@steven nguma hao wako naona ni cross breed ya gs
Unawaonaje? Tatizo lako wewe umekariri rangi fulani tu!! Ukweli ni kwamba huwezi kumtambua pure GS kwa UHAKIKA kuwa CROSS breed, vinginevyo utuambie kuwa macho yako yanaweza kuviona vinasaba(genes).Kijijini kwetu waarabu walihamia miaka mingi iliyoita na wakfanya cross na waafrika. Baadhi ya hizi cross wengine kwa macho wanaonekana kuwa ni pure waarabu (lakini ni cross) na wengine wanaonekana kwa macho kama pure waafrika (lakini ni cross), na wengine wanaonekana kwa macho kuwa ni mchanganyiko wa mwarabu na mwafrika (tunawaita MASHOMBE)!!
Sasa huyu cross wa kiarabu anayeonekana kwa macho kama pure mwarabu, akioana na pure mwarabu, au cross mwarabu anayeonekana mwarabu kwa macho, watakapopata watoto ndo siri inaweza kufumuka kwa kuangalia watoto wao!! baadhi ya watoto watatokea kuwa ni mchanganyiko(cross!), tunawaita "MASHOMBE", wengine wataonekana waafrika kabisa na wengine wataonekana ni waarabu kabisa!.
Hali kadhalika kwa mbwa!! Ndiyo maana kama unatafuta mbwa wa ulinzi, unaweza kuchukua yeyote hata kama ni cross maana mwonekano wake na sifa zake zilizo nyingi zinafanana kabisa na za Pure GS. Tatizo linakuja kama unatafuta mbwa ili uzalishe kwa ajili ya biashara!! Kama mbwa alikuwa ni cross, baadhi ya watoto wake watadhihirisha kabisa kuwa siyo pure breed ya GS, na hapo utapata hasara! Kama unatafuta kwa ajili ya kuzalisha ni vizuri ukajiridhisha kuhusu wazazi wa mbwa huyo angalau vizazi viwili nyuma!! Wafugaji wazuri huwa wanatunza historia ya mbwa kwenye kadi!! NARUDIA: Cross anaweza kufanana na pure kimwonekano asilimia mia moja, (Phenotypically similar, but genotypically different!), na huwezi kumtambua kwa macho, itabidi usubiri hadi uje uone uzao wake!! Mtu akidai kuwa atamtambua huyo ni mwongo na hana uelewa hata kidogo tu wa GENETICS!!
Mfano mwingine: Kuna mtu anaweza kuwa ni cross wa albino lakini huwezi kumtambua kwa macho!! Hana hata dalili kidogo za kuonekana kwa macho kuwa ni cross wa albino!! Huyu mtu akioana na mtu mwingine ambaye pia ni cross wa albino (naye huwezi kumtambua kwa macho), watoto wao baadhi watakuwa ni pure albino na hapo ndipo utakapojua kuwa kumbe wazazi walikuwa ni cross ya albino!!
Genetics ya watu inafanana na ile ya mbwa!! Mtu akidai anaweza kumtambua kila cross wa GS kwa macho tu, maana yake anauwezo wa kuviona vinasaba(genes) kwa macho!! Huo ni utapeli!!