Wafungwa maisha kwa ukatili wa mtoto kwenye school bus

Wafungwa maisha kwa ukatili wa mtoto kwenye school bus

Vizuri sana.

Hawa watoto wanaosoma hizi day schools usalama wao bado ni mdogo.

Wazazi tuache uzungu mwingi, tuwafundishe watoto kujilinda na mashambulio.
Wenzetu nchi zao miundombinu yao iko vizuri, magari yao yana camera, wanajari muda nk.

Sisi huku tuwafundishe watoto wetu kipi chema na kipi kibaya, kipi afanye na kipi asifanye.
Wapi asiguswe nk tusiwaamini sana watu nje ya sisi wazazi .
 
Mimi nadhani serikali ingejikita sasa kwenye kuzisimamia hizo sheria ndogo ilizowawekea hao wamiliki wa shule za mchepuo wa Kiingereza.

Kwa mfano hiyo ya magari yote ya shule kuwa na matrons!

Halafu na muda wa kwenda shule nao usogezwe mbele walau mpaka saa mbili hivi asubuhi, na muda wa kutoka uwe saa nane mchana.
Haya mambo ya kuwakurupusha watoto wadogo saa 10 alfajiri, na kuwarudisha nyumbani saa 12 jioni, na wenyewe haujakaa sawa.

Lakini pia zile shule zinazowahifadhi watoto wadogo zikaguliwe mara kwa mara ili kuangalia kama zinakidhi vigezo vya kuwahifadhi hao watoto.
 
Mnawafungaje KENGE kama hao, wakateni DHAKARI zao, wabakishie pakukojolea tu, haribuni KENDE zao kwa nyundo kisha waachieni waishi mtaani.
 
Kuhusu kesi ya dereva na konda wa school bus kumkatili mtoto wa miaka 6, aliyekuwa mwanafunzi wa shule ya star light pre and nursery school, Kinondoni, Dar es Salaam, watuhumiwa wote 2 walitiwa hatiani na walifungwa maisha kwa hukumu ya tarehe 22 mei, 2024.

Kuhusu tikio hili soma: Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni aingilia taarifa za Madereva wa School Bus kudaiwa kunajisi Watoto

Habari zaidi utazipata 'in the resident magistrates court of Kivukoni, at kinondoni' case no. 392 of 2022 between republic versus washtakiwa hao wawili.

View attachment 3029110
KUMBUKIZI YA PICHA MWAKA 2022: Nikiwa nimesimama na Mhe. Gondwe, aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, tulipotembelea shule husika kufuatilia tukio hili.

WITO: Wazazi na Walezi tuendelee kuwa karibu na watoto siku zote. Mtoto ukiona anakataa kwenda shuleni ujiulize mara kadhaa na useme naye, akitoka shule sema naye kirafiki, kagua nguo zake, muogeshe, imba naye don't touch, muulize nani kamshika wapi na kampa zawadi gani ... kuwa karibu naye

Aidha, mkienda visiting days vunjeni ukimya ongeeni na watoto kuhusu ukatili wa kijinsia dhidi yao.

Ikumbukwe, Serikali ilitoa waraka kuhusu umuhimu wa school bus kuwa na wahudumu wa kike, (matron). Tunaendelea na tathmini.
Wanaoendesha magari ya wanafunzi wapimwe kwanza afya ya akili pamoja na kujua kama hawatumii madawa ya kulevya(Bangi, cocaine nk). Ahsante na hongera sana kwa kusimamia hili na mengine .Mungu akubariki uamkapo na ulalapo.
 
Back
Top Bottom