Fahamu pia kuhusu German shepherd wa asili ya kitanzania: Kuna Tanzanian Local line ya German shepherd!!! Hawa ni wazuri sana pia kwa ulinzi. Wana miili midogo kiasi, na wana manyoa mafupi. Ila hata hawa local type wana masikio yaliyosimama wanayoweza kuyachezesha. Kwa kigezo cha masikio huwezi kuwatofautisha na German shepherd wa kizungu. Midomo yao ni mifupi, lakini ni wakali balaa!!! Kwa wanyamwezi mbwa hawa huitwa mbwa wa KIPUGE!! Tatizo lao ni kwamba ni vigumu kuwafundisha hata wakawa na nidhamu ya hali ya juu. Kwa mfano ukimpa nyama huwezi ukamnyang'anya!, atakuuma hata kama wewe ndo bwana wake!! Ukishika mtoto wake halafu huyo mtoto akalia uhesabu maumivu!! Ni vigumu kumfahamisha mipaka ya nyumba anayohitajiwa kufanya ulinzi. Kwa hiyo akimfukuza mtu atamfuata hata akitoka kwenye eneo la nyumbani. Akianza kumshambulia mtu ni vigumu kumzuia!! Tofauti kabisa na German shepherd aliyefundishwa, anashambulia kwa amri, ni mtiifu sana kwa bwana wake, kwa vyovyote vile hawezi kabisa kumshambulia bwana wake!!