Wafugaji wa mbwa kibiashara au ulinzi tukutane hapa

Wafugaji wa mbwa kibiashara au ulinzi tukutane hapa

Nina German shepherd wangu nyama huwa naenda Machinjoni kuwachukulia ,hawali kitu kingine zaidi ya nyama na maziwa

Ofcoz nikila ganja zangu nao huwa wanavuta ,kila jumapili nawatia Red wine glass basi burudani kabisa.

Napenda mbwa sana kiasi kwamba wananipa faraja
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
 
Mpendwa mwana JF, unaweza kushangaa kusikia kuwa mbwa ni biashara nzuri kupita hata kufuga ng'ombe kibiashara na ukashangaa.

Uzi huu utakuwa ni maalum katika kupeana uzoefu katika biashara hii ya kufuga mbwa kwa lengo la kujipatia kipato na ulinzi pia.

Tutajifunza aina bora na inayohimili mazingira yetu hasa Tanzania na Afrika mashariki kwa ujumla.

Hivyo mdau ikiwa wewe ni mfugaji wa wanyama hawa kibiashara, nakukaribisha sana utupatie uzoefu juu ya aina mbali mbali mfano;

a) German shephard
b) Belgian shephard
c) Bull dog
d) Rottweiler
e) Ridge back nk

mambo muhimu ya kupeana uzoefu;
1) banda/ nyumba bora ya kufugia
2) chanjo
3) Masoko nk

View attachment 916841View attachment 916842View attachment 916844



Ni nakukaribisha utupe uzoefu wako na kwa wale wanaotamani kujifunza mnakaribishwa kwa maswali na wadau watakujibu


Maelezo ya German Shepherd hapa

Maelezo ya Belgian Shepherd hapa


🙏🙏
Napenda sana kujifunza na kujua mengi kuhusu huyu mnyama 'mbwa'.
 
Ngoja niwape kisa kilimtokea family friend mmoja mwaka 2015 msimu wa xmass na mwaka mpya.

Jamaa alikuwa na GS wako nane. Kawaida huwapa msosi kila siku usiku mida ya saa 4 baada ya watu wote kuingia ndani maana ni wakali mno. Na zoezi la chakula kuna shamba boy huwa ndie anawahudumia mbwa.

Sasa shamba boy xmass alienda kwao kula sikukuu. Na family friend yeye ni mtu wa tungi sana huwa anakesha baa na wajomba zangu.

Siku shamba boy alipoondoka jamaa akawa amelewa zake akarudi home akapitiwa akalala (mbwa hawakupewa chakula kama kawaida).

Akaamka asubuhi akaandaa msosi vizuri akafungulia banda la kwanza. (Amewagawa katika mabanda mawili wanne wanne).

Baada ya kufungua banda la kwanza mbwa mmoja akaanza kumkoromea kwa hasira sana kisha akamrudia, wale wengine watatu nao wakamrukia wakaanza kumrarua kwa hasira, wale wengine ndani nao wakapandwa na wazimu mpaka wakavunja banda wakaungana na wenzao.

Mke wa jamaa ni mayowe tu kwa dirishani anashuhudia mumuwe anavyotafunwa bila kuwa na lakufanya. Watoto vilio mpaka majirani wakasogea karibu.

Bahati nzuri kuna mtoto wa jirani ni rafiki wa shamba boy na mara nyingi wakiwa wanalisha mbwa wanakuwa wote hivyo wale mbwa wamemzoea sana.

Basi dogo ndio kuingia pale akawatuliza mbwa na jamaa kukimbizwa hospital ambapo alilazwa miezi mitatu akiwa hana fahamu.

Kusema ukweli yule jamaa kama angekuwa kapuku wala asingepona kwa shambulio lile. Pesa ilimuokoa.

Baada ya kurudi uraiani alikuwa amefungwa POP miguuni wala kutembea bila magongo hawezi. Aliwatandika risasi mbwa wote na mpaka sasa sijui kama anafuga tena.

Mbwa ni Loyal Friend kuliko hata binadamu lakini ni hatari sana pia.

Wafugaji tuzingatie Terms and Conditions

[emoji190] [emoji240]
Pole sana kwake aisee
 
Glad nimeuona huu uzi.
Recently nimeanza kufuga mbwa aina ya German shepherd (week ya 3 sasa) ana miezi nane lakini nina changamoto kadhaa.
1. Huyu mbwa alikua anafugwa yard so walikua wengi mno.
2. Baada ya kumchukua namuona muoga sana na hataki kutii amri (nina week naye mbili au tatu).
3. Sheria za kumlisha na aina za chakula sijui mwanzo nilimnunulia unga flani kama wa ulezi upo kwenye mifuko special nikaja nikamnunulia kama vikaranga ila naona hanenepi. Nampa chakula mara moja kwa siku na maji muda wote. Pia kuna muda narudi katafuna vyombo ashakunja mpaka sufuria. Kala madumu yani vurugu mechi ndani.
4. Anatoa mlio kama wa dubwi au mbwa mwitu habweki ile kukaza.
5. Anaogopa watu.
6. Kutembea mpaka nimburuze au kumpa kipondo.

Sasa wadau nishaurini jinsi ya kumlea huyu jamaa.
1. Chakula.
2. Namna ya kutii amri.
3. Kuwa mkali.
4. Matunzo yake mazuri.

Kuhusu kumpeleka training kwa sasa siwezi ukitegemea starehe za december na kipigo cha january siwezi peleka dog shule nikaacha dogo. Au kama kuna sehemu gharama nafuu nijulishwe for future use.
Usimpige, mfundishe, mtembeze polepole akikataa acha umtembeze cku nyingine, mpe chakula kingi mara mbili kwa cku, mpe dawa za minyoo muoshe
 
Cha kukuongezea tu

Gs asilimia almost 70 % sio pure breed hapa bongo ndo maana unakuta zinauzwa hadi 200,000 ,kwa GS pure inaanzia milion hadi na nusu ya miezi 2 ,ila angalizo nyingi tulizonazo sio pure ilikuijua iliyopure vigezo ni hivi
1.urefu wa miguu ya mbele ni mirefu kuliko ya nyuma,na urefu ni 22-26 chini hadi bega (akiwa na zaidi ya mwaka)
View attachment 916875
2.masikio yake huwa ni makubwa yaliyosimama wima
View attachment 916876
3.Mkia wa pure breed huwa ni wenye manyoya mengi sana
View attachment 916877

4 ,kUNA AINA ZA MBWA KARIBU 200 ila DNA Hudhihilisha kama iko pure au imechanganyia ,hii ni ghali ndo maana inaepukwa ,

HITIMISHO

Breed nyingi kwa bongo zimechakachuliwa hivyo ukiamua kufuata wazohili zuri la biashara jiongeze sana kushauriwa alienishauri aliniuzia GS kwa 200,000 nimemuhoji ndo kaniambia ukweli kuwa yangu sio pure breed akaniambia niangalie masikio yamelala sana akaniambia ingekuwa pure hata laki 9 sichukui.Aidha gs akikua anauzwa hadi 8000 usd ,wazungu wa migodini ndo wateja wakishamuona na vigezo vyote unakulamzigo ilani aghali sana pia kuwalea
We ndo hujui, hao wenye miguu mifupi nyuma ni American show line, wengi wa apa bongo ni working class by au European working class, haw show line wana matatizo mengi na wanaanza kukatazwa kubreed maana ni wagonjwa wagonjwa wa miguu
 
Hawa ni show line, hawa GSD ni wagonjwa mno na ukinunua unaweza jutia, wengi Og uku ni European show line, fatilia tofaut ya working line GSD na show line GSD
Working line GSD ni sable mkuu
 
Working line GSD ni sable mkuu
We jamaa hujui ata mbwa, ingia google, sikuiz mambo ni rahis
Ila kifupi kuna showline GSD na working line GSD, hizo nyingine ni rangi tu
 
Kwakweli wanaumiza sana watu,halafu wanaluga tamu sana.[emoji23][emoji23][emoji23]
Nimwokota hawa mbwa wawili jee niwapatie chakula gani ili wakue kwa alaka alafu nifanye nini ili wawe wakali pia waweze kuelewa nicho itaji kuwa fundisha? Nimbwa wa kibongo tuu wakawaida

20210810_074907.jpg
 
Mi nafunga mbwa wa kiswahili na wako vzr Sana,kiulinzi ata adabu pia.nawapa huduma zote stahiki ikiwa chakula,chanjo zote,na kuoga kira jpili.kiukweli ulinzi tosha..
Mimi niliokota mbwa wawili dume ja jike sasanaitaji niwafuge bado wadogo wana kama miez miwili nasehe kwa kuwaona jee niwapatie chakula gani waweze kukua kwa uzur na afya njema pia wawe wakali na jinsi ya kuwafunza adabu
 
Nimwokota hawa mbwa wawili jee niwapatie chakula gani ili wakue kwa alaka alafu nifanye nini ili wawe wakali pia waweze kuelewa nicho itaji kuwa fundisha? Nimbwa wa kibongo tuu wakawaida

View attachment 1886841
Kwanza anza na chanjo. Tafuta daktari wa mifugo awafungulie kadi yao ya clinic (angalia picha) awape chanjo waepukane na magonjwa. Wanaanza na DHCP, Then vitamini na minyoo na mwisho wapate kichaa cha mbwa.... Hizi zitakuwa zinajirudia kutokana na wakati....

Chakula...
Wapikie uji wa unga wa dona na kama utapata dagaa au nyama umpatie (Vyote hivi unapata kwa bei rahisi kuna bei za vyakula vya mbwa).
Kwa ukuaji wa haraka kuna supplements madukani kwa ajili ya mbwa kanunue uwape.

Ukali
Kwanza wafungie wasizoeane na kila mtu. Wasiwe wazururaji.

Mafunzo.

Kuna wataalam wa mbwa kwa ajili ya mafunzo ila kama hutamudu gharama just google basic training for dogs uwafundishe mwenyewe.

JPEG_20210810_102311_3761757511270344243.jpg
 
Asante sana kaka nashukuru kwa ushauriko ila mimi ninaishi kijijini madctor wa mbwa huku hakn ad mjini
 
Asante sana kaka nashukuru kwa ushauriko ila mimi ninaishi kijijini madctor wa mbwa huku hakn ad mjini
Vijijini hamna mifugo maana anayemtibu ng'ombe ndio anatibu mbwa pia unaweza kwenda maduka ya mifugo ukasaidiwa.

Otherwise fuga kienyeji tu ila usimuachie kuzurura hovyo aepukane na magonjwa na minyoo...
 
Vijijini hamna mifugo maana anayemtibu ng'ombe ndio anatibu mbwa pia unaweza kwenda maduka ya mifugo ukasaidiwa.

Otherwise fuga kienyeji tu ila usimuachie kuzurura hovyo aepukane na magonjwa na minyoo...
Kaka huyu mbwaa anaogpa wala hata hawabwekei wakijabtatzo bado mdogo ama shida nn nahitaji awe anabwekew watu wanapo kuja kumuona maana nimemfungua

20210812_134214.jpg
 
Back
Top Bottom