jinsi ya kunfundisha mmbwa unavotaka??
 
Mi nadhani familia nzima inapaswa kizoeana na mbwa maana bila hivyo huyo aliyezoena naye asipokuwepo itakuwa shida sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…