Nilichogundua mbwa ni passion bila hivyo huwezi . My dog ukitaka ugomvi mkubwa na mimi mpige au mfokee nikuone . Bado mdogo ana six months now nasubiri afike 8 nimpeleke training, ninempata toka kwa mtu ambae ana gsd wawili ajabu huyu katoka golden gsd but nampenda thats why nimemuita DAZZLER.
Nilikua nampa maziwa ya ng'ombe leo nimepata jibu why alikua anaumwa sana maana ilifika kipindi mpaka kula nilikua namlisha kwa kijiko huku akiendelea na dozi, ila nilipoacha kumpa mazima na dozi ilipoisha amerecover sana kumbe ni cases za minyoo dah, alikua akiharisha na kutapika kapigwa dawa za minyoo plus za magonjwa mengine Dr wake anajua zaidi, ana card la matibabu hivyo trend yote naifuatisha.
Mazoezi kila siku 3 za kwenye wiki nafanya nae walking ya km 2 mpaka 3 pia usiku kila siku yuko loose kuzunguka ndani ya nyumba.
Mbwa ana raha yake sana, gsd anacheza na watoto safi tu . Hakika kwa mm nikikuta mtu anapiga mbwa roho inaniuma sana , hata barabarani naepuka sana kugonga mbwa sana sana sana .
Chakula nampa champdog asubuh then jioni anakula nyama nampikia na unga wa dona(namix) . Nyama hizi nimeweka order buchani huwa wanauza zile chenga wakikata na mashine wana ongeza na mafuta plus utumbo pia na stake chache bei chee sana ni tsh elf 2 tu kwa kg. Kama kuna maboresho zaidi naomba mnijuze , namtunza tu kwa kulinda familia basi sitaki hata kuzalisha na kuuza , nimemuweka na mwenzie wa kiswahili ili asiboreke
Few years from now you may wish you should have started today...